Wakonta Kapunda, Binti Aliyekuwa Akiandika Kwa ulimi, Apata Kifaa cha Kisasa

MATANGAZO

MATANGAZO


Wakonta alipata ajali siku ya mahafali yake ya kidato cha sita miaka minne iliyopita. Ajali hiyo ilimuacha akiwa amepooza kwanzia shingoni kushuka chini na kumfanya kutoweza kutumia mkono

Wiki kadhaa zilizopita, BBC iliporusha habari yake Msamaria Mwema mmoja aliguswa kumsaidia
Kupitia kipindi cha televisheni cha Focus on Africa katika BBC World Service, mwanadada Olivia Soko kutoka Afrika ya Kusini aliguswa kufanya kitu kumsaidia Wakonta.

Akiwa mkurugenzi wa kampuni ya Whirlmarket Technologies, Olivia alijitolea kutoa msaada wa programu ya kompyuta iitwayo Nuance Dragon Naturally Speaking.

Jinsi Program hii inavyofanya kazi ni kwamba mtumiaji yeye anazungumza anachotaka kukiandika kupitia kipaza sauti chake halafu programu hii inaandika yenyewe katika kompyuta ya mtumiaji
Wakonta alijaribu kuitumia jana, akaifurahia, lakini bila shaka atahitaji muda zaidi ili aizoee vizuri.
Familia yake pia imefurahishwa sana na msaada huu.