Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts

Picha: Rais Magufuli Akiwa katika Ibada ya Kumsimika Askofu Jimbo la Katoliki la Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameshiriki katika Ibada ya kumsimika Mhashamu Isaack Amani kuwa Askofu Mkuu Jimbo la Katoliki la Arusha katika Kanisa la Mtakatifu Theresia la Mtoto Yesu Jimbo Kuu Katoliki jijini Arusha leo April 8, 2018.
Read More

BREAKING: Mhariri wa Gazeti la The Guardian aokotwa Bunju akiwa hajitambui

 Mmoja wa wahariri waandamizi wa gazeti la The Guardian, Finnigan Simbeye ameokotwa eneo la Bunju wilayani Kinondoni akiwa hajitambui.

Taarifa zilizosambaa leo Jumapili Aprili 8, 2018  zinazoonyesha kitambulisho chake cha kazi cha kampuni ya The Guardian Limited zinaeleza Simbeye aliokotwa akiwa kwenye hali mbaya.

Hata hivyo, kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni, Murilo Jumanne amesema hana taarifa za tukio la kuokotwa Simbeye.

Rose Mirondo, ambaye ni mkewe Simbeye amesema mumewe aliondoka nyumbani jana Jumamosi Aprili 7, 2018 akiwa na gari lakini hakurudi hadi alipopata taarifa za kuokotwa kwake leo.

Amesema alipokwenda eneo la tukio Bunju hakuliona gari la mumewe.

Rose amesema watu aliowakuta eneo la tukio wamemweleza kwamba Simbeye alichukuliwa na polisi kupelekwa hospitali.

Amesema bado hana taarifa ya hospitali gani amepelekwa na kwamba, anakwenda Kituo cha Polisi Bunju kupata taarifa zaidi.
Read More

Serikali Kuanzisha Kampeni Ya Jiongeze Tuwavushe Salama ili kupunguza vifo vya Mama na Mtoto

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete amesema matatizo ambayo yanatokana na uzazi yapo ambayo yanaweza kuzuilika na kuhimiza wadau kushirikiana na Serikali kwa lengo la kuendelea kupunguza vifo vya mama mjazito na mtoto.

Pia ametoa pongezi kwa hatua zinazochukuliwa na Taasisi ya Childbirth Survival International(CSI) ya kuhakikisha wanatoa elimu ya afya salama ya uzazi na kushiriki kwa vitendo katika kufanikisha vifo kwa mama na mtoto vinapungua hapa nchini.

Amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akitoa hotuba yake kwenye Maadhimisho ya miaka mitano ya CSI na kutumia nafasi hiyo kuwapongeza waanzilishi wa taasisi hiyo Stella Mpanda na Profesa Tausi Kagasheki.

Rais mstaafu Kikwete amesema kumekuwepo na vifo ambavyo vinatokea kwa wajawazito na watoto ambao hawana hatia na kutumia nafasi hiyo kuhimiza wadau mbalimbali kushirikiana na Serikali katika kupunguza vifo hivyo.

Amesema ipo haja ya kuendelea kutolewa elimu ambayo itasaidia jamii kutambua umuhimu wa kuhudhuria kliniki kwa mama mjazito na kubwa zaidi kuendelea kutatua changamoto zilizopo kwenye eneo la afya ya uzazi na vifo. Ameelezea hatua ambazo zinachukuliwa katika kupunguza vifo vya wajawazito na watoto.

“Nimefurahi sana kuona taasisi hii imenzishwa na akina mama wa Tanzania. Stella Mpanda yeye ni mkunga na Tausi yeye ni mwanataaluma .Nifaraja sana wamama wa Tanzania kufanya jambo kubwa kama hili la kuhakikisha wanashiriki katika kupunguza vifo vya wajawazito,

“Wametoa heshima kubwa kwa nchi yetu na pia wamefanya jambo kubwa kwa wanawake nchini kwa kuanzisha taasisi kubwa kama hii ya CSI. Kwa bahati mbaya akina mama wakati mwingine mnashindwa kupongezana. Adui wa mwanamke ni mwanamke ni mwenyewe,” amesema Rais mstaafu Kikwete.

Kuhusu changamoto zilizopo kwenye afya ya uzazi na kwamba moja ya malengo ya milenia inazungumzia kupunguza vifo vya mama mjazito na watoto chini ya miaka mitano.

“Wakati naingia madarakani mwaka 2005 , vifo kwa watoto wanaokufa ilikuwa 578 kati ya vizazi hai 100,000 wanaozaliwa. Baadae tukapunguza vifo hadi watoto 432 lakini ikapanda tena hadi vifo vya watoto 556 wakati lengo la milenia ilikuwa ni watoto 191,

“Hivyo tukaamua kuweka mikaka katika kuhakikisha tunapunguza vifo hivyo,” amesema.

Hata hivyo takwimu za mwaka 2016 kwa mujibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ni kwamba kati ya vizazi hai 100,000 wanaopoteza maisha ni 556.

Serikali kuja na Kampeni ya JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA
Kwa upande wa Waziri  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema wanatarajia kuanzisha kampeni   itakayofahamika Jiongeze tuwavushe salama.

Amesema lengo la kampeni hiyo ni kuhakikisha mama mjazimto anajiongeza kwa kuhakikisha anakwenda kituo cha afya na akifika anayetoa huduma naye ajiongeze kwa kutoa huduma sahihi ambayo mtamuwezesha mjazmito kujifungua salama.

Waziri Mwalimu ametumia nafasi hiyo kuelezea hatua ambazo Serikali ya awamu ya tano inavyochukua jukumu la kuhakikisha vifo vya mama mjazito na mtoto vinapungua ambako akagusia kampeni hiyo.

“Tumeongeza bajeti ya wizara ya afya na sehemu kubwa pamoja na kuangalia dawa na vifaa tiba pamoja na miundombinu pia tumeweka nguvu katika afya ya mama na mtoto,” amesema.

Wakati huo huo Mwalinzishi na Mkurugenzi wa CSI Stella Mpanda ameelezea namna ambavyo taasisi yao imejikita katika kuhakikisha vifo vya mama mjazito na mtoto vinaungua na kufafanua kuwa wamekuwa wakitoa elimu ya uzazi.
Read More

Polisi 458 Wafukuzwa Kazi

Jumla ya maofisa wa Jeshi la Polisi wapatao 458 wamefukuzwa kazi kutokana na utovu wa nidhamu kuanzia mwaka 2015 hadi Machi mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa jana Aprili 7 na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro alipokuwa akizungumza mbele ya Rais John Magufuli wakati wa uzinduzi wa nyumba 31 za Polisi na ufunguzi wa kituo cha Polisi cha Utalii na Kidiplomasia jijini Arusha.

Sirro alisema kazi ya Jeshi la Polisi ni kurekebisha mienendo ya wananchi, hivyo kabla hawajawaelimisha wananchi wanapaswa kuwa na mienendo mizuri wao kwanza.

Alifafanua kwa kulitambua hilo ndiyo maana askari waliokwenda kinyume na azma hiyo walichukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi, ambapo kwa mwaka 2015, 198 walifukuzwa kazi.

Alisema kwa mwaka 2016 walifukuzwa askari 165, 2017 (81) na kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu wamefukuzwa askari 14.

“Hatuna muhali kuwachukulia hatua askari wanaokiuka utaratibu na nidhamu ya utendaji katika Jeshi la Polisi,” alisema IGP Sirro.
Read More

Mwanamke wa Kwanza Kupata Degree Tanzania Atunukiwa Tuzo

Dkt Maria Kamm ndiye  mwanamke wa kwanza wa Tanzania kupata Shahada ya kwanza (Degree) na jana ametunukiwa tuzo ya heshima katika tuzo za Malkia wa Nguvu zinazoandaliwa na Clouds Media.

Mama Kamm ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Weruweru iliyopo Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, akiwa kama Mzalendo wa kweli, ametumia maisha yake kwa kiasi kikubwa kuwashauri na kuwaelimisha vijana katika masuala mbalimbali ya Taifa.

Mgeni Rasmi katika utoaji wa Tuzo hizo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwl Nyerere Posta jijini Dar, alikuwa Waziri wa  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Ummy Ally Mwalimu.
Read More

Waziri Ndalichako atoa agizo kwa shule binafsi


Serikali imewataka wamiliki wa shule binafsi nchini kutumia ujuzi na uzoefu wao katika nyanja ya elimu ili kuishauri Serikali nini cha kufanya ili kiwango cha elimu inayotolewa hapa nchini kuendelea kukua.


Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa JOYCE NDALICHAKO amesema hayo Mjini Dodoma alipokuwa akifungua mkutano wa Chama cha Wamiliki wa shule binafsi na kuongeza kuwa ni jukumu la jamii nzima kuhakikisha elimu nchini inakuwa.
Nao baadhi ya wamiliki wa shule binafsi wamesema kuna mambo mengi ambayo Serikali inaweza kujifunza kutoka katika shule hizo na kuzifanya shule za Serikali ziwe zinafanya vizuri katika mit i hani ya kitaifa kama zilivyo za binafsi.
Mkutano wa siku moja umeshirikisha wamiliki wa shule binafsi kutoka nchi nzima, lengo kuu likiwa ni kuangalia mafanikio na matatizo ambayo shule binafsi nchini zinakabiliwa nazo.
Read More

Askofu Mkuu Zachary Kakobe aitwa Uhamiaji Jumatatu kuhojiwa juu ya uraia wake

Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dar-Es-Salaam, imemwandikia barua Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Askofu Zachary Kakobe, kumwita kwa ajili ya mahojiano.

 Askofu Kakobe ametakiwa kufika katika ofisi hiyo, Jumatatu 9.4.2018 saa 4 asubuhi, na kuonana na Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Dar-Es-Salaam, ili kuhojiwa juu ya uraia wake.

Alipoulizwa kwa njia ya simu, Askofu Kakobe amethibitisha kupokea barua hiyo, na kusema kifupi tu kwamba, atakwenda kwenye mahojiano hayo.

Tukio hili linakuja baada ya sekeseke kati ya Askofu huyo na TRA, kuhitimishwa tarehe 20.2.2018, siku ambayo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere, alipotoa taarifa kwa umma juu ya uchunguzi wao; na baadaye kusema mjadala huo umefungwa.
Read More

IGP Sirro atoa maelekezo kwa wanaotaka kuandamana

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro amesema Jeshi lake liko imara kweli kweli katika kupambana na watu wanaotaka kuleta uvunjifu wa amani nchini, huku akiwasii wanaotaka kuandamana kuacha mara moja kwani kitakachowapata wasije kulaumiana

IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo (Aprili 7, 2018) wakati akitoa salamu zake kwa Rais Dkt. Magufuli katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo mjini Arusha baada ya uzinduzi wa nyumba za askari na kushuhudia maonesho ya utayari ya jeshi hilo katika kukabiliana na uhalifu.

"Mhe. Rais Magufuli Jeshi lako la  Polisi liko imara tena imara kweli kweli, kwa kupambana na watu wote wanaotaka kuleta uvunjifu wa amani hapa nchini na kwa bahati nzuri wananchi wapo pamoja na wewe Rais na Jeshi lako.
" Ila naomba nitoe ushauri wa bure kwa wale wote wenye nia ya kuchafua amani ya nchi yetu , ni wasii waache mara moja na kama wataona ushauri huo hauna maana basi baadae tusilaumiane", amesema IGP Sirro.

Pamoja na hayo, IGP Sirro ameendelea kwa kusema "upo uhamasishaji kwenye mitandao, na hili niseme  naamini wameshaandamana kwenye mitandao na wameshamaliza maandamano yao. Kwa hiyo la msingi sana tujenge nchi yetu".

Kwa upande mwingine, IGP Sirro amesema katika kipindi cha mwezi Januari hadi Februari mwaka 2018 kuna jumla ya matukio ya jinai yaliyoripotiwa ni 96,363 ikilinganishwa na matukio 104,073 yaliyoripotiwa kipindi kama hicho mwaka 2017.
Read More

Taharuki Shinyanga : ALIYEVAA KIASKOFU NA KUSHIKILIA BIBLIA ,MAJEMBE AZUIA MAGARI BARABARANI,TAZAMA PICHA

Taharuki ya aina yake imetokea katika eneo la Sisi kwa Sisi ‘Ushirika’ barabara ya Shinyanga kwenda Mwanza mjini Shinyanga baada ya mwanaume ambaye hajajulikana jina wala makazi yake aliyevaa nguo nyekundu za kiaskofu akiwa amebeba silaha za jadi kusimamisha magari barabarani.

Tukio hilo lililodumu kwa takribani dakika 45 limetokea leo Jumamosi Aprili 7,2018 saa tano asubuhi.

Mwanaume huyo anayekadiriwa kuwa na miaka zaidi ya 40 alikuwa amevaa nguo nyekundu,kofia nyekundu yenye msalaba,biblia,mito,midoli,msumeno,baiskeli na majembe yenye mipini ya nondo.

Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog kuwa jamaa huyo alifika katika eneo la Ushirika karibu na ofisi za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kisha kusimama kwenye eneo la kuvukia ‘Zebra’ akaanza kusimamisha magari.

“Alifika hapa akiwa amevaa joho jekundu la kiaskofu pamoja na kofia nyekundu yenye msalaba huku akiwa ameshikilia biblia,baiskeli,msumeno na majembe,akatandaza barabarani vitu alivyokuwa navyo akawa anasimamisha magari huku akisema yeye ni Malkia wa Nguvu ametumwa na Mungu kuja Kukomboa nchi ya Tanzania,wameeleza mashuhuda wa tukio hilo.

Aidha wamesema wakati akisimamisha magari alisikika akisema bado usiku ,hapajakucha wasiendelee na safari na kwamba yeye ametumwa kuja kukomboa nchi.

“Alisimamisha kila gari pande zote mbili,akasababisha foleni ndefu,dereva wa basi la Mgamba lililokuwa linatoka Mwanza alipogoma kusimama ndipo jamaa akapasua kioo cha mbele akitumia majembe yake ambayo yamechomelewa nondo”,waliongeza mashuhuda.

Kufuatia taharuki hiyo jeshi la polisi lilifika eneo la tukio na kumkamata mwanaume huyo ambaye alionekana kutokuwa na wasiwasi wowote akisema wampeleke tu kwenye vyombo vya sheria kwani yeye hana kosa bali amekuja kukomboa nchi.

Hata hivyo inaelezwa kuwa jana jamaa huyo ambaye hajulikani ametokea wapi alionekana eneo la Ushirika akiwa amevaa kanzu nyeupe na kofia 'kibaraghashia' na hata juzi alifika katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga zilizopo hapo Ushirika.

Mwanaume aliyevaa nguo nyekundu baada ya kuvua joho jekundu akiwa amesimama katika eneo la kuvukia Zebra eneo la Ushirika barabara ya Shinyanga - Mwanza baada ya kuvua joho lake jekundu na kubakiza tisheti na kaptura nyekundu . Pichani ni vifaa alivyokuwa navyo ikiwemo baiskeli,mfuko mwekundu,biblia,midoli,biblia na nguo nyekundu -Picha na Malunde1 blog
Jamaa akichezea mdoli barabarani
Mwanaume huyo akiwa ameshikilia msumeno na jembe akizuia magari yasipite
Jamaa akisimamisha magari
Jamaa akisimamisha mabasi
Jamaa akisimamisha basi
Askari polisi wakimwondoa barabarani jamaa huyo akiwa amevaa nguo nyekundu na kofia yenye msalaba
Askari polisi akiokota vifaa vya jamaa huyo ambavyo ni biblia,mto,nguo na mdoli
Askari polisi akiwa ameshikilia majembe ya jamaa huyo
Askari polisi akiruhusu magari yaendelee na safari
Mwanaume huyo akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kuondolewa barabarani.Nguo nyekundu hapo chini ni joho lake la kiaskofu alilolivua baada ya kuanza kusimamisha magari
Mwanaume huyo akiwa chini ya ulinzi wa polisi 
Mwanaume huyo akipelekwa kwenye gari la polisi
Askari polisi wakimpeleka jamaa huyo kwenye gari la polisi
Mwanaume huyo akipelekwa kwenye gari la polisi
Jamaa akipanda kwenye gari la polisi
Askari polisi akiwa ameshikilia msumeno na majembe mawili ya mwanaume huyo
Jamaa akiwa kwenye gari la polisi
Wananchi wakishuhudia tukio hilo
Mwanaume huyo akiondoka na polisi
Read More

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein Ajumuika na Wananchi wa Zanzibar Katika Kisomo cha Kumuombea Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi wakati alipowasili katika ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo katika Kisomo cha Khitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 7 April baada ya kifochake,(kulia) Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Majaliwa Kassim Majaliwa,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe.Majaliwa Kassim Majaliwa wakati alipowasili katika ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo katika Kisomo cha Khitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 7 April baada ya kifochake
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na  Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji  wakati alipowasili katika ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo katika Kisomo cha Khitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 7 April baada ya kifochake









Read More
Powered by Blogger.

Hot

© Copyright KAHAMA 24