Hivi Ndivyo Vurugu za Mkutano wa CUF Ulivyokuwa Jana...Viti Vyavunjwa vunjwa, Mkutano Wahairishwa

MATANGAZO

MATANGAZO
Mkutano Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) uliofanyika kwa dharura leo katika hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam umevunjika baada ya vurugu kutokea katika mkutano huo na wajumbe waliokuwamo kushindwa kuendelea na zoezi la upigaji kura kumchagua mwenyekiti wa chama hicho.

Mkutano huo ambapo walikuwa wanatarajia kumchagua mwenyekiti wa chama hicho baada ya Prof. Lipumba kujiuzulu mwaka jana, umeshindwa kuendelea baada ya wafuasi wa chama hicho kuvamia ukumbini na kuleta vurugu wakishnikisha Prof. Lipumba awe mwenyekiti wa chama hicho.

Kufuatia vurugu hizo, aliyekuwa akiongoza mkutano huo, Julius Mtatiro ameahirisha mkutano huo hadi hapo utakapotajwa tena.

Awali, wajumbe 476 walipiga kura wakizuia Prof. Lipumba asigombee tena nafasi ya uenyekiti wa chama hicho. Kura zilizokuwa zinahitajika ili kumzuia ni 410.