NOMAAA: Bwana Samatta Aendelea Kuonyesha Ulaya Uwezo Wake wa Kufumua Nyavu..Atundika Mabao Mawili Usiku wa Jana

MATANGAZO

MATANGAZO
Mbwana Samatta ameendelea kufanya vyemma kwenye ligi ya Ubelgiji baada ya kufunga magoli magoli mawili wakati Genk ikishinda ugenini kwa magoli 3-0 dhidi ya Lokeren.

Samatta alianza kufunga goli la kwanza dakika ya 34 kipindi cha kwanza kabla ya kufunga bao jingine dakika nne baadaye.

Bao la tatu la Genk limefungwa na Leon Bailey dakika ya 48 kipindi cha pili na magoli hayo yakidumu kwa dakika zote.

Samatta alipumzishwa dakika ya 73 kumpisha mshambuliaji mwenye ya Ugiriki Nikos Karelis.

Huupa chini msimamo wa ligi ya Ubelgiji (Belgium Pro League) ikionesha Genk ikikamata nafasi ya nne kikiwa na pointi saba baada ya kucheza michezo minne.