Ghala la Kampuni ya Boss Shopping Centre likiteketea kwa moto jijini Dar

MATANGAZO

MATANGAZO
 Askari wa Kikosi cha Uokoaji cha Zimamoto wakizima moto uliokuwa ukiteketeza ghala la Kampuni ya Boss Shopping Centre Ltd zilimo kuwa zikihifadhiwa bidhaa mbalimbali eneo la Viwanda Chang'ombe jijini Dar es Salaam leo mchana.
 wananchi wakijadiliana jambo eneo la tukio.
 Kazi ya uokoaji ikiendelea.

 Askari wa uokoaji wakiwa kazini.
 
 
MOTO mkubwa umeteketeza ghala la Kampuni ya Boss Shopping Centre Ltd lililokuwa likitumika kuhifadhia bidhaa mbalimbali maeneo ya viwandani Chang'ombe jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio mmoja wa wamiliki wa ghala hilo ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa kuwa hakuwa msemaji alisema moto huo ulianza saa 9 mchana.

"Tumepata hasara kubwa katika ghala hili tulikuwa tukihifadhi friji, TV, sabufa kwa ujumla ni Boss Bland Home" alisema.

Alisema chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.

Baadhi ya waokoaji walikuwepo eneo la tukio walilalamikia Kikosi cha Uokoaji cha Zimamoto kwa kufika eneo la tukio bila ya kuwa na maji ya kutosha hivyo kushindwa kuhudhibiti moto huo kwa wakati ambapo ilizuka taharuki na kwa wamiliki wa viwanda vilivyokuwa jirani na ghala hilo.

Jitihada za gazeti hili kumpata Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro ili kuzungumzia tukio hilo hazikuzaa matunda baada ya kumpigia simu ambayo ilikuwa ikiita bila ya kupokelewa.