Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele

MATANGAZO

MATANGAZO



tende
Changamoto ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele imekuwa tishio kwa jamii huku mkoa wa Morogoro ukiongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi wa usubi na kifafa katika wilaya za Ulanga na Kilosa.
Akizungumza na Channel Ten wakati wa utoaji elimu kwa wakuu wa wilaya, wenyeviti wa halmashauri, wakurugenzi,wataalamu wa afya na watendaji mbalimbali wa Serikali, Mratibu wa taifa wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele Dk.Upendo John amebainisha Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye magonjwa hayo na Serikali imekuwa na mikakati ya kutosha kukabiliana nayo kupitia elimu na dawa zinazotolewa bure kwa ajili ya kinga na tiba.
Hata hivyo, Mratibu huyo wa taifa amesema pamoja na jitihada hizo za Serikali, takwimu zinaonyesha ni idadi ndogo tu ya wananchi waliojitokea kumeza dawa hizo kutokana na sababu mbalimbali.
Kwa upande wake, Mratibu wa magonjwa hayo wilayani Kilosa,Dk Rosmer Ngurue licha ya wilaya yake kuongoza kwa ugonjwa wa usubi, lakini wameweza kupunguza kiwango cha ugonjwa huo kwa asilimia kubwa ikilinganishwa na ilivyokuwa awali ambayo ilikuwa asilimia 42 na hivi sasa imeshuka mpaka asilimia 10.