USAIN BOLT AZIDI KUTAKATA RIO, AZIKARIBIA REKODI ZA LEWIS NA PAAVO
Mjamaica huyo alitumia sekundi 19.78 na kumaliza mbele ya Mcanada Andre de Grasse na Mfaransa Christophe Lemaitre.
Muingereza Adam Gemili alimaliza sambamba na Lemaitre
Bolt, 29, tayari hapo awali kwenye Michuano hii ya jijini Rio ameshashinda mbio za mita 100, na leo Ijumaa itakuwa ni fainali ambapo atakimbia mbio za mita 4×100 (400).
Bolt anatarajiwa kurudia rekodi ya mafanikio yake ya kushinda mbio za mita 100, 200 na 4×100 aliyoiweka mwaka 2008 jijini Beijing na 2012 jijini London.
Mjamaica huyo, ambaye mwezi February mwaka huu alisema angependa kustaafu mwaka 2017 baada ya Michuano ya Dunia (World Championships), ameshinda fainali zote za nane Olimpiki ambazo amewahi kushiriki.
“Kikubwa ambacho nimekifuata hapo ni kuendeleza furaha yangu niliyonayo kwa miaka yote niliyoshiriki,” amesema.
“Sikuwa na furaha wakati nilikuwa nimevuka mstari, lakini furaha yangu ilikuja baada ya kupata medali ya dhahabu- hicho ndicho kitu cha msingi sana.”
Mpaka sasa ni Mmarekani Carl Lewis aliyekuwa akikimbia mbio fupi na Paavo Nurmi mbio ndefu ndio wanashikilia rekodi za kuwa na medali nyingi zaidi za dhahabu za olimpiki kwenye riadha.
Lewis alishinda medali za dhahabu tisa kati ya mwaka 1984 na 1996, wakati Nurmi pia alishinda tisa kati ya mwaka 1920 na 1928.
“Kitu gani kingine nifanye ili kuuthibitishia ulimwengu mimi ni bora? Najaribu kuwa moja kati ya wabora, kuwa miongoni mwa Ali na Pele,” Bolt aliongeza.
No comments:
Post a Comment