RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 5 & 6
Muandishi : Eddazaria g.Msulwa
Ilipoishia....
.....Rahabu akapunguza mwendo wa pikipiki na agnes akaruka na kukimbilia njia aliyo kwenda kibopa,rahab akapita njia aliyo kwenda muntar.Muntar akajibanza kwenye mti na kuokota gongo kubwa na kulishika kwa umakini.Gafla rahab akajikuta akiichia pikipiki na kuanguka chini hii ni baada ya kupigwa gongo la kifua na muntar akajitokeza mbele yake huku akiwa na gongo mkononi....
Edndelea....
.....Rahab akanyanyuka haraka,akamtazama muntar ambaye alianza kucheka kwa dharau akimtazama rahab kuanzia juu hadi chini.Muntar akarusha gongo kwa kutumia nguvu nyingi,rahab akalikwepa na kurusha teke lililotua shingoni mwa muntar na akaayumba,kabla hajajiweka sawa rahab akampiga muntar ngumi kadhaa za kifua na kuzidi kumfanya muntar kuyumba mithili ya mtu aliyelewa kwa pombe za kienyeji.(mataputapu).
Muntar akajaribu kurusha ngumi ila rahab akafanya maamuzi ya haraka katika kuudaka mkono wake wa kulia,akajigeuza na kwakutumia bega lake akauvunja mkono wa muntar.Kilio cha maumivu makali kikamkumba muntar.Pasipo kuwa na huruma rahab akampiga mtama muntar na kumfanya aliachie gongo alilolishika.Rahab akaliokota gongo na kuanza kumpiga muntar gongo la kichwa hadi damu nyingi zikaanza kutoka nje kwa kasi kama bomba la maji lililo pasuka sehemu ndogo.
Kibopa akafunga breki za miguu yake baada ya kukutana uso kwa uso na agnes.Kibopa akameza funda kubwa la mate huku mwili wake ukimtetemeka kiasi kwamba akabaki akiwa hajajua nini la kufanya.Agnes akaachia tabasamu pana baada ya kuiona surulia ya kibopa ikianza kuchora ramani ya kutota kwa mikojo aliyo shindwa kuizuia.
“ni....Iisssa...Mehe”
Kibopa alizungumza kwa kigugumizi kikali,agnes akapiga hatua hadi alipo simama kibopa na akamtisha kama anampiga ngumi ya uso,kwa woga uliokithiri ukammdondosha kibopa chini kama mzigo na akaanza kulia kama mtoto mdogo
“khaa wewe si jambazi,mbona unalia sasa?”
“mimi ni nilikuwa kibaraka waoo tuu,sioooo jambaazzziiii” kibopa alizungumza kwa kuyavuta vuta maneno kama amemeza fumba la uji wa moto na anashindwa kuumeza.Agnes akamtazama kwa huruma kipopa ambaye taratibu alianza kupiga magoti akimuomba msamaha.Agnes akampiga kofi la shavu kipopa na kumuamuru kusimama
“wenzenu wapo wapi?”
“wameshakufaa”
“changanya mbaliga zako,kabla sijabadilika”
“eheee....!!”
Agnes akampiga kibopa teke la makalio huku akimsindikiza na kofi la mgongoni na kumfanya kibopa aanze kukimbia kwa kasi kubwa.Agnes akabaki kucheka kwani hakutarajia kama ataweza kukutana na mwanaume muoga kama kibopa.
*****
Jackson luther mpelelezi anaye sifika kwa kazi yake nzuri akaanza kupandisha ngazi kwenda juu alipo anna kwa lengo la kumtia nguvuni kwa kosa la mauaji.Anna akaanza kukimbia akipandisha ngazi kwa kasi hadi akafika alipo waacha wezake.
“tuondokeni kimenuka”
Wakasaidiana kumkokota fety ambaye amechoka sana kwa kazi ya kupambana na karim pamoja na shamsa.Wakaingia ndani ya lifti na kushuka hadi gorofa ya kwanza,jackson akaitoa bastola yeka na kuwa makini zaidi,taratibu akaanza kuuunguza mwili wa muntar na kuhakikisha kwamba uhai wa mwili huo umesharudi kwa Mungu baba.
Kitu ambacho kinamchanganya jackson luther ni juu ya nani aliyeweza kumuua karim kwani ni miongoni mwa majambazi ambao alijaribu kuwafuatilia kwa kipindi kirefu pasipo kupata mafanikio ya aina yoyote katika kazi ya uchunguzi wake.Akapandisha hadi gorofa ya tano alipomuona anna akimalizikia na akakuta korido ikiwa haina mtu hata mmoja.
Akachunguza sehemu yote na kumkuta mtu aliye anguka chini akiugulia maumivu na mlango wa kuingilia chumbani kwake ukiwa upo wazi, akamsogelea na kumpa mkono na kumuinua kutoka alipokuwa.
“umepatwa na nini?”
“kuna wadada bwana hapa,walikuwa wakipigana na kuniangusha”
“umeumia?”
“ndio nimepiga kiuno chini.”
“wameelekea wapi?”
“hata sijui wametoka vipi humu ndani kwangu”
“sawa”
Anna,fetty na halima wakaingia kwenye jiko kuu la kupikia vyakula kwa kutumia mlango wa chini wakashuka kwenye ngazi na kutokezea upande wenye maswimcming pool katika hotel,wakawatizama watu waliomo ndani ya hotel na kuona hakuna anayewatilia mashaka kwa mwendo wa umakini wakaanza kuelekea kwenye sehemu lilipo gati la kuingilia hotelini.Kabla ya kutoka nje ya geti walinzi wakawasimamisha,kwa jicho la kuiba fetty kwa kupitia kioo cha dirisha la kijumba cha walinzi akaona video inayomuonyesha akipambana na shamsa kupitia kwenye tv ndogo iliyopo kwenye kijumba cha walinzi
*****
Rahab alipo hakikisha amekipasua kichwa cha muntar kwa kukipiga magongo,akatafuta sehemu chini ya mti na kukaa huku akiyasikilizia maumivu makali ya kifua aliyopigwa kutokana na kupigwa gongo.Agnes akaanza kumtafta rahab na kwabahati nzuri akamkuta akiwa amekaa chini ya mti
“shost umempata huyo mjinga?”
“ndio”
“umemuua?”
“hapana,nimemuachia aende zake kwa maana nimeona hana hatia.”
“mpumbavu kweli wewe,unadhani atashindwa kwenda kujipanga na kuja kutudhuru?”
“atatupatia wapi?”
“wewe mjinga nini?” rahab alizungumza kwa hasira kubwa.
“mpumbavu mwenyewe unadhani kila mtu ni wakumuua,mtu gani huna roho ya huruma”
“ila kumbuka ni nini tulichoamua”
“si tumesha kamilisha kama ni muntar kufa umesha muua,sasa kwa nini damu nyingine zije juu yetu pasipo kuwa na sababu ya msigi”
“katika siku ambazo ag nikuona kuwa wewe ni mjinga,limbukeni,poyoyo ni leo”
Rahab aliendelea kuzungumza kwa dharau iliyo changanyikana na hasira kali
“mimi poyoyo si ndio?” agnes alizungumza kwa hasira
“ndio wewe poyoyo”
Agnes akamsukuma rahab na kumfanya rahab kunyanyuka kama mbogo mkali aliye punyuliwa na risasi,akamrukia agnes kwa kutumia teke lake na kumuangusha agnes chini.Agnes akampiga mtama rahab na kumuangusha chini,wakaanza kushikana nywele zao na kuanza kuminyana huku wakipiga piga kelele.
“rahab nitakuua”
“niue kama unaweza”
Agnes akamuachia rahab nywele na akasimama.Rahab akamtazama kwa jicho kali agnes na akachia msunyo mkali
“rahab hebu tuache maswala ya kitoto,sisi ni marafiki kitu kinacho tufanya haswa tugombane ni nini?”
“wewe si ndio mzembe,unafanya vitu vya kijinga”
“sio vitu vya kijinga,kuna mambo yakufanya na mengine sio ya kufanya.Hivi rohoni mwako unaroho gani hadi umuue mtu asiye ha hatia”
“agnes hebu mtazame yule mjinga alivyokuwa akitumiminia risasi,unadhani angetuua ingekuwaje?”
‘ila haijawa,cha msingi tufanya mpango turudi tunapo ishi”
Agnes akampa mkono rahab na kumnyanyua,wakauvuta mwili wa muntar na kuuficha kwenye kichaka.Agnes akaikagua pikipiki na kukuta haijaharibika sana zaidi ya kuvunjika kioo cha pembeni cha upande wa kushoto.Agnes akaiwasha pikipika na rahab akapanda kwa nyuma na kuondoka porini na kutokea barabara kuu iendeyo mikoani na safairi ikaendelea
*****
“hamruhusiwi kutoka humu ndani”
Mlinzi mmoja alizungumza huku akiwazuia anna,fetty na halima wasitoke,wakaongezeka walinzi wawili wakasimama mbele yao huku mikononi wakiwa na bunduki zao
“kwa nini,huturuhusiwi kutoka?” anna aliwahoji
“kwa sababu maalumu.Tunawasubir......”
Fetty hakumuacha mlinzi kumaliza sentensi yake,akamtwanga kichwa kilichomfanya mlinzi kuishika pua yake iliyoanza kuvuja damu.Kwa shambulio hilo walinzi wengine wakawa wameduwaa kumuona mkubwa wao akivujwa na damu.Anna na halimwa kwa utaalamu mkubwa wakawapokonya walinzi bunduki zao,
“polisi”
Sauti ya jackson luther ikasikika kwa nyuma ikiwaamrisha fetty na wezake kutulia kama walivyo huku akiwa ameishika bastola yake kwa umakini.Anna akageuka kwa haraka na kufyatua risasi moja iliyompiga jackson luther kwenye paja la mguu wa kushoto na kumfanya aanguke na bastola ikaangukia mbali na alipo.
Mlinzi mmoja akajaribu kumrukia halima ila risasi ya bunduki iliyotua tumboni mwake ikamfanya arudishwe nyuma na kuanguka kama mzigo wa kuni.Macho ya jackson luther yakatazama na macho ya anna akajaribu kuunyoosha mkono wake kwenye bastola yeka ila akastukia risasi nyingine ikitua kwenye mkono wake na kumfanya jackson luther kutoa ukulele mkali wa maumivu.
Fetty akamvuta kwa haraka askari aliye mpiga kichwa na kumchomolea bastola iliyopo kiunoni mwake.
“waamrishe wezako kutufungulia geti”
Fetty akamvuta kwa haraka askari aliye mpiga kichwa na kumchomolea bastola iliyopo kiunoni mwake.
“waamrishe wezako kutufungulia geti”
Fetty alizungumza huku bastola akiwa ameielekezea kwenye kichwa cha mkuu askari wa hoteli,akawaamrisha wezake waliopo kibandani na wakalifungua geti linaloendeshwa kwa umeme.Wa kwanza kutoka akawa ni halima,akawaamuru watu waliomo ndani ya gari la kifahari aina ya range rover linalo ingia kwenye hoteli.
Vijana wawili wa kiarabu waliomo ndani ya gari wakashuka na kulala chini.Halima akaingia na kuwasubiria fetty na anna ambao nao wakingia kwa na kuondoka hotelini wa kasi,gari mbili za polisi zilizokuwa zinafika hotelini baada ya kupigiwa simu na wasamaria wema zikaanza kuwafukuzia kwa nyuma.
Wakiwa ndani ya gari fetty akatoa simu na kumpigia dokta willim huku akizitazama kwa nyuma gari za polisi zinazo kuja kwa kasi
“vipi kazi imekwenda vizuri?”
“ndio ila kuna tatizo limetokea”
“tatizo gani?”
“tumezidiwa ng............”
“vipi kazi imekwenda vizuri?”
“ndio ila kuna tatizo limetokea”
“tatizo gani?”
“tumezidiwa ng............”
Fetty hakumalizia sentesi yake na akajikuta akijigonga kichwa kwenye kioo na gari yao ambayo ilikumbwa na lori la kubebea mchanga ambalo halima ajiribu kulipita kwa kupitia upande wa kushoto kinyume na sheria za barabara,gari ikaanza kuserereka ndani ya mtaro kwa kasi ya ajabu kwa ubavu wa kustoto aliopo fetty na kugonga kwenye karavati la barabara na kusababisha gari kuminyika minyika vibaya sana na gari moja ya polisi ikamshinda dereva wake kuwahi kufunga breki na ikajikuta ikiligonga lori kwa nyuma na kupenya chini ya uvungu wa lori na kusababisha askari wote sita waliopo ndani ya gari,miili yao kugawanyishwa vipande viwili
She is my wife(ni mke wangu)……6
Ajali hii mbaya ikaanza kuwakusanya wananchi waliopo jirani na eneo la ajali,kila mmoja akijaribu kujua ni nini kinacho endelea.Halima akawa wa kwanza kujichomoa ndani ya gari,sehemu kidogo ya paji lake la uso ikiwa imechanika kidogo na kumwaga damu.Anna akajiminya minya kwenye siti aliyoikalia na kufanikiwa kutoka nje ya gari.Ila ikawa ni tofauti kwa fetty ambaye amepoteza fahamu.Kabla hawajaanza kumsaidia kumtoa fetty wakashuhudia gari la polisi likisimama sehemu walipo pata ajali wezao na askari wote wakaruka ndani ya gari lao wakiwa na bunduki mikononi
“anna tuondoke”
“na fetty je?”
“twende nimekuambia tutarudi kumchukua”
Halima hakuwa na haja ya kubaki eneo la tukioa kwa maana tayari askari walishaanza kuwasaka.Wakajichanganya katikati ya askari na kuanza kukimbia kwa wakikatiza mitaani.Wakafanikiwa kufika nje ya baa moja na kumkuta mtu mmoja akishuka kwenye gari lake.Kabla hajaufunga mlango wa gari lake wakamvamia na kumuamrisha atoe funguo za gari lake
“nyinyi kama kina na......”
Jamaa hakumalizia sentesi yake akapigwa kigoti ya tumbo na anna akabaki akiwa amejishika tumbo,akazitoa funguo za gari lake aina ya ‘premore’.Anna akazichukua funguo za gari na wote wakaingia na kuondoka na kumuacha jamaa akipiga kelele za mwizi
“gari yangu ya mkopo ina wiki ya pili ile” jamaa alizungumza huku akimwagikwa na machozi,mbaya zaidi hakuna mtu aliyepo katika eneo la baa aliyeweza kutoa msaada wowote kwao
*****
Askari wakamchomoa fetty ndani ya gari na kumfunga pingu japo ajitambui kwa lolote.Wakamuingiza ndani ya gari lao na kumpeleka hospitali ya taifa muimbili huku akiwa chini ya ulinzi mkali.Wakamkabidhi kwa madaktari ambao pasipo kupoteza muda wakaanza kummuhudumia
“tunaomba mumfungue pingu za mikononi”
Daktari mmoja alizungumza na askari mmoja akatii ombi la daktari.Matibabu yakaanza kufanyika kwa haraka.Wakagundua fetty amepeta mstuko tuu uliomfanya kuweza kupoteza fahamu.
****
Pikipiki waliyopanda rahab na agnes haikuwa na mafuta ya kutosha,ikawazimikia maeneo ya saruji na kwa bahati nzuri wakapata lori linaloelekea dar es salaam ambalo linasafirisha mifuko ya saruji(cement).Wakafika eneo la kuingilia kwenye msitu kulipo na handaki lao.
Wakamuomba dereva kuwashusha,wakawashukuru na kuanza kutembea kwa miguu kuelekea ndani ya msitu, hii ni baada ya gari walilolipanda kuondoka.Japo kuna giza ila wakajiamini sana,wakiwa njiani gafla wakaona taa za gari zikija kwa nyuma yao.Gari ikasimama pembeni yao,anna akafungua kioo cha gari
“vipi nyinyi?”
“safi”
“ingieni ndani ya gari”
Rahab na agnes wakaingia ndani ya gari na safari ikaendelea.
“jamani fetty yupo wapi?” agnes aliuliza
“wee acha tuu,tumepata ajali mbaya”
“amekufa......!!?” rahab aliuliza kwa mshangao
“hajafa ila alipoteza fahamu na isitoshe,askari walikuwa wanatufukuza
“sasa itakuwaje jamani?”
“mmmm hapa nilipo mimi nimechanganyikiwa”
Wakafika kwenye handaki na kitu cha kwanza kukifanya ni kufungua tv yao kuangalia kama kuna taarifa yoyote inayo endelea.Hawakukuta chohote kinachoendelea
“hivi vyombo vya abari vya ajabu kama nini?”
Rahab alizungumza huku akiachia msunyo mkali na kuingia chumbani kwake.Agens akaanza kuwahudumia wezake majeraha waliyo yapata
“jamani tunafanyaje?”
“inabidi tujue ni wapi alipo fetty,ikiwezekana tukamuokoe sisi wenyewe pasipo msaada wa mtu yoyote”
Anna ilo ulilolizungumza ni kweli,ila ni wapi tutapata magari ya kutumia kwa maana hapa yanaitajika magari si chini ya matatu”
“mumezungumza na huyo babu?”
“nani?”
‘si huyo dokta”
“fetty ndio alikuwa akizungumza naye kabla ya ajali,ngoja”
Anna akatoa simu yake mfukoni na kumpigia dokta william
“anna mbona mmekuwa wazembe kiasi hicho?”
Sauti ya dokta william iisikika kwenye simu baada tu yakuipokea
“badala ya kutuuliza tunaendeleaj,wewe unajidai ukituambia kuwa sisi ni wazembe.Si ungeifanya kazi yako wewe mwenyewe?”
Anna naye alizungumza kwa hasira
“hata kama sijawafundisha hivyo,nyinyi mlitakiwa mtumie akili”
“akili ehhee”
Halima akampokonya anna simu na kuiweka sikioni mwake
“nisikilize wewe mzee kwa umakini,sisi hatukuwa na la kufanya zaidi ya kufanya kile tulicho kifanya.Sasa ni hivi tunakupa masaa mawili uje huku ukiwa na jibu ni wapi alipo pelekwa fetty la sivyo......Utaisoma namba kama ni ya kirumi,kichina au kimakonde.”
Halima akaikata simu na kumrudishia halima.
“jamani,mimi nimechoka ngoja nijipumzieshe”
Agnes alizungumza na kuingia ndani kwake.Anna na halima wakabaki wakiwa amejilaza kwenye masofa,kila mmoja akitafakari kitu cha kufanya akilini mwake
Asubuhi na mapema dokta william akawasili kwenye handaki.Hadi anaingia hakuna aliye msalimia zaidi ya kutazamwa kama kinyago
“habari yenu”
“salama”
“ehee agens vipi kazi ya tanga mmeifanikisha?”
“ndio ila kwa shida kubwa”
“ehee na nyinyi?’
“kwani hujui”
Anna alijibu kwa dharau huku akitafuna taratibu popkone zilizopo kwenye kifuko.Dokta william akashusha pumzi nyingi huku akiwatazama halima na anna.
“fetty yupo katika hospitali ya taifa muhimbili,ila yupo chini ya unagalizi mkubwa wa madaktari na askari wenye silaha kali”
“tutampataje?” anna aliuliza
“kikubwa ni kusubiri siku ambayo atasafirishwa kupelekwa gerezani
“alafu.....”
“ndio tunaweza kufanya harakati za kumuokoa”
“dokta hivi unadhani,mwezetu atajisikiaje.Kama atakaa hospitali mwaka basi tusubirie tuu?” anna alimuuliza dokta william huku akimtazama kwa macho makali
“sijamaanisha hivyo....”
“kwani hapa ulisemeje? Si umesema hadi siku atakayo pelekwa hospitali ndio tukamuokoe au?”
“anna kuwa mpole,”
“sio niwe mpole.Fetty kwetu ni muhimu sana kuliko unavyo fikiria”
“oya anna kausha mwanagu tumsikilize dokta atakacho kizungumza,kupanick haisaidii kitu” rahab alimkanya anna na akakaa kimya
“sikilizeni,fetty anataokolewa kesho hospitalini.Atasafirishwa muda wa saa mbili usiku kupelekwa gereza la segerea”
‘”ngoja kwanza,watapitia njia ipi?”
“kwa njia bado sijafahamu,ila watatumia magari matatu yanayo fanana.Gari moja atakuwepo fetty na gari mbili watakuwepo midoli inayo fanana na fetty”
“sasa hapo itakuwa vipi?”
“muda wote mutawasiliana na mimi,kutokana mimi ndio ninaye shughulika na utengenezaji wa madoli yanayo fanana na fetty”
“je niwapi sisi tutapata usafiri?”
“kuhusiana na hilo wala musijali,kikubwa ni kuwa makini kwa kila jambo na kitu kikubwa ni kujipanga vizuri.Sitaki kutoke tatizo la kijinga”
“sawa”
Dokta william akaondoka zake na kurudi jijini dar es salaam
*****
Gari tatu aina ya gvc zilizotolewa kama msaada kutoka katika serikali ya marekani na kukabidhiwa katika jeshi la polisi nchini tanzania.Zipo tayari nje ya hospitali ya muhimbili kwa ajili ya kumsafirisha fetty ambaye anahesabiwa kama jambazi sugu.Ulinzi mkali unazidi kuhimarishwa kwenye eneo zima la hospitali ya muhimbili kila gari linaloingia na kutoka ni lazima liweze kukaguliwa na askari.
Kuanzia majira ya saa kumi na mbili asubuhi waandishi wa habari wamepiga kambi katika hospitali ya taifa muhimbili kusubiria kumuona fetty ambaye amepata umaarufu katika wakati mchache,hii ni kutokana na mkuu wa jeshi la polisi kutoa siku kumi na mbili za kujisalimisha kwa halima na anna.
Anna,rahab,agnes na halima wapo tayari kwa ajili ya kazi moja tuu,yakumuokoa fetty kutoka mikononi mwa askari.Wote wanne wamevalia nguo nyeusi na viatau vya jeshi vyenye rangi nyeusi.Vifuani wamevalia majaketi ya kuzuia risasi kupenya.Kila mmoja katika suruali yake aliweza kuchomeka magazine zipatazo kumi zilizo jaa risasi za kutosha.Mabomu ya kurusha kwa mkono kila mmoja aliweza kubeba ya kutosha kadri ya mtu alivyo kadiria kuona yanamtosha kwa kazi iliyopo mbele yao.Kila mmoja alachukua bunduki anayo ipenda yeye mwenye.
“kila mmoja yupo tayari?” rahab aliuliza
“ndio”
Kwa pamoja wakaikutanisha mikono yao ya kulia wakiwa wakekunja ngumi huku viganja vyao vikiwa vimefunikwa na gloves ngumu za rangi nyeusi tuu
“kwa umoja tunaweza”
Waliizungumza kauli mbiu yao,inayowafariji kila wanapofanya jambo la pamoja
“jamani msiniache nife usiku wa leo”
Rahab alizungumza huku akiwatazama wezake machoni kwa umakini
“hakuna atakaye kufa,tunakwenda wanne na tunarudi watano” halima aliweka msisitizo
Wakakumbatiana kwa pamoja kisha wakaachiana.Wakaanza kutoka ndani y a handaki lao mmoja baada ya mwengine.Wakazitazama gari tatu zilizopo mbele yao aina ya ferrali zilizo letwa na dokta william alizoziagizia kutoka nchini china.Kutokana na uwezo wa kifedha alio nao dokta william gari hizo ziliweza kusafirishwa kwa haraka na kuingizwa tanzania kwa njia magendo zikipokelewa mpakani mwa kenya na tanzania uliopo mkoani tanga.Kila dereva ambaye aliweza kuzifikisha gari hizo kwenye handaki aliuawa kwa kupigwa risasi dokta william kwa lengo la kuficha siri ya lilipo handaki lao
“hei mnanisikia”
Anna alizungumza huku akikirekebisha kinasa sauti chake alicho kichomeka sikioni.Kila mmoja akamjibu amemsikia kutokana wote walikuwa na vinasa sauti hivyo ambavyo vinaweza kuwasaidia katika mawasiliano kati yao pamoja na dokta william.Wakaingia kwenye magari yao huku anna akiwa gari moja na agnes.Halima na rahab kila mmoja akiwa ndani ya gari lake.Saa zao za mikononi zinawaashiria ni saa moja na nusu usiku.Na muda uliopangwa kwa fetty kupelekwa gerezani ni saa mbili na dakika tano usiku.
Kwa mwendo kasi wa gari zao wakafika maeneo ya muhimbili na gari zao wakazisimamisha umbali kidogo kutoka lilipo geti la kuingilia hospitaini.Rahab kwa kutumia darubin akaweza kuyaona magari matatu meeusi yakitoka katika geti la hospitali huku mbele yao zikiwa zimetangulia pikipiki tatu za polisi.Gari zote zimefungwa vioo ambavyo ni vyeusi
“mnanisikia mabinti”
Sauti ya dokta william ilisikika katika vinasa sauti walivyo vichomeka masikioni mwa
“ndio”
“sasa sijui mumeshafika eneo la tuukio”
“ndio”
“mumeziona hizo gari zinazo toka?”
“ndio”
“zote zinamidoli,inayo fanana na fetty”
“sasa dokta mbona unatuchanganya sasa”
“tuli,kuna kagari chenye bodi chakavu aina ya taksi kitatoka kama dakika tano zijazo”
“hicho kigari ndipo alipo fetty”
“hapana”
“ila?”
“hicho kina askari wapelelezi wapatao wanne,ambao wao watapita njia za panya kuhakikisha wanakwenda kumpokea fetty maeneo ya kimara na fetty anapelekwa iringa na sio segerea kama tulivyo tarajia”
Anna akashusha pumzi nyingi kila mmoja hakujua kama lengo litabadilika
“hiyo ni plan b iliyo badilishwa muda mfupi kabla ya fetty kupelekwa segerea”
“yeye fetty anatapitishwa njia gani?”
“kuna bomba la maji machafu lililopo chini ya ardhi ndilo atakalo pitishwa fetty,askari waliopo kwenye bomba hilo wapo sita.Na wanatembea kwa miguu”
“duu,na zile gari tatu?”
“zile ni danganya toto.Na zile zote zinakwenda segerea na zitapita njia tofauti.Ninacho waambia mimi kiaminini”
“ni muda gani watatumia hadi kufika kimara?”
“kama lisaa na nusu kutokana wanatumia miguu”
“hiyo nayo ni mpya,sasa ni kimara gani kwa maana zipo nyingi?”
“kikubwa ifwateni hiyo taksi tena kwa umbali mkubwa na ikiwezekana muifwate kwa gari moja tuu ili wasistuke kwani wote waliopo humo ni watu hatari sana”
“tumekupata,baby’s kazi ni kwetu tondokeni” rahab alizungumza na gari zao wakaziwasha na kuondoka kwa mwendo wa kawaida
*****
Hata fetty mwenyewe hakutarajia kama atapitishwa kwenye bomba kubwa la maji machafu,ambalo maji yake yalizuiwa kwa muda ili kuwafanya wao kupita kiurahisi.Fetty akiwa kwenye vazi la kiaskari aliweza kufanana mavazi na askari wanao mshikilia.Tofauti yao iliyopo kati yao ni fetty yeye ni mualifu amefungwa pingu za mikononi na kufungwa cheni nene na ndefu miguuni ila askari wangine watano ni wanaume wenye silaha huku askari mwengine wa kike aliye tengenezwa sura kama fetty na kimo kikiwa ni sawa,ni tofauti sana kwa mtu yoyote kuweza kumgundua.Isitoshe na yeye amefungwa pingu za mikono ila miguuni hakufungwa kitu cha aina yoyote
Harufu ya maji machafu haikuwazudia wao kusonga mbele wakitumia tochi kubwa zilizo wasaidia kuona mbele.Akili ya fetty ikawa na kazi ya kumchunguza mmoja baada ya mwengine na akaapia akipata nafasi yoyote ni lazima ajiokoe kuliko kwenda kunyongwa kisiri kwani ndio mazungumzo aliyoyasikia wakizungumza askari kipindi amelazwa wodini.Gafla fetty akajiangusha na kujifanya amepoteza fahamu,kwa umahiri mkubwa akazibana pumzi zake na kuyafanya mapigo yake ya moyo kupoteza muelekeo.
“bosi tumepata tatizo,over”
Askari mmoja alizungumza kwa kutumia simu ya upepo
“tatizo gani? Over”
“amepoteza fahamu huyu binti,over”
“fanyeni chochote,ila muhakikishe munatoka naye,over”
“sawa mkuu.Over”
Askari mmoja mwenye mwili mkubwa akamnyanyua fetty na kunuweka begani mwake na safari ikaendelea.Fetty akayafumbua macho yake na kuona askari aliye mbeba ndio wa mwisho katika mstari wanao tembea,kwa ustadi wa hali ya juu,fetty akaichomeka mikono yeke katikati ya shingo ya askati,kwakutumia pigu akaanza kumnyonga askari huku akiwa ameninginia kwa nyuma.Mikoromo ya asakri ikawastua wezake waliopo mbele kitendo cha wao kugeuka wakamkuta mwenzo ndio yupo kwenye hatua za mwisho huku macho yake akiwa ameyatoa nje....
Itaendelea.......
No comments:
Post a Comment