Visamkasa: Nazi yagoma kuvunjika, Wachezaji waingia mitini

MATANGAZO

MATANGAZO
IMANI za kishirikina bado zimeendelea kutawala katika soka la mchangani baada ya hivi karibuni timu ya Chandimu kushindwa kuingia uwanjani kutokana na nazi waliyopewa na mganga wa kienyeji kugoma kuvunjika wakiwa njiapanda.
Tukio hilo la ajabu lilitokea hivi karibuni ambapo timu hiyo ina kawaida ya kuendekeza imani ya kishirikina, ilipofika njiapanda ambako wachezaji wote hushuka na kuanza kunena maneno waliyoelekezwa na mganga wao, kisha kuibamiza chini lakini cha ajabu nazi ilidunda kama mpira.

“Mganga alisema kabla ya kuingia uwanjani twende njiapanda tukavunje nazi na ikivunjika uhakika wa ushindi unakuwa mkubwa, lakini ikishindikana tutafungwa si chini ya mabao 6-0.
Baada ya nazi kushindwa kupasuka viongozi wakasema hakuna haja ya kwenda kuaibika uwanjani tukarudi nyumbani,” alisema mmoja ya wachezaji wa timu hiyo ambaye hakutaka kutaja jina lake.