RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 7 & 8
Muandishi : Eddazaria g.Msulwa
Ilipoishia
Askari mmoja mwenye mwili mkubwa akamnyanyua Fetty na kumuweka begani mwake na safari ikaendelea.Fetty akayafumbua macho yake na kuona askari aliye mbebe ndio wa mwisho katika mstari wanao tembea,Kwa ustani wa hali ya juu Fetty akaichomeka mikono yeke katikati ya shingo ya askati,kwakutumia pigu akaanza kumnyonga askari huku akiwa amening'inia kwa nyuma.Mikoromo ya asakri ikawastua wenzake waliopo mbele kitendo cha wao kugeuka wakamkuta mwenzo ndio yupo kwenye hatua za mwisho huku macho yake akiwa ameyatoa njee
ENDELEA
Askari mmoja akataka kufyatua risasi ila mkuu wa masafara akamzuia,Fetty akaiachia shingo ya askari huku akiwa amehakikisha kwamba askari huyo yupo kwenye hali mbaya sana.Askari mmoja akampiga Fetty kwa kutumia kitako cha bunduki na kumfanya Fetty ajikunje huku akitoa mguno mkali wa maumivu
“Kumbukeni kuwa,anahitajika akiwa hai”
Mkuu wao alizungumza
“Sawa mkuu,ila anahitaji kupata kibano kidogo”
Wakaendelea kumtazama mwenzo,ambaye hadi hapa alipo hali yake haipo vizuri sana.Vichwa vya askar vikaanza kupata moto kwani mwenzao ambaye alikuwa anakaribia kunyongwa ndio anaye fahamu njia ya bombo hilo japo imenyooka ila kuna sehemu mbele imegawanyika katika njia nne.Mwenzao anayejulikana kama inspector Julio hawezi kuendelea mbele na safari
“Mkuu kuna tatizo jengine limejitokea,Over”
“Nini tena inspector John? Over”
“Huyu binti alimkaba Inspector Julio,Over”
“Nyinyi mulikuwa wa hadi mwenzetu akabwe?”
Sauti ya mkuu wao ilizungumza huku akiwa anafoka,
“Mkuu alizimia,ndipo inspector Julio alipo amua kumbeba”
“Pumbavu zenu.Hakikisheni anatoka huyo binti,akiwa hai na Julio naye akiwa hai”
Fetty akatabasamu huku akiwatazama askari,kwani kwake kazi yake imeshaanza kuwa nyepesi kwani mtu ambaye anamuhofia ni huyu Inspector Julio,ambaye kwa mtazamo wake tu anaonekana ni mtu hatari sana katika swala zima la kutumia silaha.Askari mmoja akasimama mbele ya Fetty huku akiwa amempa mgongo akisaidiana na wezake katika kumpa huduma Inspector Julio,huku kazi yake ikiwa ni kuzifungua kamba za viatu vya Julio
Kwa umakini wa hali ya juu,Fetty akazichomoa funguo nyingi zinazo ning’inia kiunoni mwa askari huyo pasipo yeye mwenyewe kujua.Kwa bahati nzuri katika wingi wa funguo hizo zipatazo kumi na mbili,mbili ni funguo za pingu.
Macho ya Fetty yakawa na kazi ya kuwatazama askari jinsi wanavyo pata shida katika kumsaidi mwenzao ambaye hali yake inazidi kuwa mbaya.
Hakuna askari aliye kuwa na muda wa kumtazama Fetty kwani wanaamini kile kitako cha bunduki alicho pigwa kwenye tumbo,bado anaendelea kukisikilizia maumivu yake.Fetty akafanikiwa kufungua pingu za mikono pasipo askari yoyote kugundua.Akajaribisha kufungu mnyororo wa miguni ila akashindwa kwani hakuna funguo inayo ingiliana na kufuli alilo fungwa miguuni.
Macho ya Fetty yakawa na kazi ya kuwatazama askari jinsi wanavyo pata shida katika kumsaidi mwenzao ambaye hali yake inazidi kuwa mbaya.
Hakuna askari aliye kuwa na muda wa kumtazama Fetty kwani wanaamini kile kitako cha bunduki alicho pigwa kwenye tumbo,bado anaendelea kukisikilizia maumivu yake.Fetty akafanikiwa kufungua pingu za mikono pasipo askari yoyote kugundua.Akajaribisha kufungu mnyororo wa miguni ila akashindwa kwani hakuna funguo inayo ingiliana na kufuli alilo fungwa miguuni.
“Ja............ama..ani mmmim...i siwezi ku...pona.Ila,njia uki...oony......sha utaku...nja kulia...kwenye shimo lenye mlang....o wa....”
Inspector Julio alizungumza kwa shida na hakuweza kumalizia sentesi yake,mauti yakamchukua.
Inspector John akanyanyuka kwa hasira na kumfwata Fetty sehemu aliyo kaa.Kufumba na kufumbua akajikuta akirushwa juu kimo cha mbuzi tena beberu na kutua chini kama mzigo.
Hii ni baada ya Fetty kuikutanisha miguu yake kwa pamoja,Kisha mikono yake aliikita chini na kujizungusha kwa kasi kubwa.Askari walio salia wakiwa wanamtizama mkuu wao.Fetty akajinyanyua kwa haraka na kumvaa askari aliye mchomolea funguo,akaichomoa bastola ya askari huyo ambaye alijitahii kumpiga ngumi za mbavu Fetty
Inspector John akanyanyuka kwa hasira na kumfwata Fetty sehemu aliyo kaa.Kufumba na kufumbua akajikuta akirushwa juu kimo cha mbuzi tena beberu na kutua chini kama mzigo.
Hii ni baada ya Fetty kuikutanisha miguu yake kwa pamoja,Kisha mikono yake aliikita chini na kujizungusha kwa kasi kubwa.Askari walio salia wakiwa wanamtizama mkuu wao.Fetty akajinyanyua kwa haraka na kumvaa askari aliye mchomolea funguo,akaichomoa bastola ya askari huyo ambaye alijitahii kumpiga ngumi za mbavu Fetty
Bila ya huruma Fetty akafyatua risasi iliyo penya kwenye kichwa cha akari anayepambana naye na kumtuliza kimya.Askari watatu wa kiume wakazikoki kwa haraka bunduki zao na kuanza kuzifyatua risasi,ila kwa haraka sana kama tairi la gari liendalo kwa kasi sana,akawa na kazi ya kubiringika huku akiwafwata askari kwenye miguu yao mita chache kutoka alipo.
Akiwa anabiringika, bastola iliyopo mkononi mwake ikawa na kazi ya kufyatua risasi zilizo waangusha askari watatu chini na akabaki Inspector John na askari wa kike aliyetengenezwa kama yeye,na wakati wote tukio la wezake kuangamizwa lilimpa kiwewe hadi akawa na kazi ya kuyaziba masikio yake akiziba asisikie milio ya risasi.Fetty akalala katikati ya miguu ya Inspector John huku mdomo bastola yake akiwa ameuweka kwenye sehemu za siri za Inspector John.Bunduki ya inspector John akawa ameilekezea kwenye kichwa cha Fetty ambaye macho yake yanatazamana na macho ya Inspector John
“Shoot ni kushooti”
Fetty alizungumza huku akitabasama,na bastola yake akawa na kazi ya kuigusisha gusisha kwenye vitenesi vya Inspector John
*************
Gari waliyopanda askari wapelelezi ikazidi kuongeza mwendo,huku kila mmoja akiwa na bastola yake mkononi.Kwa uelewa wao mkubwa katika kazi yao ya upelelezi wakagundua kuna gari tatu ambazo kwa Tanzania ni watu wachache sana ambao wanazimiliki kutokana na gharama zake kuwa ni kubwa sana.
“T upo tayari?”
“Ndio Y”
“l je?”
“Ndio Y”
“X je?”
“Ndio Y”
Askari hawa waliweza kupeana herufi za moja moja kurahisishana kuitana majina waliyo pewa kazini au na wazazi wao.
Y ndio kiongozi wao mkubwa ambaye ndio dereva wa gari hili ambalo kwa mtazamo wa bodi(umbo) lake la nje,inaonekana ni chakavu Ila injini yake na vifaa vingine ni vipya na inauwezo wa mwendo kasi 250 KM/H.
Kila mmoja akawa na kazi ya kuzitazama gari hizo zinazo wafwata kwa mwendo kama wanao kwenda nao
Y ndio kiongozi wao mkubwa ambaye ndio dereva wa gari hili ambalo kwa mtazamo wa bodi(umbo) lake la nje,inaonekana ni chakavu Ila injini yake na vifaa vingine ni vipya na inauwezo wa mwendo kasi 250 KM/H.
Kila mmoja akawa na kazi ya kuzitazama gari hizo zinazo wafwata kwa mwendo kama wanao kwenda nao
Rahab akiwa ametangulia gari lake mbele akawawashia wezake taa huku akikanyaga breki za gari lake,akiwaashiria wapunguze mwendo.
“Baby’s munanisikia?” Rahab alizungumza kwa sauti ya kawaida
“Tunakupata”
“Wale jamaa,ninamashaka nao wamestukia dili”
“Kwa nini?” Ann aliuliza
“Kwa maana mwendo wao ni wamashaka mashaka”
“Haya sasa,Plan B yetu ni nini?” Halima aliuliza
“Kuwavamia bwana kwa pamoja” Agnes alishauri
“Tukiwavamia tutampataje Fetty?”
“Sasa ishu inakuwa vipi?” Rahab alizungumza
“Tuwafwateni tu” Anna alishauri
“Oya gari zetu,si zina map direction?”
“Ndio”
“Rahab wewe uliopo mbele tuambie,namba za gari la hao jamaa ni ngapi?”
“T234KSJ”
“Tuiingizeni hiyo namba kwenye hizi ramani zetu tutaweza kuiona kwa ishara hiyo gari kila inapo kwenda” Agnes alizungumza
“Sasa Ag wewe ndio mtaalamu wa hivi vitu sisi wezako wala hatujui”
“Ok,ngoja niingize”
Agnes akaiingiza namba ya gari na kwamsaada wa satellite aliweza kuiona gari ya wapelelezi kila inapo kwenda huku ikionekana kwa alama nyekundu.
Akawaelekeza wenzake jinsi ya kufanya na kila mmoja pembeni ya mskani wa gari lake kuna kioo kidogo kilicho unganishwa na sateliti na kazi yake ni kuweza kuonyesha ramani ya sehemu ambayo unahitaji kwenda au gari unayo taka kuifwata sehemu ilipo kikubwa ni kuweza kuzitambua namba za usajili wa gari hilo.
Akawaelekeza wenzake jinsi ya kufanya na kila mmoja pembeni ya mskani wa gari lake kuna kioo kidogo kilicho unganishwa na sateliti na kazi yake ni kuweza kuonyesha ramani ya sehemu ambayo unahitaji kwenda au gari unayo taka kuifwata sehemu ilipo kikubwa ni kuweza kuzitambua namba za usajili wa gari hilo.
Wakaziendesha gari zao kwa mwendo wa kawaida na kuifanya gari ya wapelelezi kuzidi kutokomea,huku wakiwa hawana wasiwasi kuipoteza gari hiyo.
Wapelelezi wakaanza kupata matumaini baada ya gari tatu zinazo wafwata kuziacha nyuma sana.Gari ya wapelelezi ikafika Kimara Gas Station na wakashuka kwa haraka kwenye gari.Rahab na wezake wakalishuhudia gari la wapelelezi likiingia kwenye kituo cha gesi kilichopo Kimara.Wapelelezi wakaingia kwenye msitu wa miti ulipo hapo ambapo ndipo lilipo shimo ambalo wanatarajia kuwapokea Fetty na askari wengine
Wapelelezi wakaanza kupata matumaini baada ya gari tatu zinazo wafwata kuziacha nyuma sana.Gari ya wapelelezi ikafika Kimara Gas Station na wakashuka kwa haraka kwenye gari.Rahab na wezake wakalishuhudia gari la wapelelezi likiingia kwenye kituo cha gesi kilichopo Kimara.Wapelelezi wakaingia kwenye msitu wa miti ulipo hapo ambapo ndipo lilipo shimo ambalo wanatarajia kuwapokea Fetty na askari wengine
“Jamani tusishuke kwanza” Agnes alizungumza
“Kwa nini?”
“Hamuwezi kujua kama jamaa wamejificha wanatusubiria tushuke watushambulie”
“Hapo,umezungumza point”
Wakazisimamisha gari zao mbali kidogo na kilipo kituo cha gesi,wakisubiria kufanya kazi moja tu ya kuwashambulia askari hao pale watakapo mchukua Fetty
***************
Inspector Julio akaanza kutetemeka huku akimeza mafumba ya mate,kwani ni mwaka wa 25 sasa analitumikia jeshi la polisi,ila hajawahi kukutana na mwanake hatari kama Fetty.Kwa woga akajikuta akiminya kitufe cha kuziruhusu risasi kutoka,kwa bahari mbaya bunduki yake tayari imeisha risasi.
“Kwaheri”
Fetty alizungumza huku akiziruhusu risasi mbili kuchomoka kwenye bastola yake aina ya ‘browningu SFS’ na kuzichangua sehemu za siri za Inspector John,Fetty akasimama na kumtazama askari wa kike anaye fanana naye kuanzia mavazi hadi sura ya bandia aliyo valishwa.Fetty akataka kumuua askari huyo ila akasitisha zoezi lake na kumnyanyua
“Nipe funguo nijifungue”
“Zip.....o kwa inspector John”
Fetty akamtazama kwa umakini askari,akachuchumaa kwa umakini huku bastola yake akiielekeza kwa askari huyo anaye itwa Rehema.Akaipapasa mifuko ya Inspector John na kuzitoa fungua nyingi.Akachagua funguo moja inayoweza kufungua kwenye mnyororo,kwa bahati nzuri akaipata.Akajifungua na kumuomba Afande Reheme kutangulia mbele huku akiwa ameshika tochi inayowasaidia kuona mbele.Wakafika kwenye njia nne tofauti,wakabaki wakiwa wamesimama wakiwa hawajui ni wapi waende
“Sema njia ni ipi?”
“Sujui hata mimi”
Fetty akampiga kofi la shavu Afande Rehema huku akiwa amemnyooshea bastola
“Sema ni njia gani la sivyo nakumwaga ubongo?”
“Hii.....”
Afande Rehema alizungumza ili mradi aepukane na kifo cha kupigwa risasi.Japo amejitamkia ila njia aliyo ionyesha ndio sahihi.Wakaendelea na mwendo wao hadi wakafika sehemu yenye ngazi za chuma za kutokea nje.Fetty akamtanguliza afande Rehema japo amefungwa pingu za mikononi ila akajitahidi hivyo hivyo kuanza kupanda kwenda juu
*****************
Milio ya risasi waliyo isikia kupitia redio ya upepo,iliwachanganya sana wakuu wa polisi na kuwafanya waanze kubabaika na kuwapa taarifa wapelelezi kuwa kuna hali tete ambayo inaendelea chini walipo askari.
Mbaya zaidi kila wanapo jaribu kuwasiliana na wenzao hawakuweza kupata jibu la aina yoyote.Wapelelezi wakajiandaa kwa chochote kitakacho jitokeza kwenye shimo huku bastola zao wakiwa wameziandaa kwa umakini wa hali ya juu
Mbaya zaidi kila wanapo jaribu kuwasiliana na wenzao hawakuweza kupata jibu la aina yoyote.Wapelelezi wakajiandaa kwa chochote kitakacho jitokeza kwenye shimo huku bastola zao wakiwa wameziandaa kwa umakini wa hali ya juu
Wakauona mfuniko wa shimo,ukifunguliwa na kichwa cha Afande Rehema kikatokeza,
“Musiniue”
Afande Rehema alizungumza huku akijitoa kwa kasi kwenye shimo.Fetty akajua kuna hali ya hatari ipo juu,akaishika bastola yake vizuri na kupandisha ngazi kwa hataka kabla hajajitokeza juu akakiona kichwa cha mpelelezi mmoja akichungulia,Mpelelezi akiwa anashangaa kati ya Rehema na Fetty yupi ni muhalifu kwani wanafanana,akastukia risasi ikipiga kwenye paji la uso wake na kumuangusha chini
Milio wa risasi ukawastua Rahab na wenzake,kwa haraka wakawasha magari yao na kuyasimamisha pembeni ya kituo cha gesi.Wakashuka kwa haraka kila mmoja banduki yake ikiwa mkononi.
Walinzi wa kitua cha gesi wakazidi kuchanganyikiwa kwani mlio huo wa risasi umesikika nyuma ya kituo na watu walio ingia kwenye kituo chao hawaeleweki.Mlinzi mmoja akaikoki bunduki yake aina ya gobora,kitendo cha mlinzi kuishika bunduki yake,Anna alikiona vizuri,pasipo kuuliza ni nini mlinzi anataka kukifanya,akafyatua risasi iliyo muangusha mlinzi chini.Walinzi wengine wakalala chini kwa woga baada ya kumouona mwenzao akivuja damu nyingi
Wapelelezi wakabaki katika hali tata,huku kila mmoja akikataa kwenda kuchungulia kwenye shimo asije akakutwa na ktu kilicho mkuta X.
Wakiwa katika taharuki risasi zisizo na idadi zikatua mwilini mwao zikitokea nyuma yao na ukawa ndio mwisho wa maisha yao.Agnes akanza kupiga hatua za haraka akimfwata Afande Rehema aliye lala chini
Wakiwa katika taharuki risasi zisizo na idadi zikatua mwilini mwao zikitokea nyuma yao na ukawa ndio mwisho wa maisha yao.Agnes akanza kupiga hatua za haraka akimfwata Afande Rehema aliye lala chini
“Fetty nyanyuka tuondole”
Fetty alianza kushua ngazi kurudi kwenye shimo ila baada ya kuisikia milio mingi ya bunduki.
“Fetty twende”
Agnes alizidi kumuita Afande Rehema baada ya kumuona anababaika.Kabla Fetty hajamalizi kushuka kwenye ngazi ya mwisho kuingia kwenye shimo akaisikia sauti ya Agnes.
“Agnes huyo sio Fetty ni polisi mimi nipo humu”
Fetty alizungumza huku akianza kupanda ngazi kwa haraka,Agnes akabaki akiwa ameshangaa,akamuona Fetty akichomoza kichwa kwenye shimo.Afande Rehema akajaribu kuiokota bastola ya askari mmoja aliye anguka chini.Risasi kama sita zikatua mgongoni mwake kutoka kwa Rahab.Fetty akamkimbilia Agnes na kumkumbatia
“Pole shosti”
“Asante”
Kabla hawajaondoka,mwanga mkali wa helcopar ya polisi iliotumwa kufika kwenye eneo hilo,ukaanza kuwamulika.Wakaanza kukimbia wakielekea mbele ya kituo walipo ziacha gari zao, kitendo cha Halima kujitokeza wakakutana na gari zipatazo kumi za polizi zikiwa zimetanda mbele ya kituo na askari wengi wakiwa na bunduki zao wakiwa wameelekezewa wao.
“WEKENI SILAHA ZENU CHINI”
“Shitii”
Wote watano wakabaki wakiwatazama askari huku helcopar ya polisi ikiwa inawamulika kwa mwanga mkali mweupe ambao umelifanya eneo walilo simama wao kuwa kama mchana na endepo watafanya kitu chochote cha kijinga,askari wenye bunduki wapatao thelasini wenye bunduki watazifyatua risasi zao pasipo kuwa na huruma
SHE IS MY WIFE(NI MKE WANGU)……8
“Nini tunafanya”
Rahab aliwauliza wenzake,huku taratibu mikono yake akiwa anainyanyua juu.Kila kitu ambacho kinaendelea katika eneo la kituo cha gesi,Dokta William anakifwatilia akiwa amelisimamisha gari lake mbali kidogo na eneo walilopo askari.
Kwa haraka alifungua nyuma ya gari lake kwenye buti na kutoa bunduki yake yenye uwezo wa kupiga risasi kwa masafa marefu inayoitwa ‘THE BOR SNIPER’ yenye uzito wa kilo sita na urefu wa milimita 1,038 sawa sawa na nchi 40.9 za urefu.
Akaiweka chini pembeni ya gari lake,kisha akalala na kufungua kifuniko cha lenzi inayoweza kuvuta karibu,Uzuri wa hii bunduki yake unaweza kuona muda wowote hata kama kuna giza ila kwa kutumia mwanga wa kijani uliopo kwenye lenzi yake unaweza kuona vizuri bila shida.
Akaifunga kiwambo cha kuzuia sauti.Alipo hakikisha kila kitu kipo sawa,akwakavuta kwa karibu Rahab na wezake na kuwaona wamenyoosha mikono yao juu .Pembeni na walipo jipanga askari kuna tanki kubwa la gesi.Akapiga ishara ya msalaba kisha akafyatua risasi moja iliyoingia kwenye tanki la gesi.
Ndani ya sekunde mlipUko mkubwa wa gesi ukawarusha mbali askari karibia wote,mbaya mlipuko huo ukaendelezwa na magari yao yanayo tumia mafuta ya petrol na desel
Haikuwa kwa askari tu kurushwa,ila hata Rahab na wezake wakarushwa na kurudishwa nyuma walipo tokea.Halima akawa wa kwanza kunyanyuka,
“Jamani tuondokeni”
Alizungumza akiwahimiza weNzake,wakanyanyuka kwa haraka na kuanza kutokomea kwenye pori.Mitungi iliyo chimbiwa chini ya ardhi ikaanza kupata moto,mwisho wa siku ikaanza kulipuka mmoja baada ya mwIngine na kuzidi kusababisha vifo vya askari.Rubani anaye iendesha helcoptar ya polisi akachanganyikiwa sana,na jinsi moto unavyo waka.
Akaipeleka juu kidogo Helcoptar yake.Dokta William akaona kitendo cha rubani wa Helcoptar kuinyanyua juu.Akamvuta karibu rubani na bila ya huruma akamtandika risasi ya kifua na kumfanya aachie kila kitu alicho kishika na helcoptar ikaanza kurudi chini kwa kasi ya ajabu na kuingia kwenye moto mwingi wa gesi na kuzidi kuongeza mlipuko wa eneo la kituo
Dokta William akainyanyua bunduki yake kwa haraka na kuirudisha sehemu alipo itoa kwenye gari kisha akaingia ndani ya gari na kuondoka eneo alilopo,huku akilini mwake akiwa amejawa na mawazo mengi sana kwani kitendo ambacho amekifanya kwanza ni kinyume na sheria za nchi ya Tanzania pamoja na hata nchi yake ya Israel na endapo tukio hili litajulikana kama yeye ndio mtendaji mkuu atahukumiwa kifungo cha maisha jela au kunyongwa mbele ya halaiki ya watu.Kingine kinacho muumiza kichwa ni Fetty na wezake ambao aliwashuhudia wakirushwa na mlipoko wa tanki la gesi
Akatoa simu yake ambayo anawasiliana na Rahab na wezake.Akawapigia na kwabahati nzuri akazisikia sauti zao
“Mupo wapi?”
“Tupo kwenye haka kapori kalichopo nyuma ya kituo,tunakaribia kufika kwenye makazi ya watu”
“Sasa nyinyi,katokeeni katika barabara kuu maeneo ya Mbezi”
“Sawa”
Rahab na wezake wakabadilisha muelekeo na kuanza kukimbia kuelekea walipo elekezwa na Doktar Willian,ndani ya robo saa wakawa ameshafika Mbezi.Fetty kutokana amevaa nguo za polisi,ikawa ni nafasi nzuri kujitokeza barabarani kutazama ni wapi lilipo gari la Dokta William.
Dokta Willim akamuona Fetty na kumtambua mara moja,akawasha gari lake kwani alikuwa amelisimamisha pembezoni mwa bararaba.Akafika sehemu walipo Fetty na wezake na wote kwa haraka wakaingia ndani ya gari ya dokta William aina ya Ford na kuondoka kwa mwendo wa kasi
***********
Tangu mwaka 1961 nchi ya Tanzania ilipo pata uhuru hapakuwahi kutokea tukio la kinyama lililo husisha mauaji ya askari zaidi ya thelathini kwa wakati mmoja tena wakiwa wanapambana na jeshi la polisi,isitoshe kuna baadhi ya wanachi waliokuwa katika kituo hicho nao pia wamefariki dunia.Tukio hili likaingizwa katika matukio ya kigaidi.Vilio vingi vilitanda kwenye nyumba za askari ambao wamefariki,hivyo hivyo kwa wananchi walio fariki hali ilikuwa ni moja ya kuomboleza vilio
Magazeti ya serikali na udaku yakatawaliwa na taarifa ya magaidi kulitingisha jeshi la polisi.Moja ya magazeti linalo itwa Story Za Eddy likatawaliwa na kichwa cha habari kilicho wakera viongozi wengi serikalini
(UZEMBE WAUA ASKARI 30)
“Nitafutieni muandishi wa hili gazeti”
Mkuu wa polisi alizungumza kwa jazba,huku akiwatazama askari wake watatu walio simama mbele yake.Akaendelea kulipitia gazeti moja baada ya jingine kuangalia habari zilizo andikwa kwenye magazeti ya nchi hii.Akakutana na habari nyingine iliyo andikwa
(CHEZEA MAJAMBAWAZI WEWE,WAMEUNYUTI WENYEWE) Huku pembeni kukiwa na picha yake ya kikatuni ikitazama jinsi makatuni askari wakilipuliwa na moto wa gesi.Bwana Gudluck Nyangoi IGP wa polisi ikambidi kufumba macho yake na kuachana na habari ya kuyasoma magazeti ambayo yanazidi kuipandisha hasira yake.Akaitisha kikao cha wakuu wa jeshi la polisi nchi nzima na akawapa masaa manne wote wawe wamefika makao makuu ya polisi,hakujali wengine umbali wa mikoa yao ila tamko lake akaitaji lifanyiwe kazi mara moja
************
Katika siku walizo amka na furaha ni hii ya leo,Agnes akaingia jikoni na kuwaandalia wezake kifungua kinywa cha nguvu na wote wakakutana katika meza ya chakula,pamoja na dokta William
“Fetty hongera” Agnes alizungumza
“Na nini?”
“Nimekukubali sana,wewe ni noma”
“Ahaa mbona kawaida”
“Ahaa,hivi ulisema wale askari uliwafanya nini ndani ya mtaro?”
“Wazembe wale,sema wamekufa ila wangekuwa hawajafa ningewashauri warudi tena mafunzoni”
Wakati Fetty na Agnes wanazungumza,dokta William akawa na kazi ya kupitia habari zinazo endelea kwenye mitandao ya kijami,akianzia na Facebook
“Jamani mambo sio mazuri kabisa”
“Kwa nini?” Halima aliuliza
“Huko nje mnatafutwa kama nini”
“Wametujua?”
“Hakuna picha hata moja inayo waonyesha sura zenu ila ni habari tuu”
“Doktar picha ya Fetty je?”
“Huyu picha yeke niliiona tuu,ila haijaandikwa vibaya”
“Imeandikwaje?” Fetty aliuliza
“Iliandikwa anatafutwa”
Wakabaki wakiwa wanacheka na kumfanya Dokta William kushangaa
“Mnacheka nini......!!?”
“Si hivyo unavyo sema kuwa haijaandikwa vibaya sana...ila anatafutwa,Doktar sasa hapo unadhani hayo maneno ni mazuri?” Rahab aliuliza huku akicheka
“Sawa tusikilizane,mimi nitaondoka mara moja kwenda Israel nyumbani.Hii ishu ikipita nitarudi”
“Dokta,pesa yetu?”
“Hiyo pesa yenu mimi nitawaingizia kila mmoja kwenye akaunti yake”
“Hapa sote unapo tuona hakuna hata mmoja ambaye ana akaunti benki,sasa hatujajua kama kunauwezekano wa sisi kuipata hiyo pesa”
Anna alizungumza huku sura ya furaha ikiwa imepotea usoni mwake
“Nimewaelewa,kikubwa ni mawasiliano kati yangu mimi na nyinyi kwani hata nikiwa nje ya nchi nitaendelea kuwasiliana na nyinyi”
“Dokta mbona kama sijakuelewea? Ina maana pesa yetu ndio hakuna?”
Anna aliuliza huku akijiweka sawa kwenye kiti alicho kalia
“Pesa yenu ipo.Ila kwa kiasi cha pesa mbacho mnanidai chote kipo katika benki ya serikali ambayo kwa sasa akaunti zote zimefungwa kutokana na tukio la jana”
“Wewe kama wewe una kiasi gani kwenye hiyo benki?”
“Milioni mia sita”
“Mmmmm,wataifungua lini?”
“Hata mimi mwenyewe sijui”
“Wewe umejuaje?”
“Kuna mtu alinitumia meseji asubuhi”
“Ni nani?”
“Ni kiongozi wa juu,kwenye hiyo benki”
Swala la Dokta William kuto kuwa na pesa ya kumalizia kuwalipa Agnes na wenzake likaanza kumsumbua akili mmoja baada ya mwengine.Anna akanyanyuka na kuingia chumbani kwake na kurudi na bastola na kukaa kwenye kiti alicho kuwa amekikalia
“Dokta,tunakuamini tena sana.Ila mimi kwa hili bado hujanishawishi hata kidogo.Kwanza kumbuka sisi ni wasichana wadogo sana ambao kama tungeendelea kufanya kazi yetu ya kuiuza miili yetu tusinge tafutwa kwa mabaya kama hivi sasa.Sasa ninakupauchague vituu viwili,Uzungumze ni lini unatupa pesa yetu au uzungumze na huyu mjamaa hapa”
Anna alizungumza huku bastola akiiweka mezani,wenzake wote wakamtazama kisha wakamgeukia Dokta William
“Anna mimi nipeni masaa kadhaa nitawaletea pesa yenu”
“Huyu muongoo” Halima alidakia
“Siwadanganyi jamani”
“Mbona saa zote ulikuwa unajikenua kenua mbele yetu tuu?”
“Nilikuwa ninawapima kama mnaniamini au laa” Doktar William alizungumza kwa kujiamini
“Kuna vitu vya kudanganyana na vingine si vyakudanyanyana.Pesa ndio kila kitu bwana”
Fetty alizungumza huku akimtazama Dokta William kwa macho makali sana yasiyo na utani hata kidogo.Dokta William akasimama na kutoka nje ya handaki huku nyuma akiwa ameongozana na Fetty.Wakafika chini ya mti mmoja uliopo karibu sana na handaki lao,Dokta William akafukua kidogo na kutoa mfuko wa rambo ulio jaa pesa nyingi za kigeni.
“Duuu kumbe tunaishi na benki hapa ila hatujui chochote kinacho endelea”
“Si kutokana na nyinyi sio wachunguzi,mngejuaje”
Dokta Willia akampa mfuko Fetty na wote wakarudi ndani.Dokta William akawalipa kila mmoja kiasi chake anacho hitaji kulipwa.
“Jamani ninaondoka Tanzania leo.Mtajua ni nini cha ufanya na hizo pesa.Ila kwa ushauri sasa hivi ninawaomba msitembee tembee sana kwa maana mtakuwa munatafutwa kupindukia”
“Sawa”
Dokta William akandoka na moja kwa moja akafika nyumbani kwake ambapo alichukua nguo baadhi na kuelekea uwanja wa ndege
**************
“Jamani dokta ndio hivyo ameondoka”
Rahab alizungumza huku akiwatazama wezake
“Itakuwaje sasa?”
“Ina bidi madili tujitafutie sisi wenyewe” Anna alizungumza
“Ngoja kaka nilisikia kuwa kuna pesa ambazo zipo benki ya Taifa?”
“Ndio”
“Sasa mnaonaje,tukapiga ishu ya mwisho kila mtu akaamua kwenda kivyake kutafuta maisha kwa mbele” Halima alitoa wazo lililo wanyamazisha wezake kwa muda
“Jamani mimi kuishi bila nyinyi mwenzenu wala siwezi” Rahab alizungumza
“Sote kuishi mbali mbali hatuwezi”
“Sasa inakuwaje,kwa maana kwa sasa tunatafutwa na vijipesa tulivyo navyo hivi hata tukisema tuondoke nchini huko tuanapokwenda tutapata shida”
“Ni kweli hicho ulicho kizungumza Fetty,kama mimi natamani siku na mimi niitwe mama fulani.Niwe na mume wangu tuishi maisha salama tuu” Rahab alizungumza
“Sawa ,ni lini tunapiga hiyo ishu?”
“Tuanze kuitafuta ramani ya benki ambayo tutakwenda kupiga tukio”
“Wewe Agnes tunakutegemea wewe ndio fundi mitambo,ingia kwenye kompyuta hizo ututafutie ramani ya benki tukapige tukio”
Agnes akasimama na kukaa kwenye kompyuta zilizopo sebleni kwao na kuanza kufanya utundu wake kwenye mtandao,baada ya dakika kadhaa akawa ameipata tamani ya jengo zima la benki kuu ya Tanzania
“Kazi imeanza”
***********
Ulinzi ukazidi kuimarishwa katika viwanja vya ndege vilivyopo nchini Tanzania,mipaka na bandari zote zipo chini ya uangalizi mkali wa polisi ambao kila unaye muona unatambua ana hasira na majambazi yalio waua wenzao.Hakuna mtu hata mmoja ambaye alihitaji kutoka nje ya nchi pasipo kukaguliwa.
Simu ya dokta William inaita akiwa hatua chache kufika ulipo uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius K.Nyerere.Simu inatoka kwa mkuu wa polisi bwana Gudluck Nyangoi,mapigo ya moyo yanampasuka na kujikuta akiitazama simu kwa muda na anaamua kulisimamisha gari lake pembezoni mwa barabara na kuipokea simu kabla haijakata
“Habari yako dokta William”
“Salama tuu”
“Samahani dokta kwa kukusumbua,”
“Bila samahani”
“Tunakuhitaji hapa makao makao makuu”
“Saa ngapi?”
“Sasa hivi”
Simu ikakatwa na kuzidi kumuongezea wasiwasi Dokta William,akaitazama simu yake na kutaka kumpigia mkuu wa polisi bwana Gudluck Nyangoi ila akaacha.Akashuka kwenye gari na kutembea hatua kadhaa hadi ulipo uwanja wa ndege na kuzishuhudia gari nyingi zikiwa kwenye foleni na moja baada ya nyingine inakaguliwa.Akashusha pumzi nyingi huku asijue nini afanye,akarudi kwenye gari lake na kuingia.Nafsi moja inamuambia aende makao ya polisi huku nafsi nyingine ikimuambia asiende.
“Ngoja niende”
Akawasha gari lake na moja kwa moja akaelekea makao makuu ya polisi,akasimamisha gari lake kwenye maegesho na kushuka.Akatazama pande zote na kuona polisi wakiwa katika kazi ya kuimarisha ulinzi mkali.Baadhi ya polisi wakawa wanamtazama kwa macho makali.Akajikaza kiume na kuanza kupiga hatua za kawaidia na kungia ndani ya ofisi
“Samahani dada nahitaji kuonana na mkuu” alizungumza na askari mmoja wa kike
“Ingia kwenye lifti pandisha hadi gorofa ya tano,utakunja kulia utaona kibao kidogo juu ya mlango kimendika UKUMBI WA MKUTANO,Utamkuta hapa”
“Asante”
Dokta William akaingia kwenye lifti kabla haijafunga wakaingia askari wawilii wenye vyeo vingi kwenye mashati yao.
“Hawa majambazi,tukiwakamata mama yangu nitawanywa damu yao hadharani”
“Kweli bwana,yaani nimeacha msiba wa mwanangu ninakuja kwenye hicho kikao.Naapa haki ya Mungu nikimkamata mmoja wao lazima nivunje sheria za nchi”
“Hivi mwanao ni miongoni mwa askari walio kufa?”
“Ndio,tena ndio kwanza anamwaka wa pili kazini”
“Pole sana”
Dokta Williama aliendelea kuwasikiliza wakuu hawa wa polisi ambao vyeo vyao vinawatambulisha kama ma RPC kwenye mikoa yao.Lifti ikafunguka na wote wakatoka ndani ya lifti.Askari hao wakaendelea kwa mwendo wa kasi na kuingia kwenye ukumbi wa mikutano.Dokta William akajiweka sawa nguo zake na kuingia ndani ya ukumbi huu.Gafla macho yake yakatazamana na midomo ya bastola alizo elekezewa na wakuu wa polisi waliokaa kwenye viti vyao huku wakioneka kukasirishwa sana na uwepo wake
Itaendelea.......
No comments:
Post a Comment