Madiwani Dar Walia na Itikadi za Kisiasa Kuwakwamisha Katika Maendeleo

MATANGAZO

MATANGAZO
Madiwani Dar Walia na Itikadi za Kisiasa Kuwakwamisha Katika Maendeleo
Vitendo vya kuingiza itikadi za kisiasa vinavyofanywa na baadhi ya madiwani wa vyama mbalimbali jijini Dar es Salaam, vinadaiwa kukwamisha juhudi za maendeleo na huduma za kijamii kwa wananchi.

Wakijadiliana katika semina iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), baadhi ya madiwani wa mkoa huo walisema itikadi hizo zimegeuka kuwa mwiba wa maendeleo.

Diwani wa viti maalumu kutoka Ubungo, Rehema Mayunga alisema linapokuja suala la kuwaletea maendeleo wananchi kila mmoja anapaswa kushirikiana na mwenzake.

Diwani wa Kivule, Wilson Molel alisema suala la kuingiza siasa katika kila jambo la maendeleo linachelewesha na kukwamisha miradi mingi, lakini waathirika ni wananchi.

Ofisa programu na uchechemuzi wa TGNP, Deogratius Temba aliwaomba madiwani kuhakikisha mikutano ya kisheria inafanyika kwa wakati na kuweka kwenye mbao za matangazo maazimio ya Serikali za vijiji na mitaa, mapato na matumizi ya fedha za umma.