Waziri Ndalichako atoa agizo kwa shule binafsi

MATANGAZO

MATANGAZO

Serikali imewataka wamiliki wa shule binafsi nchini kutumia ujuzi na uzoefu wao katika nyanja ya elimu ili kuishauri Serikali nini cha kufanya ili kiwango cha elimu inayotolewa hapa nchini kuendelea kukua.


Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa JOYCE NDALICHAKO amesema hayo Mjini Dodoma alipokuwa akifungua mkutano wa Chama cha Wamiliki wa shule binafsi na kuongeza kuwa ni jukumu la jamii nzima kuhakikisha elimu nchini inakuwa.
Nao baadhi ya wamiliki wa shule binafsi wamesema kuna mambo mengi ambayo Serikali inaweza kujifunza kutoka katika shule hizo na kuzifanya shule za Serikali ziwe zinafanya vizuri katika mit i hani ya kitaifa kama zilivyo za binafsi.
Mkutano wa siku moja umeshirikisha wamiliki wa shule binafsi kutoka nchi nzima, lengo kuu likiwa ni kuangalia mafanikio na matatizo ambayo shule binafsi nchini zinakabiliwa nazo.