Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Waziri Mwakyembe Awaasa Watanzania Kupambana Na Viashiria Vinavyo Sababisha Mauaji Ya Kimbari

Na: Mwandishi wetu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe, amewaasa Watanzania kuhakikisha wanapambana na viashiria vyote vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani na mauaji ya kimbari. Kauli hiyo  Dkt. Mwakyembe ameitoa wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu za mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda miaka 24 iliyopita.

Kwenye hotuba yake Dkt. Mwakyembe amesema mauaji ya kimbari hayatokei ghafla bali huanza kwa chokochoko na kauli za kichochezi ambazo zina lengo la kuigawa jamii vipande vipande. 
“Kilichotokea Rwanda ni fundisho kwetu, mauaji ya kimbari hayatakiwi kutokea tena. Kuhakikisha hayatokei lazima tuyadhibiti mambo yote yanayoweza kuligawa taifa kwa faida ya kizazi cha leo, kesho na keshokutwa” Dkt. Mwakyembe alisisitiza.

Kuendelea kutia mkazo wa ujumbe wake Dkt. Mwakyembe aliinukuu kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, aliyoitoa wakati wa ziara yake ya kikazi nchini Rwanda  ambapo alisema “haya hayatatokea tena, hatuwezi kubadili kilichotokea awali, lakini tunaweza kubadilisha hali ya leo na hata ya baadae”.

Balozi wa Rwanda nchini mheshimiwa Eugine Kayihura ameishukuru Serikali na wananchi wa Tanzania kwa kuendelea kuwa pamoja na Wanyarwanda. Pia ameahidi kuendeleza ushirikiano wa kindugu kati ya Tanzania na Rwanda kwa maendeleo ya watu wake.

Kwa upande wake Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez amesema nchi zote zina wajibu wa kuwalinda wananchi wake dhidi ya mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. Pia zinatakiwa kuhakikisha zinaungana kupambana na mtu au kikundi chochote chenye nia ya kutekeleza uhalifu kama huo.

Kumbukumbu za mauaji ya kimbari ya Rwanda huadhimishwa kila mwaka na mwaka huu maadhimisho hayo kwa Tanzania yamefanyika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City ambapo Dkt. Mwakyembe alikuwa mgeni rasmi. Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, watu mashuhuri, viongozi wa serikali na mashirika ya kimataifa na wanafunzi wa shule za sekondari za jijini Dar-es-salaam
Read More

Meya aliyesifiwa na Rais afunguka kuhusu kuhama


Meya, Wajiji la Arusha, Kalista Lazaro (CHADEMA) amefunguka na kusema kitendo cha Rais kumsifia mbele ya hadhara ni heshima kwake na viongozi wa Arusha na kusema hakuna sababu kiongozi aliyechaguliwa na wananchi kuhama chama kwa kumuunga mkono Rais.

Kalista Lazaro alisema hayo April 7, 2018 baada ya Rais Magufuli kumsifia kuwa ni kati ya watu ambao wanapenda maendeleo na kufanya maendeleo katika jiji la Arusha Mjini licha ya kiongozi huyo kutokea katika chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

"Hii pongezi ya Rais ni kwa sababu alipokea taarifa ya utendaji ya jiji la Arusha na tangu alipoingia nilimweleza mambo ambayo tumefanya kwa mfano amepongeza jitihada kubwa ya ujenzi wa madarasa tangu mwaka 2016 ambapo tumejenga madarasa 105, 2017 tumejenga madarasa 61
"Tunapandisha vituo vya afya mara moja na dispensary kwa ujumla tano, hospitali ya wilaya, barabara za lami, barabara za vumbi na juzi tumetangaza tenda ya kilometa 10 za lami katika jiji la Arusha ambapo barabara ya Njiro, Kwa Mlombo, Sombetini zinaenda kujengwa lami pamoja na barabara ya Ngarenalo kwangu mimi ni heshima na hii heshima nimeipokea kwa niamba ya wananchi wa jiji la Arusha" alisema Kalista Lazaro

Aidha Kalista Lazaro amedai kupongezwa kwake kuwe funzo kwa viongozi wengine ambao wamekuwa wakihama kutoka CHADEMA na kwenda CCM kwa kigezo cha kuunga mkono serikali na kudai kuwa ukitaka kufanya hivyo unachotakiwa kutekeleza tu yale uliyoahidi kwa wananchi wako na si kwa kigezo cha kuhama chama.

"Wale ambao walikuwa wanabeza na hawatambui sasa wametambua kuwa Meya wao anapongezwa na Rais Magufuli mbele ya halaiki ya watu, mbele ya polisi, mbele ya Mkuu wa Majeshi hivyo Rais anaona kazi tunayofanya na niwaambie wananchi hakuna sababu ya kiongozi wa kuchaguliwa kuhama, ukitaka kutekeleza wajibu wako na kuunga mkono serikali unatakiwa ufanye kazi ambayo umeahidi wananchi wako. Mimi leo napongezwa nikiwa ndani ya CHADEMA, nikiwa Meya wa CHADEMA na diwani wa CHADEMA kwangu mimi ni heshima" alisisitiza
Read More

TUCTA Nao Wataka Watumishi Darasa la 7 Warudishwe Kazini

Baraza Kuu la Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) jana Jumamosi Aprili 7, 2018 limetoa tamko lenye mambo saba, likiwemo la kupinga uamuzi wa Serikali kuwafuta kazi watumishi wake wenye elimu ya darasa la saba.

Akisoma tamko hilo mbele ya wajumbe wa baraza kuu la Tucta katika mkutano wa baraza hilo uliofanyika mkoani Morogoro mwenyekiti wa Tucta, Tumaini Nyamhokya alisema uamuzi huo wa Serikali si sahihi na hivyo wametaka watumishi hao kurejeshwa kazini.

Alisema baraza limesikitishwa na uamuzi wa kuwaondoa kazini watumishi wa umma na taasisi zinazopokea ruzuku kutoka serikalini.

Nyamhokya alisema uamuzi huo si wa kisheria ikizingatiwa kuwa watumishi hao waliajiriwa kwa kufuata taratibu halali za ajira.

“Kwa hiyo Tucta tunaitaka serikali kutengua uamuzi wake na kuwarudisha watumishi hao kazini bila kupoteza haki zao za kiutumishi kwa kipindi chote,” alisema.

Mambo mengine sita yaliyopo katika tamko hilo wanayotaka yafanyiwe kazi ni; ongezeko la mishahara, kodi ya mishahara (PAYE), kupandishwa madaraja na vyeo kwa watumishi wa umma, malimbikizo ya mishahara kwa wafanyakazi na watumishi kwa baadhi ya taasisi, ucheleweshwaji wa malipo ya wastaafu kwa baadhi ya mifuko ya hifadhi ya jamii na uamuzi wa Serikali kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii.
Read More

Viongozi wa kitaifa,Wazungumzia maendeleo yaliyoachwa na Rais wa kwanza Z'bar

Viongozi wa Kitaifa kutoka Zanzibar na Tanzania Bara wamesema Watanzania wanaendelea kumkumbuka Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume kutokana na Maendeleo makubwa aliyoyafanya wakati wa Uongozi wake miaka minane na kufanikiwa kuacha historia isiyofutika kwa kufanikisha Mapinduzi ya Zanzibar na tukio la kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania April 26, mwaka 1964.

Viongozi hao wametoa kauli jhiyo jana kwa nyakati tofauti, muda mfupi baada ya kukamilika kwa shughuli ya kumbukumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume iliyofanyika katika ofisi kuu ya Chama cha Mapinduzi iliyopo Kisiwandui visiwani hapa.

Walisema yanayooneka hivi sasa Zanzibar yametokana na dira ya maendeleo iliyoachwa na Marehemu Abeid Amani Karume ya kuwaletea wananchi Maendeleo katika sekta mbalimbali kwa kuondosha matabaka na kufanikiwa kujenga umoja wa kitaifa pamoja na kuasisi Muungano ambao umevunja rekodi kwa kudumu zaidi ya miaka 50.

Kila ifikapo April 7 kila mwaka, Watanzania huadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Sheikh Abeid Amani Karume ambaye aliuwawa na Wapinga Maendeleo na kuacha simanzi na majonzi kwa wanaharakati wa ukombozi wa Bara la Afrika.
Read More

Baba Mzazi: 'Abdul Nondo babu yake ni muasisi wa TANU'

Abdul Nondo, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambaye anakabiliwa na kesi ya kujiteka mwenyewe, mzazi wake Omar amethibitisha kuwa baba yake alizaliwa mwaka 1919 huko Ujiji, Kigoma na kuwa ni miongoni mwa waasisi wa chama cha Tanu.

Mzee Omar, alisema baba yake huyo aliyemtaja kwa jina la Omar Kagobe alipata watoto 30, mmoja akiwa yeye.

“Nashangaa hao wanaomkamata na kumhoji mtoto wangu kuwa sio raia, wananichekesha sana kwa kuwa najua mwisho wa siku watajua ukweli wake. Ukweli ni kwamba wazazi wangu ndio waasisi wa Tanu na walishiriki kikamilifu katika kupigania uhuru wa nchi hii, hivyo suala hilo halinipi wasiwasi wala hofu na hivyo vyeti wanavyovitaka mbona vipo tu, ila waelewe kuwa sisi ni Wamanyema halisi na ni raia halali wa nchi hii,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa ACT - Wazalendo, Mkoa wa Kigoma, Sendwe Mbaruku, alitoa taarifa Alhamisi kuhusu suala la Nondo kuhojiwa na uhamiaji na kusema; “Kijana Abdul ni mtoto wetu hapa Kigoma, wazazi wake ni wakazi na wapiga kura wa hapa Ujiji, zaidi ni Watanzania wenzetu.”

Maelezo haya yametolewa na mzazi huyo Siku chache baada ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo kuhojiwa na Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam kuhusu uraia wake.

Mzazi huyo amesema babu yake Nondo, alishawahi kuwa Polisi kwa miaka 18 kuanzia mwaka 1940 hadi 1958 na alishafanya kazi huko Mabatini mkoani Mwanza na sehemu nyingine za nchi.

Alisema babu yake wakati akiwa polisi, ndipo zilipoanzishwa Kota za Msimbazi, Dar es Salaam na jina lake lilikuwa maarufu, akijulikana kama Mzee Kagobe.

Kama haitoshi alisema bibi yake Nondo alikwenda kuhiji, mnamo 1970 na alipewa hati ya kusafiria ya Tanzania, huku akihoji, “Kama angekuwa sio raia wa Tanzania angepewaje hati hiyo?”

Baada ya Nondo kuripoti polisi mjini Mafinga alishikiliwa na jeshi hilo Mkoa wa Iringa na baadaye kukabidhiwa kwa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa alisema kupitia uchunguzi wa kisayansi, wamebaini kuwa hakuwa ametekwa, bali alijiteka na tayari suala lake lipo mahakamani, Iringa.
Read More

Mbunge Mchafu aitaka Serikali kupitia Sheria upya

Wakati Wabunge walikuwa wakichangia mapendekezo yao katika  bajeti ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2018/19   Mbunge wa viti maalum CCM Hawa Mchafu Chakoma  ameishauri serikali kuanzisha namna bora ya  mpango wa pensheni kwa wazee waliolitumikia taifa.

Hawa Mchafu alisema ;"Nashindwa kufahamu mfuko wa moja kwa moja ambao upo kwa ajili ya wazee, muda umefika sasa ule mchakato wa pensheni kwa wazee uje sasa ili kuweza kuwasaidia wazee wa taifa letu ambao kwa nafasi zao walisaidia sana nchi yetu”

“Niipongeze Serikali pia kwa kuanzisha miradi mbalimbali mikubwa ikiwemo ujenzi wa bomba la mafuta, ujenzi wa viwanja vya ndege n.k  ....ni wazi itaambatana na upatikanaji wa ajira lakini niishauri Serikali ihakikishe inafuatilia mikataba ya kazi kwa watanzania inayofanyika katika miradi hiyo kwamaana kumekuwa na ukakasi mkubwa sana mikataba mingi inaukiukwaji wa kisheria” –Hawa Mchafu
Read More

Serikali Yapata Mkopo Wa Shilingi Bilioni 34 Kutoka Mfuko Wa Maendeleo Ya Kiuchumi Wa Kuwait

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), na Serikali ya Tanzania zimetiliana saini  rasimu ya mkataba wa  kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 15.3, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 34, kwa ajili ya mradi wa  kilimo cha umwagiliaji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma,  lenye ukubwa wa  hekta 3,000.

Rasimu hiyo ya Mkataba imesainiwa na Kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na Mshauri wa Masuala ya Kilimo wa Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait,  Dkt. Abdulrida Bahman na  kwa upande wa Tanzania ikisainiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, mjini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)  amesema hatua hiyo imfikiwa baada ya timu ya wataalamu kutoka Kuwait kutembelea eneo la mradi mkoani Kigoma na kuridhishwa na umuhimu wake kiuchumi kwa wananchi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.

 “Mradi huo una umuhimu mkubwa kwa watanzania kwa kuwa wataweza kuwa na kilimo cha umwagiliaji cha Mpunga na Mbogamboga kwa mwaka mzima badala ya kilimo cha msimu cha kutegemea mvua, na katika siku zijazo Kigoma itakua miongoni mwa mikoa inayozalisha mchele kwa wingi”, alisema Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango amesema kuwa Serikali ya Tanzania na Kuwait zitatia saini mkataba rasmi wa mkopo huo wenye masharti nafuu ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu ili mradi huo uanze kutekelezwa ili kuongeza kipato cha wananchi na  kuwa na uhakika wa chakula.

Amesema Nchi ya Kuwait imekuwa ikiisaidia Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya ukarabati wa Hospitali ya Mnazi mmoja, Zanzibar kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 13.6 sawa na shilingi bilioni 31.

"Kwa upande wa Tanzania Bara wametoa mkopo nafuu wa shiingi bilioni 115 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Chaya hadi Nyahua (km 85) kwa kiwango cha lami ambayo ni muhimu kwa kuwa inaunganisha mikoa ya Magharibi mwa Tanzania" aliongeza Dkt. Mpango

Miradi mingine ambayo  nchi hiyo imeonesha nia ya kuisaidia nchi, ni pamoja na ujenzi wa jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza, uboreshaji wa barabara ya kutoka Morogoro hadi Dodoma na ujenzi wa barabara za mzunguko za kuingia na kutoka mjini Dodoma ambazo zitasaidia kuondoa msongamano wa magari yanayopita katikati ya mji huo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na vyombo vya moto baada ya Makao Makuu ya Serikali kuhamia Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mpango ameishukuru nchi ya Kuwait kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait, kwa nia yake njema na thabiti katika kusaidia nchi ya Tanzania kutekeleza kwa mafanikio miradi ya Maendeleo ya kiuchumi katika nia yake ya kupata maendeleo Stahiki.

Kwa upande wake Kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na Mshauri wa Masuala ya Kilimo wa Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait, Dkt. Abdulrida Bahman, ameishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Fedha na Mipango kwa ukarimu pamoja na Idara ya Taifa ya Umwagiliaji kwa ushirikiano mzuri katika hatua za kufanikisha utekelezaji wa mradi wa umwagiliaji  wa Bonde la Luiche, Mkoani Kigoma.

“Tumetembelea eneo la mradi kwa takribani wiki mbili tumejionea uzuri wa nchi hii na fursa zilizopo, hii ni nchi tajiri na inaweza kuwa tajiri kuliko Kuwait kwa kuwa kila kitu kinachoweza kufanya nchi hii iwe tajiri kipo”.Alieleza Dkt. Bahman.

Amesema mradi huo wa umwagiliaji hautakuwa wa mwisho kupewa fedha na mfuko huo bali utaendelea kusaidia kutekeleza miradi mingine mingi kama ilivyokuwa ikifanya, kutokana na ushirikiano mzuri, wa kihistoria, na wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili.

Mwisho.
Read More

Rais Magufuli atangaza ajira mpya 1500 Polisi....Pia Kawapa Bilioni 10

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  tarehe 07 Aprili, 2018 ameungana na Watanzania wote kuadhimisha siku ya mmoja wa waasisi wa Taifa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi kwa kuzindua kituo cha polisi, kufungua nyumba 31 za askari polisi na kushuhudia maonesho ya Polisi katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Jijini la Arusha.

Kituo cha polisi cha watalii na wanadiplomasia kilichopo Naura, kituo cha polisi cha Muriet, na nyumba za 18 kati ya 31 za makazi ya polisi vimejengwa kwa mchango wa wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha  na Benki ya CRDB kwa gharama ya Shilingi Milioni 753, wakati nyumba za polisi 13 zimejengwa na Serikali kwa gharama ya Shilingi Milioni 250.

Mhe. Rais Magufuli aliagiza kujengwa kwa nyumba hizo baada ya kutokea ajali ya moto iliyosababisha nyumba 13 za makazi ya askari polisi na mali zao kuungua moto tarehe 27 Septemba, 2017.

Katika kutekeleza agiza hilo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo akaamua kuwashirikisha wafanyabiashara na benki ya CRDB kuchangia ujenzi huo na kufanikiwa kujenga nyumba nyingine 18 na vituo hivyo viwili vya polisi.

Pamoja na kuzindua miradi hiyo Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia maonesho ya Jeshi la Polisi ya kuzuia na kupambana na uhalifu yakiwemo kukabiliana na waandamanaji haramu, wezi, waporaji watumiao silaha na magaidi, yaliyofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid.

Akizungumza baada ya maonesho hayo Mhe. Rais Magufuli amesema Taifa litaendelea kumkumbuka Hayati Sheikh Abeid Amani Karume kwa juhudi zake za kujenga nchi ikiwemo kuwajengea makazi wananchi masikini kule Zanzibar na ametoa wito kwa Watanzania kumuenzi kwa kudumisha amani na kuchapa kazi.

Pamoja na kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo kwa jitihada zake za kuwaunganisha wadau na kisha kufanikiwa kujenga nyumba za askari na vituo vya polisi Mhe. Rais Magufuli ametoa Shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari polisi wa vyeo vya chini nchini, na amewaagiza viongozi wa mikoa yote kuwashirikisha wadau katika ujenzi huo kama ilivyofanyika mkoani Arusha ili kukabiliana na tatizo la askari kukosa nyumba za makazi.

“Askari polisi mnafanya kazi kubwa sana ya kulinda raia na mali zao, natambua juhudi kubwa mnazofanya na napenda kuwashukuru sana, naomba Watanzania wote tuendelee kuliunga mkono Jeshi la Polisi.

“Wakati naingia madarakani kulikuwa na mauaji kila wakati, kule Kibiti pekee yake waliuawa watu 59 wakiwemo askari polisi 17 na raia 42, Jeshi la Polisi limefanya kazi kubwa na sasa mauaji yale yamedhibitiwa, ni lazima tulipongeze jeshi letu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amekubali maombi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro la kuongezewa idadi ya askari na kupandishwa vyeo kwa maafisa wa polisi ambapo ameruhusu Jeshi la Polisi kuajiri askari wapya 1,500 kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na kumpelekea mapendekezo ya maafisa wanaostahili kupandishwa vyeo.

Mhe. Rais Magufuli amempongeza IGP Sirro kwa hatua ya kuwafukuza kazi askari polisi 458 waliokutwa na makosa ya kinidhamu na uadilifu kuanzia mwaka 2015 hadi sasa, na ametaka hatua hizo ziendelee kuchukuliwa dhidi ya askari wengine wanaokiuka maadili na taratibu za kazi ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi yakiwemo upokeaji rushwa na unyanyasaji raia kwa kuwabambikiza kesi.

Halikadhalika Mhe. Rais Magufuli amepiga marufuku askari, maafisa wa polisi na viongozi wengine wa Serikali kushiriki ufyekaji wa mashamba ya bangi na badala yake ametaka mashamba hayo yanapobainika yafyekwe na wanavijiji wenyewe waliohusika kuyalima.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Mke wa Rais Mhe. Mama Janeth Magufuli na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Naibu Mawaziri, viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, wabunge na wananchi.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Arusha
07 Aprili, 2018
Read More

Kauli ya Humphrey Polepole Baada ya Askofu Kakobe Kuitwa na Idara ya Uhamiaji

Baada ya watu mbalimbali kutoa maoni yao juu ya kuitwa kwa Askofu Kakobe na idara ya Uhamiaji kuhojiwa Uraia wake, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Humphrey Polepole ameandika yafuatayo kwenye ukurasa wake wa Twitter; “Mbona kuhojiwa jambo la kawaida? baadhi ya watu wanajenga tabia ya hovyo sana”

“Watu “wakubwa” wakiitwa kuhojiwa inaonekana kitu cha ajabu. Mbona huku mtaani kuhojiwa Polisi ni kitu cha kawaida tu, tuanze kuzoea na hasa ktk awamu ya 5 kwamba, na tunasisitiza binadamu wote ni sawa” 
Read More

RC Gambo Amtoa Hofu Rais Magufuli Kuhusu Maandamano ya Mange Kimambi

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho gambo amemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutotishwa na maandamano ya mitandaoni yanayoratibiwa na Mange Kimambi, kwani mkoa wa Arusha uko salama.

Mrisho Gambo ameyasema hayo leo alipokuwa akitoa salam zake kwa Rais Magufuli, kwenye sherehe za uzinduzi wa nyumba za polisi mkoani Arusha, kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abedi.

Kwenye salamu hizo Mrisho Gambo amesema mkoa wa Arusha ni salama na wakazi wa Arusha hawana haja ya maandamano, kwani wanachohitaji ni uongozi wake ambao unawaletea maendeleo makubwa.

Mrisho gambo aliendelea kwa kueleza kuwa anatambua kazi ya kubwa aliyonayo Rais ya kupigana vita ya uchumi, na watu wengi wasiopenda nchi hii watachukia kutokana na hilo.

“Mheshimiwa Rais nikuhakikishie tu Arusha ni salama, wala usitishwe na mbwembwe za kwenye mitandao, watanzania halisi ni hawa hapa wenye Arusha yao. 
"Watanzania wa Arusha wamechoka na maandamano, wanataka uongozi wa kwako ambao unawaletea maendeleo. Ninajua vita uliyokuwa nayo ni kubwa sana, Mwl. Nyerere alikuwa na vita ya ukombozi, akaimaliza salama, 
"Mheshimiwa Rais vita yako wewe ni ya kiuchumi, ni vita inayopigana na mabeberu ambao wanawatumia wengine kukwamisha jitihada zako. Watu wengi ambao hawaitakii mema nchi hii hawawezi kuipenda”, amesema Mrisho Gambo.

Sambamba na hilo Mkuu wa mkoa huyo wa Arusha amemshukuru Rais Magufuli na wadau kwa kufanikisha ujenzi wa nyumba hizo za askari polisi, ambazo awali ziliteketea kwa moto.
Read More

Rais Magufuli Awapiga Marufuku Polisi Kufyeka Mashamba ya Bangi

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka maofisa wa Jeshi la Polisi na Makamishna wake kutoyafyeka na kuyachoma moto mashamba ya bhangi na badala yake watumie njia za kiintelijensia kuwababini watuhumiwa, kuwakamata na kuwashughulikia ikiwa ni pamoja na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Rais ameyasema hayo leo wakati akiwahutubia wananchi wa Arusha katika Uwanja wa Amri Abeid baada ya kuzindua kituo cha polisi na nyumba za polisi mkoani humo.

“Hakuna kitu kinachonikera kama Askari Polisi kwenda kufyeka mashamba ya bhangi, makamanda wako na askari wako, wasikate mashamba ya bangi, hawakuajiriwa kufyeka bhangi. Niwashauri tu kwamba, tumieni njia za kintelijensia, mtawashika tu, kama shamba lipo karibu na kijiji, kamata kijiji kizima, wazee, vijana, wanawake hata na watoto, ndio wakafyeke hilo shamba la bhangi.

“Nasema askari wasiende kufyeka bhangi, hawakuajiriwa kufyeka bhangi, usiwatume askari wako kufyeka bhangi, wataumwa nyoka bure, wamevaa uniform nzuri, msidhalilishe jeshi kwa kufyeka bhangi, mimi nisingefyeka bhangi na wa kufyeka wapo.

“Nilimuona Waziri naye yumo anafyeka na kuchoma moto shamba la bhangi, juzi nikaona tena RPC wa Dodoma naye anafyeka shamba la bhangi na askari wake, mpaka akachoka anasema hili shamba lililobaki tutalimalizia kesho. Inashangaza sana, tusijidhalilishe hivyo,” alisema Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya Usalama kuendelea kuimarisha hali ya amani nchini na kuwatumikia Watanzania kwa maendeleo ya Taifa.
Read More

Rais Magufuli awapa rungu polisi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka jeshi la polisi kufanya lolote lililopo ndani ya uwezo wao, ili kuhakikisha mani ya nchi haivunjwi na kubaki na utulivu.

Kauli hiiyo imetolewa leo jijini Arusha alipokuwa akihutubia kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, na kusema kwamba anatambua kazi ya jeshi la polisi ingawa kuna watu ambao wana wabeza, hivyo wasiyumbishwe na watu hao, ila waendelee kuchapa kazi kwani yeye kama Amiri Jeshi Mkuu wao yuko pamoja nao.

“Kuna watanzania wanaongea maneno ya kebehi kebehi kuhusu polisi, hawajui thamani ya polisi, ndugu zangu polisi tembeeni kifua mbele, na kwa bahati nzuri mimi ni shemeji yenu, mkwe wenu, msiwe na wasi wasi, maneno ya kashfa na kebehi yanayozungumzwa na wengine wala yasiwakatishe tamaa. 
"Nilipopewa urais nikaapa kuhakikisha nchi inakuwa salama, na kuhakikisha nchi inakuwa salama, lazima jeshi la polisi liwe salama, endeleeni kuilinda amani ya nchi yetu, mtakayoyaamua yaamueni na mimi nitawasapoti, niliapa kuilinda amani ya nchi hii kwa nguvu zote na nitailinda”, amesema Rais Magufuli.

Sambamba na hilo Rais Magufuli amesema anatambua mazingira magumu waliyonayo askari polisi hususan wa vyeo vya chini, hivyo atahakikisha anatatua kero zao ikiwemo kuboresha makazi yao.
Read More

Madiwani Dar Walia na Itikadi za Kisiasa Kuwakwamisha Katika Maendeleo

Madiwani Dar Walia na Itikadi za Kisiasa Kuwakwamisha Katika Maendeleo
Vitendo vya kuingiza itikadi za kisiasa vinavyofanywa na baadhi ya madiwani wa vyama mbalimbali jijini Dar es Salaam, vinadaiwa kukwamisha juhudi za maendeleo na huduma za kijamii kwa wananchi.

Wakijadiliana katika semina iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), baadhi ya madiwani wa mkoa huo walisema itikadi hizo zimegeuka kuwa mwiba wa maendeleo.

Diwani wa viti maalumu kutoka Ubungo, Rehema Mayunga alisema linapokuja suala la kuwaletea maendeleo wananchi kila mmoja anapaswa kushirikiana na mwenzake.

Diwani wa Kivule, Wilson Molel alisema suala la kuingiza siasa katika kila jambo la maendeleo linachelewesha na kukwamisha miradi mingi, lakini waathirika ni wananchi.

Ofisa programu na uchechemuzi wa TGNP, Deogratius Temba aliwaomba madiwani kuhakikisha mikutano ya kisheria inafanyika kwa wakati na kuweka kwenye mbao za matangazo maazimio ya Serikali za vijiji na mitaa, mapato na matumizi ya fedha za umma.
Read More

Rais Magufuli: Mke wangu ni mtoto wa polisi, Maisha Yao Nayajua

Rais John Magufuli leo ametoboa siri kuwa mke wake, Janeth alikuwa ni mtoto wa polisi.

Ameyasema hayo leo Aprili 7 wakati wa uzinduzi wa nyumba 31 za polisi  mjini Arusha na kusema baba mkwe wake alikuwa sajenti wa polisi.

“Nyumba za polisi ndizo zimenipa mke kwa hiyo nyumba za polisi ninazifahamu, huyu mke wangu niliye naye alikuwa mtoto wa polisi, marehemu baba yake hakuwa na cheo kikubwa alifariki akiwa sajenti,” amesema.

Ameongeza kuwa, “Ingekuwa nazindua Moshi, angenionyesha nyumba walizokaa lakini za Oysterbay alizoishi alishanionyesha na za Ukonga na za sehemu nyingine. Kwa hiyo maisha ya polisi ninayafahamu.”
Read More

Rais Magufuli atoa agizo kwa IGP Sirro

Rais Dkt. John Magufuli amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro kuhakikisha inapofika kesho (Aprili 8, 2018) awe ameshawaingiza askari Polisi walionguliwa nyumba zao hapo awali katika nyumba mpya ambazo zimezinduliwa hii leo.

Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo leo (Aprili 7, 2018) wakati alipokuwa anazungumza muda mchache alipomaliza kuzindua nyumba za askari zilizojengwa mkoani Arusha na kusema anawapa pole kwa majanga yaliyotokea ya kuunguliwa moto, huku akiwapongeza wadau mbali mbali waliojitolea kwa mioyo yao katika ujenzi wa nyumba hizo.

"Nimepata mawazo ni kitu gani tunaweza kufanya kuhusina na matatizo ya nyumba za Polisi, sasa ninachoomba Mhe. IGP wale walionguliwa nyumba, kesho waingie katika nyumba zao hizi mpya ambazo zimemalizwa kujengwa. Kwasababu najua muda mwingine wanaweza wakachomekwa Polisi wengine halafu waliokuwemo wakaambiwa hapana", amesema Dkt. Magufuli.

Pamoja na hayo, Rais Magufulia ameendelea kwa kusema "sasa nataka wale wale walionguliwa ndio waingie humo kwenye nyumba kwasababu Mungu aliwasaidia, moto ukaungua ungua kwa faida ya wao lakini hii inadhihirisha ni kwa namnagani makazi ya nyumba za polisi yalivyo kuwa mabovu"..
Read More

Serikali yawapa siku 23 wamiliki wa nyumba

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema serikali itawafikisha Mahakamani na kuwafutia hati ya umiliki wananchi wote wanaomiliki ardhi ambao wamekuwa hawalipi kodi ya ardhi.

Lukuvi ametoa kauli hiyo mara baada ya kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwa watendaji wake ambapo amesema serikali inapoteza mapato mengi kwa kuwa baadhi ya wananchi kukosa uaminifu wa kulipa kodi ya ardhi kwa wakati.

Kutokana na hali hiyo, Waziri Lukuvi amesema ameamua kutoa muda hadi Aprili 30, 2018 ili kila mtu anayemiliki ardhi awe amekwisha lipa kodi hiyo na kwa wale ambao hawatalipa kodi kwa wakati ni wazi serikali itawafikisha mahakamani, kuwafutia hati za viwanja hivyo na kuviuza upya kwa wamiliki wengine ama kuuza nyumba zao.

Aidha Mhe. Lukuvi amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika zoezi hilo ili kupunguza ukubwa wa kazi na kukusanya fedha kwa wakati na kuongeza pato la taifa.
Read More

LIVE: Fuatilia Hapa Hotuba ya Raiis Magufuli Akizindua Nyumba za Polisi Arusha

LIVE:  Fuatilia Hapa  Hotuba ya Raiis Magufuli Akizindua Nyumba za Polisi Arusha
Read More

Aesh Atishia Kuzichapa Bungeni

Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aesh Hillary (CCM), ameeleza kushangazwa na kitendo cha Serikali kutenga Sh bilioni 15 kati ya Sh bilioni 80 zilizoombwa na Hifadhi ya Chakula ya Taifa (NFRA) na kwamba iwapo serikali itafunga mipaka ya nchi ili chakula kisiuzwe nje, watashikana mashati bungeni.

Akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma jana Ijumaa aprili 6, Aesh alisema fedha hizo zilizotengwa zinatosha kunua mahindi Wilaya ya Sumbawanga pekee.

“Kama mkishindwa kununua haya mahindi msifunge mipaka, mwaka jana mmefunga mkaja kufungua wakati muda umekwenda na kuweka masharti magumu, nawaambia safari hii mkishindwa kununua mkafunga mipaka tutashikana mashati humu ndani.

“Siyo kazi ya mkulima kuhakikisha nchi haina njaa ni kazi ya Serikali, nashangaa huku mnasema tu tumbaku na pamba, bila mahindi huyo mkulima hawezi kulima hayo mazao yake,” alisema Aesh.

Aeshi pia amezungumzia watumishi wenye elimu ya darasa la saba kufukuzwa kazi akisema mmoja wa Madereva waliofukuzwa kazi alimwendesha mpaka Waziri Mkuu Mstaafu (hakutaja jina la waziri huyo).

“Huyu dereva alikuwa amebakisha miaka mitano tu astaafu, sasa hivi mmemfukuza kazi hana cha kufanya, suala hili mliangalie upya,” alisema.
Read More

Kitwanga Ahofia Wabunge Kutumia Vitambulisho vyao Kujinyonga



Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga (CCM), amedai vitambulisho vya wabunge vina kamba ambazo baadhi ya wabunge wanaweza kuzitumia kujinyonga hivyo viondolewe.
Read More

Kitwanga Ahofia Wabunge Kutumia Vitambulisho vyao Kujinyonga

Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga (CCM), amedai vitambulisho vya wabunge vina kamba ambazo baadhi ya wabunge wanaweza kuzitumia kujinyonga hivyo viondolewe.

Akiomba mwongozo bungeni leo Ijumaa Aprili 6, Kitwanga amesema kutokana na hali hiyo ni kwanini Bunge lisione umuhimu wa kutumia vitambulisho vya kisasa badala ya hivyo.

“Maana hivi vina kamba ambazo nina wasiwasi watani wangu kama Lukuvi (Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi) na wahehe wanaweza kujinyonga,” amesema Kitwanga.

Akijibu mwongozo huo, Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge amesema ni lazima waende na wakati kwa kutumia vitambulisho vya kisasa ambavo ni hivyo.
Read More
Powered by Blogger.

Hot

© Copyright KAHAMA 24