Marekani yatangaza vikwazo dhidi ya Warusi 38 na makampuni ya Urusi
Ikulu  ya Marekani, White House imetangaza vikwazo dhidi ya Warusi 38 na  makampuni, ikisema Marekani inakabiliana na kile kinachoendelea ikiwa ni  mbinu za Serikali ya Urusi  za “vitendo vya kuvuruga” demokrasia nchi  za Magharibi na ulimwenguni kote.
Katika  muhtasari alioutoa msemaji wa White House Sarah Huckabee Sanders Ijumaa  amesema Marekani bado inataka kushirikiana naUrusi
“Pia,  kile tunachotaka kukiona ni serikali ya Urusi ibadilishe mwenendo wake  kikamilifu. Tunataka kuendelea kuwa na mazungumzo na kufanya kazi siku  za usoni kwa kujenga mahusiano mazuri,” Sanders amesema.
Vikwazo  hivyo vitawekwa dhidi ya makampuni saba ya Urusi – ikiwemo Oleg  Deripaska, kampuni ya aluminium ambayo ni mshirika wa karibu na Rais  Vladimir Putin- na makampuni mengine 12 ambayo wanayamiliki au  kuyahodhi.
Pia  maafisa 17 wa serikali ya Urusi, na kampuni ya kutengeneza silaha  inayomilikiwa na serikali ya Urusi na kampuni zake tanzu, benki ya  Urusi, pia zitalengwa na vikwazo hivyo.

No comments:
Post a Comment