POLISI WAMHARIBIA MAKONDA. ASHTAKIWA KWA RAISI MAGUFULI.
Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Msamaha kwa Wafungwa (Parole), Augustine Mrema amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Simon Sirro ni lazima wawawaondoe polisi jamii mitaani haraka, vinginevyo atatua kwa Rais Magufuli kuwasemea.
Mrema amesema hayo wakati akizungumza na wakazi wa Tandale ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukutana na makundi mbalimbali na kusikiliza kero zao.
Ametoa msimamo huo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wakazi hao kutokana na kero wanayoipata kutoka kwa polisi jamii ambao wanashirikiana na polisi.
No comments:
Post a Comment