Showing posts with label UDAKU. Show all posts
Showing posts with label UDAKU. Show all posts

Bata la Zari Dubai lawachanganya wengi



 DAR ES SALAAM: Wakati suala la mzazi mwenzake Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kutanua pande za Dubai likidaiwa kuwezeshwa na kigogo mmoja, imebainika tofauti na maneno ya watu mitandaoni.

Kwa takriban wiki moja na zaidi, Zari ameonekana Dubai akiwa na wanaye wakubwa watatu, wakila bata katika viunga mbalimbali vya kuponda raha hali iliyofanya watu wengi kutoa maoni yao mitandaoni.
Kuna baadhi ya watu walimsifia kwa kueleza kuwa anachokifanya ni sahihi kwani anao uwezo wa kifedha hivyo kula bata si tatizo, tofauti na wanawake wenzake waliowahi kutoka na Diamond, Wema Sepetu na Hamisa Mobeto.
Kuna wengine walimponda kwa madai kuwa fedha hizo anazotumia, si zake bali kuna kigogo anayemwezesha hivyo asijishebedue na kuwarusha roho kina Wema na Mobeto.
Risasi Jumamosi lilifanikiwa kuzungumza na mtu wa karibu na Zari ambaye aliomba hifadhi ya jina na kubainisha, licha ya Zari kuwa na fedha zake lakini nyuma ya safari yake hiyo, yupo mdhamini anayemwezesha.Alisema, safari hiyo Zari amedhaminiwa na kampuni moja (jina kapuni) ambaye ndiye anayempa jeuri hiyo.
“Watu hawajui tu. Nimeona wanasema mengi sana mitandaoni, ooh sijui kuna kigogo sijui Zari hana pesa ya kukaa Hoteli ya Dusit Marina pale Dubai, kwanza watambue Zari ana fedha.
“Mtu anamiliki mashule, ana maduka Afrika Kusini atashindwa kulipia hoteli shilingi milioni tano kwa siku? (Chumba cha hoteli hiyo gharama yake kwa siku ni kati ya shilingi laki 5 na milioni moja na ushee),” alisema mtu huyo wa karibu na Zari.
Kama hiyo haitoshi, mtu huyo aliweka bayana kuwa licha ya kujimudu kifedha, safari hiyo Zari alidhaminiwa na ndio maana hata picha alizoposti kwenye mtandao wa Instagram, amewataja wadhamini.
Risasi Jumamosi liliingia kwenye kurasa mbalimbali katika mtandao wa Instagram na kukutana na kampuni hiyo iliyomdhamini Zari.
Hadi tunakwenda mitamboni juzi, imeelezwa kuwa Zari pamoja na wanaye watatu wakubwa pamoja na kijana mwingine, walikuwa bado wapo Dubai wakitumbua maisha.
Read More

Nandy: Huwa Napuuza kwa Kumuonesha Anachofanya ni cha Kijinga

Hitmaker wa ngoma ‘Kivuruge’, Nandy a.k.a African Princess amesema moja ya vitu asivyovipenda katika muziki wake ni kuingia katika beef na msanii mwingine.

Muimbaji huyu ameiambia Clouds TV kuwa yeye sio msanii wa kupenda ugomvi na yeyote anayetaka ugomvi kwake huwa anampuuzia.

“Mimi sio mtu wa ugomvi wa mara kwa mara kwa hiyo sitamani kuingia kwenye ugomvi na mtu.
" Huwa napuuzia kwa kumuonyesha kuwa anachokifanya ni cha kijinga sifuatili, yaani Simuonyeshi kuwa nimeshtushwa na kitu ambacho anakifanya au labda nakifuatilia,” amesema Nandy.

Utakumbuku kumekuwa na stori zinazodai kuwa Nandy na Ruby wana beef, hata hivyo wote wawili wamekuwa wakikanusha hilo kila wanapoulizwa na vyombo vya habari.
Read More

Harmonize Afungukia Kuvunjika Kwa Mahusiano Ya Zari na Diamond

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Harmonize kwa mara ya kwanza amefungukia suala la kuvunjika kwa Mahusiano ya Zari na Diamond Platnumz.

Miezi miwili iliyopita siku ya wapendanao Zari alitumia ukursa wake wa Instagram kumwaga aliyekuwa mpenzi wake Diamond baada ya kuzidisha michepuko ingawa suala hilo lilitokea muda mrefu uliopita lakini mpaka leo linatrend.

Harmonize mbali ya kuwa msanii wa Diamond lakini pia ni mtu wa karibu ambaye pia alikuwa na ukaribu na Zari kwaiyo alipoulizwa anachukuliaje wawili hao kuachana alisema anaheshimu maamuzi ya Zari.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Funiko Base ya Radio Five, Harmonize amefunguka na kusema kuwa yeye binafsi anaheshimu maamuzi ya Zari kwa sababu ana maamuzi yake binafsi.

"Mimi naheshimu sana maamuzi ya mtu siwezi kuongea kama ni vibaya au ni vizuri Kwanza muda wa kumshauri mtu kuhusu Mahusiano Yake ndio sina”.

Lakini pia Harmonize alisisitiza kuwa hawezi kumuongelea sana Zari na kuorodhesha mambo ambayo alimsaidia kwani unaweza ukaonekana mnafki.
Read More

Nisha Akana Skendo Ya Kumtongoza Young Dee

Muigizaji wa Bongo movie  Salma Jabu 'Nisha'   anayefanya vizuri hivi sasa na ngoma yake ya Bachela amejibu tuhuma alizotupiwa kuwa ana Mahusiano ya kimapenzi na msanii wa Bongo fleva Young Dee.

Siku ya Alhamis msanii wa Bongo fleva Amber Lulu alitoboa Siri na kusema kuwa kipindi ana Mahusiano ya kimapenzi na Young Dee, mwanadada Nisha alikuwa anamtongoza Young Dee.

Amber Lulu aliweka wazi kuwa jambo hilo lilikuwa la wazi hadi alikuwa ana ushahidi kwani alikamata meseji za wawili hao huku akikiri kuwa Nisha ni fundi wa mapenzi maana alikuwa anampa maneno matamu Young Dee.

Baada ya kutupiwa tuhuma hizo Enews ya EATV ili mtafuta Nisha kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo na moja kwa moja alikataa na kusema kuwa hajawahi kuwa na Mahusiano na Young Dee zaidi ya urafiki:

"Mimi sina Mahusiano na Young Dee ila kilichotokea ni kwamba nilikuwa nataka kuingia kwenye muziki hivyo  Young Dee kama msanii wa Bongo fleva alikuwa ananisaidia na lazima niwe karibu na wasanii we zangu.

" Alafu mimi nimemjua Young Dee kabla hata hajawa na Mahusiano na Amber Lulu kwaiyo ni mtu wangu wa karibu na trust me angekuwa mpenzi wangu nisingeweza kuficha maana mimi nikipenda nataka watu wote wajue”.
Read More

Shilole Achora Tatoo ya Mwisho Yenye Jina la Mumewe

Mwanamuiki wa kike ambae pia ni mjasiriamali, Shiloleh ameonyesha tatoo aliyochora kwenye mwili wake yenye jina la mume wake mpendwa uchebe yenye jina ‘ASHRAF‘  na kusema kuwa hiyo ndio tatoo yake ya mwisho kuichora katika mwili wake.

Katika ukurasa wake wa instagram , Shilole aliandika;“Kwa mara ya kwanza na ya mwisho nimechora tatooooo ya jina la mume wangu Nampendaa sana”

Shilole aliwahi pia kuchora tattoo ya aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Nuh Mziwanda na baadae kuifuta na hii itakuwa tattoo yake ya pili kuichora yenye jina la mwanaume ambae ni mpenzi wake na kuionyesha hadharani..

Read More

Fahamu Mambo Yanayomfanya Mume/ Mchumba Wako Akupende Zaidi


Wapo baadhi ya wanawake hudiliki hata kutumia dumba hii yote ikiwa kuwafanya wanaume zao wawapende, lakini wengi wao wamesahau ya kwamba kufanya hivo sio chachu ya kufanya mahusiano hayo yakue bali ni kuyadidimiza.Lakini ukweli kwamba mambo ya libwata yamepitwa na wakati katika karne hii hivyo ili mumeo akupende zaidi katika mahusiano yenu unatakiwa kufanya yafautayo;

1. Muamini mmeo au mchumba wako.

2. Usimkatishe tamaa katika maono yake.

3. Usimlazimishe kupenda mambo unayoyapenda.

4. Kila wakati kila unapo tatizo ni vyema ukamwambia kuliko kusema kwa wengine.

5. Usidhani kwamba hawezi kutambua uwepo na uzuri wa wanawake wengine hivyo mfanye awe karibu nawe ilia one thamani yaw ewe pekeee..

6. Usilazimishe kuwajibika juu ya mambo yako: Kama vile kwenda saluni, umeme, vocha na mambo mengine hasa kama bado mko katika mchakato wa uchumba, kama atafanya hivyo mwache afanye mwenyewe msimlazimishe eti kwa sababu shosti wako huwa anafanyiwa hivyo na wewe unataka, ladies huo ni utoto.
Read More

Unatafuta Mwenzi wa Maisha Yako? Soma Hii Inakuhusu Sana

Ni kawaida watu kudhani kwamba kama zawadi imefungwa kwa kabrasha au mfuko au package nzuri sana basi kilichomo ndani kitakuwa ni kitu chenye thamani kubwa sana na kizuri sana.

Ukweli ni kwamba ufungaji wa zawadi au uzuri wa material yanayotumika kufunga zawadi haviwezi kukwambia uhakika wa uzuri wa kitu kilichomo ndani, badala yake unahitaji kufikiria zaidi, au kufanya utafiti zaidi ya hayo makabrasha ya kufungia zawadi ili kujua kilichomo ndani.

Linapokuja suala la mahusiano, hasa mahusiano mapya, watu wengi huwaangalia partners wao kwa nje bila kuangalia undani wa mtu mwenywe ili kujua ndani kuna kitu gani.
Wengi huvutiwa na uzuri wa nje au sifa za nje badala ya kuangalia na kuchunguza kile kilichomo ndani ya huo uzuri.
Watu hawaoni sababu ya kuchunguza au kutumia muda kupata ukweli na matokeo yake ni kujuta mbele ya safari.

Siku hizi si ajabu ukakuta mtu ameshakubaliana na mtu hadi kufika hatua ya mbali sana katika mahusiano bila hata kujua majina yote mawili ya mtu ambaye anasema anampenda na kwamba bila yeye anaona maisha hayana maana.
Watu wanafahamiana na baada ya mwezi tayari wanakubaliana kuoana na kuwa mke na mume.

Unahitaji ku-dig deeper linapokuja suala la mahusiano,
Utajiri, Kujulikana, Cheo, Urembo, Uzuri wa ngozi,
Familia yenye uwezo, Vipaji, Usomi, Umaskini au
kitu chochote cha nje ni sawa na kabrasha ambalo linatumika kuibeba zawadi yenyewe.

Inaweza kuwa zawadi ni makaratasi na matambala tu yamewekwa humo na utakapokuja kugundua unakuwa umeshachelewa kabisa na matokeo yake kujuta.
Umeuziwa mbuzi kwenye gunia.
wakati unao fikiria kwa makini

Kawaida kama unatafuta uhusiano wa kudumu ni vizuri uka-invest muda mwingi kuhakikisha unamfahamu mtu vizuri, moyo wake
(marry the soul not the skin).

Maisha tunapoishi hupelekea mabadiliko ya sifa za nje, watu hufirisika, watu hunyonyoka nywele, watu huzeeka, watu hupata stress, watu huwa vilema, watu hunenepeana, watu huugua, watu hubadilika, watu hukonda hata wakawa tofauti na walivyo labda wakati wa kuanza urafiki wenu muwe mmekubaliana kwamba yakitokea mabadiliko tu kila mtu aanze mbele au achukue chake, ndo maana leo ndoa ni kama watu wanaoenda shopping
Read More

Zijue sifa za mpenzi asiyekupenda kwa dhati


Watu wengi hawapendi kutambua kwamba mtu anayempenda yeye hampendi, kwasababu ni maumivu makubwa sana moyoni. Unapokuwa kwenye mahusiano na mtu huyo nae inamuwia vigumu kukwambia "sikupendi" hufanya hivi katika kuzihurumia hisia zako juu yake.

Hivyo ukiona dalili hizi zifuatazo lazima ujue kwamba uliyenaye hakupendi.

1. Anapokuwa nawe inamuwia vigumu sana kukwambia neno NAKUPENDA mara kwa mara, utajikuta wewe ndio unakuwa mtumwa kwake kwa kumwambia nakupenda kila mara.
Majibu yake baada ya neno hilo, mara nyingi atakwambia asante kwa kunipenda basi, na akikuhurumia sana atakwambia nakupenda pia ili kukuridhisha wewe na moyo wako.

2. Utajikuta una mawazo sana juu yake na kujiuliza "hivi kweli mtu huyu ananipenda?"
Utajaribu kumuuliza, "je unanipenda?"
Jibu lake kwanza litafikiriwa sana, sababu ya kufanya hivyo ni kwa vile anatambua kwamba hakupendi sasa kukwambia ukweli wa swali lako anahisi utaumia, kwahiyo baada ya swali hilo anaweza kukuuliza swali na wewe "kwani unaonaje?" kwavile unampenda sana utamjibu, "naona kuwa unanipenda" naye atakwambia "basi ndio hivyo".

Mara nyingine baada ya wewe kumuuliza swali kuwa je anakupenda kweli, atakujibu "ukweli unaujua ila kwanini unapenda kuniuliza swali hilo kila mara?" kama umeshaingiza dosari juu ya upendo wake utajikuta unamuuliza "ukweli upi?" naye atakujibu "kuwa nakupenda", hapo utajikuta umepata furaha kugundua kuwa anakupenda kumbe mwenzio amekuhurumia tu.

3. Huwa hajali mambo yako unayomwambia, ukimueleza muda huu badae anajifanya kusahau ili tu akupotezee mueleleo.

4. Unapopanga kukutana nae huwa ni mtu asiyeishiwa na sababu za kushindwa kufika, huwa na aibu ya kukutambulisha kwa watu.
Unaweza kufika nae mahali akakwambia kuwa "kuna watu wanafahamiana na mama/baba mahali hapa kwahiyo tusiongozane karibu", hapo anaweza yeye akatangulia mbele au kukuacha wewe utangulie.

5. Hufanya tabasamu la kuigiza au kicheko cha kejeli ili wewe uridhike kwamba anafurahishwa na uwepo wako kwake.

6.Wakati mwingine inampasa mtu kujitambua na kumpa uhuru huyo umpendaye aweze kuamua mwenyewe labda kuendelea na wewe au kumfata anayempenda yeye.
Cha muhimu ni kuwa using'ang'anie mahusiano ambayo yanayoumiza moyo kwani yanaweza pasua moyo wako kwa mawazo.
Read More

Ebitoke ajibu ishu ya kumsaliti Ben Pol na kutembea na Shemeji yake

Mchekeshaji kutoka kundi la Timamu, Ebitoke amejibu tetesi za kutoka kimapenzi na Wyse ambaye ni msanii anayesimamiwa na Ben Pol.

Utakumbuka kuwa Ebitoke na Ben Pol kwa kipindi kirefu sasa wamekuwa wakieleza kuwa wao ni wapenzi hivyo, Wyse ni shemeji yake na Ebitoke.

Mchekeshaji huyo amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote kwani mapenzi yake na Ben Pol bado ni ya moto kabisa na picha zilizotoka wakiwa wana-kiss ni katika kutengeneza video ya Wyse.

“Director alituambia tu-kiss ili kuvaa uhalisia ila kati yangu na Wyse ni urafiki hakuna mapenzi,” Ebitoke ameiambia Bongo5.

Muimbaji Wyse anasimamiwa na Ben Pol na kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Siamini’, pia alishirikishwa na Ben Pol katika wimbo wake uitwao Bado Kidogo.
Read More

Mwanadada Kutoka Kenya Ajitolea Kumsaidia Wema kupata Mtoto.

Ni muda mrefu sasa umepita tangu mwanadada wema sepetu akiwa analalamika na kuonyesha kiu yake ya kupata mtoto , baadhi ya watu wamekuwa wakimuonea huruma na wengine kumsema na kumtukana lakini mwanadada huyo hajawahi kuacha kuonyesha kiu yake ya kutaka kupata mtoto.

Akiongea katika chaneli ya EATV,Wema anasema “kwakweli nimekuwa nikitamani kupata mtoto hata leo kwa muda sasa tangu nikiwa na miaka 24 hadi leo nina miaka 29”

Hata hivyo moja ya warembo kutoka kenya aliyekuwa akiishi dubai anaejulikana kwa jina la 2g diva, amejitolea kumsaidia wema kupata mtoto ili kuweza kutimiza ndoto zake za muda mrefu.

Katika moja ya video zilizovuja mtandaon zikimuonyesha dada huyo akiongea anasema kuwa ” wema sepetu darlin suluhisho tunalo, may be unaenda kuwa mama soon”
Read More

Kajala afunguka kuongeza mtoto wa pili na mipango ya mwanae

Msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja amesema hatarajii kabisa kuwa mwanae, Paula ataingia katika tasnia ya burudani nchini.

Muigizaji huyo ameiambia Planet Bongo ya EA Radio mwanae ana mpango wa kuwa mwanasheria na si nje ya hapo.

“Hivi vitu industry, sijui radio, muziki, movie hapana , hayupo interest kabisa yeye kila siku anaseama anataka kuwa mwanasheria, kwa hiyo tunasubiria amalize shule tuwe na mwanasheria mkali,” amesema.

Alipoulizwa kuhusu kuongeza mtoto wa pili, alijibu; “Mungu akijalia atotokea mwingine tu soon,”.
Read More

Maajabu: Tajiri Aliyeshinda Mnada Nyumba za Lugumi kwa Blioni 3.3 Anaishi Nyumba ya Kupanga....Kodi Kwa Mwezi ni 50,000

Wakati maswali mengi yakijitokeza kuhusiana na Dk. Louis Shika, ambaye aliibuka mshindi katika mnada wa nyumba za kifahari za Said Lugumi zilizoko Mbweni JKT na Upanga jijini Dar es Salaam kwa thamani ya jumla ya Sh. bilioni 3.3, imebainika kuwa anaishi katika chumba kimoja cha kupanga.

Imebainika  kuwa  Dk. Shika anakaa kwenye nyumba hiyo iliyopo Mtaa wa Amani kwa kipindi cha takribani mwaka mmoja sasa na kodi anayolipa kwa mwezi ni takribani Sh. 50,000.

Aidha, baadhi ya majirani zake wamemuelezea kuwa ni mtu asiye na makeke, huku baadhi wakidai kuwa aliwahi kuwaahidi wauza mihogo ya kukaanga walio jirani na mahala anapoishi kuwa atawaunganishia kupata mikopo nafuu ili wakuze biashara zao, lakini bila ya kuwatajia taasisi atakayowaunganisha nao. Inadaiwa kuwa vilevile, kwa baadhi ya watu hufahamika kwa jina la ‘profesa’.

Dk. Shika alijipatia umaarufu katikati ya wiki baada ya kuibuka mshindi katika mnada wa nyumba za kifahari za Lugumi, kwa kununua nyumba moja ya Mbweni kwa Sh. bilioni 1.2, nyumba ya pili iliyoko pia Mbweni Sh. milioni 900 na nyumba ya tatu iliyoko Upanga alishinda na kutaka kununua kwa Sh. bilioni 1.2.

Hata hivyo, alishindwa kutumiza masharti ya kulipa asilimia 25 ya fedha kwa kila nyumba baada ya kushinda, hivyo kujikuta akitiwa mikononi mwa vyombo vya dola kwa kuharibu mnada.

Katikati ya wiki hii, jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, lilimtia nguvuni Dk. Shika kutokana na tuhuma za kuharibu mnada huku likidai kuwa linafanya uchunguzi zaidi ili kubaini kwa nini alifanya hivyo.

Mbali na kuchunguza juu ya hatua ya kuharibu mnada, kamanda wa kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alisema walikwenda nyumbani kwake kufanya upekuzi sambamba na kuchunguza udaktari wake. Shika aliwahi kukaririwa kuwa ni msomi wa shahada ya uzamivu (Ph.D).

Hata hivyo, Mambosasa alisema udaktari wake huo unatia shaka kwa kuwa ameshindwa kuonyesha vielelezo kuthibitisha kama anastahili hadhi hiyo.
Read More

Kijana Anyofolewa Ulimi na Mwanamke Wakati Wakipigana Denda


Mkazi wa Mandewa, Manispaa ya Singida, Said Mamba (24), amelazwa katika hospitali ya mkoa mjini Singida baada ya kung’atwa theluthi tatu ya ulimi wake na mwanamke waliyekuwa wakinyonyana ndimi. 

Tukio hilo la aina yake lilitokea Septemba 12, saa 3:30 usiku wa sikukuu ya Idd el Hajj. 
Mamba, ambaye hawezi kuzungumza ametoa maelezo ya tukio hilo kwa njia ya maandishi. 

Alisema siku ya tukio alikutana na mwanamke huyo kwenye grosari iliyopo eneo la Mandewa na baadaye mwanamama huyo alimwomba amsindikize nyumbani kwake. 
“Nilikubali kumsindikiza, tukiwa njiani aliniomba tufanye mapenzi. Nilipokataa alinilazimisha na baada ya kuona sitaki aliomba tuagane kwa kunyonyana ndimi, nilikubali ombi hilo,” alisema. 
Mamba alisema wakati wakiendelea, mwanamke huyo alianza kumvua mkanda wa suruali lakini alimzuia ndipo alipomng’ata ulimi na kuondoka na kipande. 
Mzazi wa Mamba, Fatuma Alli alisema alipata taarifa ya tukio hilo baada ya siku tatu na kwamba, siku hiyo hiyo mume wa mwanamke aliyetenda kitendo hicho alikwenda kwake akieleza kijana huyo alijaribu kumbaka mkewe. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Peter Kakamba, alisema hana taarifa za tukio hilo. 

Daktari wa meno wa hospitali hiyo, Dk Hamisi Kakandilo alisema ulimi wa kijana huyo hauwezi kutibika isipokuwa kuusafisha ili asipate maambukizi. 

“Hata kama kipande kilichotolewa kingepatikana kisingeweza kushonwa,” alisema.
Read More

Esma Platnumz Akiri Kupagawa Sana na Penzi la Petit Man Awaomba Nyaku Nyaku Wasimyakue


Dada wa Diamond ameamua kufunguka ya moyoni na kudai anampenda sana mume wake Petit Man ambae walitengana kwa muda kutokana na kutokuelewa hapa na pale lakini kwa sasa inaonekana wameweka mambo sawa...Ameandika haya kwenye ukurasa wake
_esmaplatnumz
Baby dady mkimuona mwambieni mi Nampenda tuu ukiniuliza hata sijui... kuna wakati unaweza kufichaficha au kujionesha hupendi au ukajikaza usiseme unachojisikia kusema but mi naona bora uwe muwazi ili roho yako Iwe na Amani... Jamani mi Nampenda huyu kaka plz nyakunyaku kuweni makini huyu mi nahisi km kafika kigoma mwisho wa reli...na natania msije nikomoa...hamchelewi...

Read More

Barakah Da Prince Akiri Kimombo Kwake Bado ni Tatizo, Aanza Mpango wa Kutafuta Mwalimu


Msanii wa muziki Barakah Da Prince amekiri kuwa lugha ya Kiingereza kwake ni tatizo huku akiweka wazi mpango wa kutafuta mwalimu wa kumfundisha.

Muimbaji huyo ambaye ameachia wimbo ‘Nisamehe’ hivi karibuni akiwa amemshirikisha AliKiba, amesema katika interview yake kubwa iliyopita na MTV aliomba kutumia lugha ya Kiswahili kwa kuwa ndio lugha ambayo anaweza kuizungumza.

“Niliulizwa kwenye interview ya MTV kama naweza kuongea Kiingereza, nilichowajibu naweza ila sio Kiingereza kilichonyooka ndio maana nikatumia Kiswahili. Nafurahi kwa kuwa walivutiwa na Kiswahili,” Barakah alikiambia kipindi cha Uhondo cha EFM Jumanne hii.

Pia muimbaji huyo amesema mpenzi wake wa sasa Naj ameshindwa kumfundisha huku akiweka wazi mpango wa kutafuta mwalimu.

“Hanifundishi lugha kwa sababu tuna masihala mengi hivyo nahitaji mtu ambaye atakuwa serious,” alisema Barakah.

Diamond ni miongoni kati ya wasanii ambao walikuwa hawajui kuongea lugha ya Kiingereza lakini alijifunza na sasa anakichapa kama kawaida.

Bongo5
Read More

Walichofanyiana Shilole na Nuh Mziwanda walipokutana kwenye basi la Fiesta


Shilole na Nuh Mziwanda walikutana kwenye basi walipokuwa wanaenda Fiesta, wasanii hawa wamekuwa na bifu na walichuniana walipokutanishwa kwenye kipindi cha tv clouds na wamekuwa wakipigana majungu mitandaoni.
Lakini walipokutana kwenye basi Shilole alimuambia Nuh Mziwanda yaishe na kumwambia yupo kwa ajili yake na kumwagia mabusu mazito, pengine watarudiana. Angalia:

Read More

Kutana na Mtangazaji Mchafu Zaidi Duniani


Raphael Tenthani inasemekana kuwa ndiye mtangazaji mchafu zaidi kutokea duniani

Raphael mara zote utakazo kutana nae huwezi ukamkuta nadhifu , mara kwa mara utamkuta amevaa nguo zilizo chakaa na muda mwingine nguo zenye matobo au viraka

Raphael ingawa ni mwandishi wa habari katika shirika la habari la BBC nchini malawi lakini kwenye suala la usafi yeye limemkalia kushoto sana ,wakati mwingine unaweza ukakutana nae nywele hajachana, viatu vimeachama , mdomo unanuka na mara kwa mara anakuwa katika hali ya ulevi

Raphael amekuwa gumzo sana katika mitandao ya kijamii huku wengi wakimuhisi huenda anafanya hivyo ili asivunje masharti ya mganga

Ni kawaida kumuona Raphael akirusha habari akiwa mchafu bila kujali mahali husika alipo kuwepo.
Read More

Wema Sepetu kuzindua bidhaa yake mpya ya viatu vya kike kwenye show yake ya vigoma Tanga


Malkia wa filamu Wema Sepetu ametumia show yake ya vigoma iliyofanyika Jumamosi hii katika Viwanja vya Mkwakwani mkoani Tanga kuzindua bidhaa yake mpya ya viatu vya kike.
Mwigizaji huyo ambaye mwishoni mwa mwaka jana alizindua bidhaa yake ya kwanza ya lipstick, amesema bidhaa hiyo itaanza kupatika madukani hivi karibuni.

“Wakati naanza kutumia jina langu kwa ajili ya kuendeleza brand yangu ya Wema Sepetu, nilianza na lipstick na sasa nimekuja na viatu vya kike,” alisema Wema mbele ya umati wa watu waliojitokeza katika usiku wa vigoma. “Hivi viatu ni vya kitamaduni kabisa kwa sababu wanasema uzalendo kwanza,”

Aliongeza, “Kwa hiyo nilisema nifanye kitu gani ambacho kitawakilisha na uzinduzi wa hivi viatu, nikasema niandae show ya usiku wa kitu fulani, kwa hiyo nilivyokuwa nataka kuzindua hivi vitu nikasema nitumie akili, nifanye usiku wa Kiswahili, kwa sababu hata hivi viatu vinaenda Kiswahili, nikafikiria usiku wa vigoma, tumeanza Dar es salaam na kutaamua tuje Tanga na baadae mikoa mingine,”.

Mwigizaji huyo amesema anaamini akizunguka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ataweza kupata support kubwa kwenye bidhaa zake pamoja na kazi zake za filamu.
Read More

Shepu ya Snura yamdatisha Reyvanny Kitandani Wakati wa Ku-Shoot Video


Baada ya kutoka video ya “Natafuta Kiki” pamekuwa na zengwe, kwa kile kilichoonekana kuwa ni mahaba juu ya Snura na Rayvanny kwa lile denda zito lililopigwa kitandani.
Akipiga stori na eNewz Rayvanny amesema “Ni kweli ile scene ya kitandani ilinipa wakati mgumu sana, hasa ukizingatia ile shepu ya Snura, kuna wakati nilisahau kama tuko location”.

Lakini kwa upande wa Snura anasema yeye aliifanya ile scene kama kazi tu, kama ambavyo script ilimtaka afanye ndicho alichokifanya, na wala hakumtamani Ray.

Snura kwa ujasiri akaongeza kwa kusema “Kama script inataka nimkiss hata mwanangu ninaweza kufanya hivyo”.

Lakini pia kwa upande mwingine Ray alipoulizwa juu ya sababu za kutumia video aliyojishut na Wema katika birthday ya Romy Jones, alisema “Sina tatizo kabisa na Wema na tokea zamani nilitamani sana Wema aonekane kwenye hii video yangu, lakini ilishindikana kumpata sababu ya u-bize wake hivyo nikaona bora nitumie tu ile video tukiwa kwenye birthday ya Romy Jones”.
Read More

Picha 17: JAMAA ANAYEDAIWA KUFANYA MAPENZI NA WAKE ZA WATU KICHAWI SHINYANGA AKAMATWA,ASHUSHIWA KIPIGO



Wananchi wenye hasira kali katika kijiji cha Bugayambele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga wamemshushia kichapo jamaa anayedaiwa kuwaingilia wanawake nyakati za usiku kisha kufanya nao mapenzi kwa njia za kishirikina.

Tukio hilo limetokea leo majira ya saa kumi jioni ambapo wakazi wa kitongoji cha Bugayambelele jirani na kijiji cha Nhelegani kilichokumbwa na taharuki ya kuwepo mtu anayefanya mapenzi na wake za watu kimazingara,walimshtukia jamaa huyo baada ya kuonekana akifanya vitendo walivyodai kuwa vya kishirikina katika familia mbili za kitongoji hicho.

Malunde1 blog baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa tukio hilo ilifika eneo la tukio haraka zaidi na kushuhudia umati mkubwa wa watu ukiwa umemzingira jamaa huyo huku askari polisi wakiwa eneo la tukio kuzuia wananchi wasiendelee kumshushia kipigo jamaa huyo.

Wakazi wa eneo hilo walisema mtu huyo aliingia kwenye nyumba mbili(kaya mbili) bila kupiga hodi huku akidai kuwa alikuwa anatafuta mke wake, akidai kuwa ametoka kwa mganga wa kienyeji kaelekezwa kuwa mke wake yupo eneo hilo.

Hata hivyo baada ya kumtilia mashaka jamaa huyo alianza kukimbia na kutupa simu zaidi ya tatu za mkononi alizokuwa nazo,wananchi wakafanikiwa kumkamata kisha kumpeleka kwenye mkutano wa sungusungu na walipompekua wakamkuta na dawa za kienyeji zinazodaiwa kuwa za mapenzi,zikisomoka kama ifuatavyo;

“Imala yose -kuchoma kuomba mke wako roho yake irudi kwako akupende” na nyingine maandishi yakisomeka kuoga na kuchoma kuomba mkeo akupende na arudi kwako”.
 
Wakazi wa eneo hilo walisema kutokana na maelezo yake,pia kuingia katika familia moja bila hodi huku akidaiwa kupotea kimiujiza eneo hilo na kuibukia katika familia nyingine pamoja na dawa za kienyeji alizokuwa nazo walimhusisha moja kwa moja na tukio la ubakaji kwa njia za kishirikina.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Bugayambelele Donald Francis alisema alipigiwa simu na kuelezwa kuwepo kwa mwanamme anayehusishwa na tukio la kubaka wanawake kishirikina katika kijiji jirani cha Nhelegani kata ya Kizumbi.
 
Alisema mwanamme huyo alikutwa na dawa za kienyeji huku akitoa maelezo yasiyoeleweka ikiwemo kudai amefika hapo kwa ajili ya kutafuta kazi ya kufyatua matofali,kutafuta mke wake na anatoka kwa mganga wake wa kienyeji aliyemnyweshwa dawa za ajabu.
Tutawaletea taarifa kamili hivi punde....

Mwanamme aliyejitambulisha kwa jina la Shaban Charles kutoka Kitangiri katika manispaa ya Shinyanga anayedaiwa kujihusisha na vitendo vya kubaka wanawake kishirikina nyakati za usiku-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Polisi wakiwa eneo la tukio


Wananchi wakiwa eneo la tukio

Dawa za kienyeji alizokutwa nazo jamaa huyo

Dawa za kienyeji za jamaa pamoja simu yake

Dawa za kienyeji

Polisi na wananchi wakiwa wamemzunguka jamaa huyo

Mwandishi wa habari wa Radio Faraja Steve Kanyeph akifanya mahojiano na jamaa huyo

Wananchi wakiwa eneo la tukio

Wananchi wakiwa eneo la tukio

Gari la polisi likiwasili eneo la tukio


Jamaa akipanda kwenye gari la polisi

Baiskeli ya mtuhumiwa ikipandishwa kwenye gari la polisi


Polisi wakiondoka na mtuhumiwa

Wananchi wakiondoka eneo la tukio
Mwenyekiti wa kitongoji cha Bugayambelele Donald Francis akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema alipigiwa simu na kuelezwa kuwepo kwa mwanamme anayehusishwa na tukio la kubaka wanawake kishirikina katika kijiji jirani cha Nhelegani kata ya Kizumbi.
Read More
Powered by Blogger.

Hot

© Copyright KAHAMA 24