Rais Magufuli aahirisha ziara yake ya Zambia.

MATANGAZO

MATANGAZO
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha ziara ya siku tatu ya kwenda Zambia ambapo pamoja na mambo mengine alikuwa ahudhurie sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa sita wa Zambia Edgar Chagwa Lungu. Rais Magufuli amechukua huo uamuzi ili aweze kushughulikia madhara ya tetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya watu 16, kujeruhi watu zaidi ya 120, kuharibu nyumba zaidi ya 284 na miundombinu na uharibifu mkubwa wa mali.

 Rais Magufuli amemtuma Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kumuwakilisha ambapo sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa sita wa Zambia zinatarajiwa kufanyika tarehe 13 September 2016 kwenye mji wa Lusaka.