Rufaa ya Wambura yagonga mwamba.......Ataendelea na Kifungo

MATANGAZO

MATANGAZO
Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF imetupilia mbali rufaa ya aliyekuwa makamu wa Rais wa shirikisho hilo Ndg. Michael Wambura aliyefungiwa maisha kutojihusisha na soka mapema mwezi Machi.

Taarifa ya TFF leo, imeeleza kuwa baada ya kupitia hoja zake za kukata rufaa kamati imejiridhisha na maamuzi ya awali yaliyotolewa na Kamati ya Maadili ya kumfungia Maisha.‬

Machi 14 Wambura akiwa Makamu wa Rais wa TFF alifikishwa kwenye kamati hiyo kwa masuala ya kimaadili, akikabiliwa na makosa matatu kupokea fedha za shirikisho malipo yasiyo halali, kugushi barua na kushusha hadhi ya Shirikisho.

Machi 15 Kamati ya Maadili ya TFF ilimfungia Michael Wambura kifungo cha kutojihusisha na mpira wa Miguu maisha kwa mujibu wa kifungu cha 73(1) (c) cha Kanuni za Maadili ya TFF Toleo la 2013. Baada ya kupatikana na makosa matatu.

Mara kadhaa Wambura amekuwa akijitokeza hadharani na kuweka wazi kuwa hakubaliani na maamuzi hayo kwani hakupewa nafasi ya kujitetea na aliamua kukata rufaa lakini nayo imetupiliwa mbali leo.