SAKATA LA SAKAYA KUSIMAMISHWA CUF LAMTOKEA PUANI NDUGAI,WABUNGE WAMSHAMBULIA KWA KULIINGILIA..!!!

MATANGAZO

MATANGAZO
WABUNGE sita wa upinzani jana walimshambulia vikali Spika wa Bunge, Job Ndugai, baada ya kukosoa hatua iliyochukuliwa na uongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) kuwasimamisha uanachama wabunge wake wawili hivi karibuni.

 
Mwishoni mwa mwezi uliopita, chama hicho kilisimamisha uanachama wa Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya na wa Mtwara Mjini, Maftah Nachuma kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.
Mbali na wabunge hao ambao kusimamishwa kwao na kufukuzwa kunakoweza kutarajiwa hatimaye kutapoteza sifa za kushika wadhifa huo, CUF ilimsimamisha pia Mwenyekiti aliyejiuzulu, Profesa Ibrahim Lipumba.
Ndugai alisema kufukuza Mbunge kutoka uanachama kuna athari za kiuchumi kwa taifa kwa sababu "ni gharama kubwa sana kumpata mbunge mwingine.""Ni gharama kwa serikali."
Baada ya maelezo ya Ndugai ambaye jana aliongoza kikao cha pili tangu arejee kutoka India alikokwenda kwa matibabu miezi minne iliyopita, wabunge sita kutoka upinzani walisimama na kuomba mwongoza wa Spika.
Aidha, wawili kati ya wabunge sita hao walitaka Ndugai aeleze alikotoa mamlaka ya kuingilia shughuli na katiba za vyama vya siasa.
Wabunge waliomvaa Spika ni Sakaya mwenyewe, Katani Katani (Tandahimba-CUF), Frank Mwakajoka (Tunduma-Chadema), Susan Lyimo (Viti Maalum-Chadema), Pauline Gekul (Babati Mjini- Chadema) na Mwita Waitara (Ukonga-Chadema).
Ndugai alijitetea hata hivyo, kwamba "Haya ni maelezo yangu binafsi ndiyo maana nimeomba radhi mapema kabla ya kutoa maoni haya.