Nimeshakuwa sasa, kiukweli nina kiu ya mume – Johari
Msanii wa filamu, Johari Chagula amefunguka kwa kusema kuwa kwa sasa ana kiu yakumpata mume sahihi ambaye ataingia naye kwenye maisha ya ndoa.
Mwigizaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja, amesema umri wake kwa sasa unamruhusu kuingia kwenye maisha ya ndoa
“Mimi ni mwanamke kamili, ni mtu mzima. Nimeshakuwa sasa, kwahiyo kiukweli nina kiu ya mume,” Johari aliliambia gazeti la Mtanzania.
“Mungu akinipa mume bora, nitaolewa. Sitaki kuzungumzia sana mambo yaliyopita, lakini muhimu kwa sasa ni mume,”
Mbali na hayo mwingizaji huyo amewataka kukaa mkao wa kula kwa ajili ya filamu yake mpya ambayo amewashirikisha wasanii wachanga kutoka mkoani Mwanza.
(h)
ReplyDelete