TUKIO LA KUPATWA KWA JUA LINALOTAZAMIWA KUTOKEA SEPTEMBA MOSI, MJI WA RUJEWA MKOANI MBEYA NDIO SEHEMU PEKEE LITAONEKANA VYEMA

MATANGAZO

MATANGAZO
WATU Mbalimbali wakiwemo watalaam wa anga, wanasayansi,wanafunzi, wanavyuo na makundi mengine  kutoka duniani kote wanatarajia kushuhudia tukio la kihistoria la kupatwa kwa jua katika Mji wa Rujewa wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya Kusini Magharibi wa Tanzania.

Tukio hilo ambalo ni nadra kutokea  linatarajiwa kutokea septemba 1, mwaka 2016  katika maeneo mengi ya dunia, lakini mji wa Rujewa ndiyo eneo pekee ambapo kupatwa kwa jua kutaonekana vizuri zaidi kuliko maeneo mengine.

Kupatwa kwa jua katika mji wa Rujewa kutatokea siku ya Alhamisi, Septemba 1, saa 4:17 asubuhi hadi 7:56 Adhuhuri na eneo hilo litaonekana kwa asilimia 90 hadi umbali wa kipenyo cha km 100 ambapo pia watu wa maeneo hayo wanaweza kujionea kupatwa kwa jua.
Ikumbukwe kuwa  tukio kama hilo lilitokea Julai 31, 1962  takribani miaka 50 iliyopita na tukio lingine lilitokea April 18, 1977.
 
Watalaam wa anga wanasema tukio kama hilo litatokea tena nchini Tanzania  Mei 21, 2031 takribani mika 15 ijayo  na miaka 48 ijayo ambapo itakuwa Februari 17, 2064.

Mbali na kushuhudia kupatwa kwa jua wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchini watakaotembelea katika mji wa Rujewa wataweza kujionea shughuri kubwa za Kilimo cha Mpunga kwa kutembelea mashamba makubwa ya mpunga ya wananachi wa kawaida na mashirika pamoja na kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha iliyokaribu sana na mji huo wa Rujewa.

Pia wageni hao wataweza kujionea madhali nzuri za Bonde la Usangu katika safu za Milima ya Chunya na eneo la makao ya aliyekuwa Mtemi wa Kabila la wasangu Chifu Merere katika Kijiji cha  Utengule-Usangu pamoja na  vivutio vingine katika mkoa wa mbeya na mikoa jirani na Tanzania kwa Ujumla.

Wenyeji wa Bonde la Usangu ambao ni wasangu ni moja ya makabila yenye ukarimu mzuri nchini Tanzania  na wageni watakaotembelea katika mji huo watajifunza mila na tamaduni za Kabila hilo  la Wasangu