Asakri MTWARA waagizwa kupambana na wahalifu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi MWIGULU NCHEMBA amewaagiza askari polisi wa mkoa wa MTWARA kupambana bila kuchoka na uhalifu wowote
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi MWIGULU NCHEMBA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi MWIGULU NCHEMBA amewaagiza askari polisi wa mkoa wa MTWARA kupambana bila kuchoka na uhalifu wowote unaojitokeza katika maeneo yaoWaziri NCHEMBA ametoa agizo hilo katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani MTWARA wakati wa mkutano wake na askari wa Jeshi la Polisi, Jeshi la Uhamiaji, Jeshi la Magereza na Jeshi la Zimamoto
Kwa upande wao Kamanda wa Polisi wa mkoani wa MTWARA, - HENRY MWAIBAMBE na Kamanda wa Jeshi la Uhamiaji mkoani humo ROZI MHAGAMA wamesema kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni pamoja na uhaba wa mafuta na magari ya kusafirisha mahabusu
Pamoja na mambo mengine ,Waziri huyo wa Mambo ya Ndani ya Nchi MWIGULU NCHEMA amesema kuwa anatambua changamoto zinazowakabili askari hao na kuahidi kuzifanyia kazi.
No comments:
Post a Comment