Mbowe Atua Bungeni Kutoa Msimamo Wa Ukawa Kushiriki Bunge
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ametua bungeni mjini Dodoma leo kuongoza kikao ambacho pamoja na mambo mengine kitatoa msimamo wa wabunge wa Umoja wa Katiba ya Watanzania (Ukawa), kushiriki au kutoshiriki vikao vya Bunge la Bajeti linaloendelea na vikao vyake mjini humo.
Mbowe pamoja Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa ambao pia ni miongoni mwa viongozi wa chama hicho waliopata dhamana jana katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi saba wa chama hicho, wamewasili bungeni leo mchama na kuingia moja kwa moja katika Ukumbi wa Msekwa kwa ajili ya kikao hicho.
Baadhi ya wabunge wamesema kikao hicho kinatarajia kutoa hatma ya kambi hiyo kushiriki mkutano huu wa Bunge la Bajeti na masuala mengine ambayo yatatikisa.
Tangu kuanza kwa vikao vya Bunge la Bajeti juiz Jumanne, wabunge wa upinzani wameonekana kususia bunge hilo huku idadi ya wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF) pelee wakionekana kwa uchache wakati viti vya wabunge wa Chadema vikiwa vitupu.
No comments:
Post a Comment