NYOTA YA MBWANA SAMATTA YAZIDI KUNG'ARA.

MATANGAZO

MATANGAZO
Usiku wa August 18 mtanzania Mbwana Samatta amefanikiwa kufunga bao kwa mara nyingine kwenye michuano ya UEFA Europa Leagua wakati klabu ya ya KRC Genk ikicheza dhidi ya Locomotiva Zagreb ya Croatia kuwania kupangwa kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Samatta alifunga bao dakika ya 47 likiwa ni bao la pili kwenye mchezo huo, bao la kwanza la Genk lilifungwa na Leon Bailey kwa mkwaju wa penati na kuipa klabu hiyo ya Ubelgiji uongozi wa bao 2-0.
Lakini wenyeji walikuja juu na kusawazisha magoli yote na kushuhudia mchezo huo ukimalizika kwa sare ya magoli 2-2. Magoli ya Locomotiva yalifungwa na Mirko Marić kwa penati dakika ya 52 na dakika ya 59 Ivan Fiolić akaisawazisha Locomotiva.
Dakika saba kabla ya mchezo kumalizika Samatta alipumzishwa nafasi yake ikachukuliwa na Karelis.
Mchezo wa marudiano utapigwa August 25 huku safari hii Genk wakiwa kwenye dimba lao la nyumbani  Cristal Arena kuwaalika Locomotiva Zagreb kwenye mchezo ambao Genk watakuwa wakihitaji ushindi, sare ya 0-0 au 1-1 ili kusonga mbele moja kwa moja.