Watu waamua kulala nje ya nyumba Bukoba baada ya Tetemeko Kutokea kwa Mara ya Pili
September 10 2016 lilitokea tetemeko la ardhi Kagera kanda ya ziwa Tanzania lenye kipimo cha 5.7 na kusababisha vifo vya watu 16 na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa ambapo ndani ya saa 24 baadae (September 11 saa tano kasoro usiku) likatokea tena tetemeko jingine.
Tetemeko hilo la pili ambalo ni dogo halijaripotiwa kusababisha majeruhi au vifo mpaka usiku wa saa nane lakini limeleta hofu kwa wakazi wa Bukoba ambao baadhi wameamua kutoa magodoro nje ya nyumba zao na kulala kwa kuhofia tetemeko linaweza kutokea tena usiku na kuwakuta ndani ya nyumba zao.
No comments:
Post a Comment