Showing posts with label HADITHI. Show all posts
Showing posts with label HADITHI. Show all posts

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 7 & 8


Muandishi : Eddazaria g.Msulwa

Ilipoishia
Askari mmoja mwenye mwili mkubwa akamnyanyua Fetty na kumuweka begani mwake na safari ikaendelea.Fetty akayafumbua macho yake na kuona askari aliye mbebe ndio wa mwisho katika mstari wanao tembea,Kwa ustani wa hali ya juu Fetty akaichomeka mikono yeke katikati ya shingo ya askati,kwakutumia pigu akaanza kumnyonga askari huku akiwa amening'inia kwa nyuma.Mikoromo ya asakri ikawastua wenzake waliopo mbele kitendo cha wao kugeuka wakamkuta mwenzo ndio yupo kwenye hatua za mwisho huku macho yake akiwa ameyatoa njee

ENDELEA
Askari mmoja akataka kufyatua risasi ila mkuu wa masafara akamzuia,Fetty akaiachia shingo ya askari huku akiwa amehakikisha kwamba askari huyo yupo kwenye hali mbaya sana.Askari mmoja akampiga Fetty kwa kutumia kitako cha bunduki na kumfanya  Fetty ajikunje huku akitoa mguno mkali wa maumivu
“Kumbukeni kuwa,anahitajika akiwa hai”
Mkuu wao alizungumza
 
“Sawa mkuu,ila anahitaji kupata kibano kidogo”
Wakaendelea kumtazama mwenzo,ambaye hadi hapa alipo hali yake haipo vizuri sana.Vichwa vya askar vikaanza kupata moto kwani mwenzao ambaye alikuwa anakaribia kunyongwa ndio anaye fahamu njia ya bombo hilo japo imenyooka ila kuna sehemu mbele imegawanyika katika njia nne.Mwenzao anayejulikana kama inspector Julio hawezi kuendelea mbele na safari
 
“Mkuu kuna tatizo jengine limejitokea,Over”
“Nini tena inspector John? Over”
“Huyu binti alimkaba Inspector Julio,Over”
“Nyinyi mulikuwa wa hadi mwenzetu akabwe?”
Sauti ya mkuu wao ilizungumza huku akiwa anafoka,
“Mkuu alizimia,ndipo inspector Julio alipo amua kumbeba”
“Pumbavu zenu.Hakikisheni anatoka huyo binti,akiwa hai na Julio naye akiwa hai”
 
Fetty akatabasamu huku akiwatazama askari,kwani kwake kazi yake imeshaanza kuwa nyepesi kwani mtu ambaye anamuhofia ni huyu Inspector Julio,ambaye kwa mtazamo wake tu anaonekana ni mtu hatari sana katika swala zima la kutumia silaha.Askari mmoja akasimama mbele ya Fetty huku akiwa amempa mgongo akisaidiana na wezake katika kumpa huduma Inspector Julio,huku kazi yake ikiwa ni kuzifungua kamba za viatu vya Julio
 
Kwa umakini wa hali ya juu,Fetty akazichomoa funguo nyingi zinazo ning’inia kiunoni mwa askari huyo pasipo yeye mwenyewe kujua.Kwa bahati nzuri katika wingi wa funguo hizo zipatazo kumi na mbili,mbili ni funguo za pingu.

Macho ya Fetty yakawa na kazi ya kuwatazama askari jinsi wanavyo pata shida katika kumsaidi mwenzao ambaye hali yake inazidi kuwa mbaya.

Hakuna askari aliye kuwa na muda wa kumtazama Fetty kwani wanaamini kile kitako cha bunduki alicho pigwa kwenye tumbo,bado anaendelea kukisikilizia maumivu yake.Fetty akafanikiwa kufungua pingu za mikono pasipo askari yoyote kugundua.Akajaribisha kufungu mnyororo wa miguni ila akashindwa kwani hakuna funguo inayo ingiliana na kufuli alilo fungwa miguuni.
 
“Ja............ama..ani mmmim...i siwezi ku...pona.Ila,njia uki...oony......sha utaku...nja kulia...kwenye shimo lenye mlang....o wa....”
Inspector Julio alizungumza kwa shida na hakuweza kumalizia sentesi yake,mauti yakamchukua.

Inspector John akanyanyuka kwa hasira na kumfwata Fetty sehemu aliyo kaa.Kufumba na kufumbua akajikuta akirushwa juu kimo cha mbuzi  tena beberu na kutua chini kama mzigo.

Hii ni baada ya Fetty kuikutanisha miguu yake kwa pamoja,Kisha mikono yake aliikita chini na kujizungusha kwa kasi kubwa.Askari walio salia wakiwa wanamtizama mkuu wao.Fetty akajinyanyua kwa haraka na kumvaa askari aliye mchomolea funguo,akaichomoa bastola ya askari huyo ambaye alijitahii kumpiga ngumi  za mbavu Fetty
 
Bila ya huruma Fetty akafyatua risasi iliyo penya kwenye kichwa cha akari anayepambana naye na kumtuliza kimya.Askari watatu wa kiume wakazikoki kwa haraka bunduki zao na kuanza kuzifyatua risasi,ila kwa haraka sana kama tairi la gari liendalo kwa kasi sana,akawa na kazi ya kubiringika huku akiwafwata askari kwenye miguu yao mita chache kutoka alipo.

Akiwa anabiringika, bastola iliyopo mkononi mwake ikawa na kazi ya kufyatua risasi zilizo waangusha askari watatu chini na akabaki Inspector John na askari wa kike aliyetengenezwa kama yeye,na wakati wote tukio  la wezake kuangamizwa lilimpa kiwewe hadi akawa na kazi ya kuyaziba masikio yake akiziba asisikie milio ya risasi.Fetty akalala katikati ya miguu ya Inspector John huku mdomo bastola yake akiwa ameuweka kwenye sehemu za siri za Inspector John.Bunduki ya inspector John akawa ameilekezea kwenye kichwa cha Fetty ambaye macho yake yanatazamana na macho ya Inspector  John
“Shoot ni kushooti”
Fetty alizungumza huku akitabasama,na bastola yake akawa na kazi ya kuigusisha gusisha kwenye vitenesi vya Inspector John

 *************
Gari waliyopanda askari wapelelezi ikazidi kuongeza mwendo,huku kila mmoja akiwa na bastola yake mkononi.Kwa uelewa wao mkubwa katika kazi yao ya upelelezi wakagundua kuna gari tatu ambazo kwa Tanzania ni watu wachache sana ambao wanazimiliki kutokana na gharama zake kuwa ni kubwa sana.
“T upo tayari?”
“Ndio Y”
“l je?”
“Ndio Y”
“X je?”
“Ndio Y”
 
Askari hawa waliweza kupeana herufi za moja moja kurahisishana kuitana majina waliyo pewa kazini au na wazazi wao.

Y ndio kiongozi wao mkubwa ambaye ndio dereva wa gari hili ambalo kwa mtazamo wa bodi(umbo) lake la nje,inaonekana ni chakavu Ila injini yake na vifaa vingine ni vipya na inauwezo wa mwendo kasi 250 KM/H.

Kila mmoja akawa na kazi ya kuzitazama gari hizo zinazo wafwata kwa mwendo kama wanao kwenda nao
Rahab akiwa ametangulia gari lake mbele akawawashia wezake taa  huku akikanyaga breki za gari lake,akiwaashiria wapunguze mwendo.
 
“Baby’s munanisikia?” Rahab alizungumza kwa sauti ya kawaida
“Tunakupata”
“Wale jamaa,ninamashaka nao wamestukia dili”
“Kwa nini?” Ann aliuliza
“Kwa maana mwendo wao ni wamashaka mashaka”
“Haya sasa,Plan B yetu ni nini?” Halima aliuliza
“Kuwavamia bwana kwa pamoja” Agnes alishauri
“Tukiwavamia tutampataje Fetty?”
“Sasa ishu inakuwa vipi?” Rahab alizungumza
“Tuwafwateni tu” Anna alishauri
“Oya gari zetu,si zina map direction?”
“Ndio”
 
“Rahab wewe uliopo mbele tuambie,namba za gari la hao jamaa ni ngapi?”
“T234KSJ”
“Tuiingizeni hiyo namba kwenye hizi ramani zetu tutaweza kuiona kwa ishara hiyo gari kila inapo kwenda” Agnes alizungumza
“Sasa Ag wewe ndio mtaalamu wa hivi vitu sisi wezako wala hatujui”
“Ok,ngoja niingize”
 
Agnes akaiingiza namba ya gari na kwamsaada wa satellite aliweza kuiona gari ya wapelelezi kila inapo kwenda huku ikionekana kwa alama nyekundu.

Akawaelekeza wenzake jinsi ya kufanya na kila mmoja pembeni ya mskani wa gari lake kuna kioo kidogo kilicho unganishwa na sateliti na kazi yake ni kuweza kuonyesha ramani ya sehemu ambayo unahitaji kwenda au gari unayo taka kuifwata sehemu ilipo kikubwa ni kuweza kuzitambua namba za usajili wa gari hilo.

Wakaziendesha gari zao kwa mwendo wa kawaida na kuifanya gari ya wapelelezi kuzidi kutokomea,huku wakiwa hawana wasiwasi kuipoteza gari hiyo.

Wapelelezi wakaanza kupata matumaini baada ya gari tatu zinazo wafwata kuziacha nyuma sana.Gari ya wapelelezi ikafika Kimara Gas Station na wakashuka kwa haraka kwenye gari.Rahab na wezake wakalishuhudia gari la wapelelezi likiingia kwenye kituo cha gesi kilichopo Kimara.Wapelelezi wakaingia kwenye msitu wa miti ulipo hapo ambapo ndipo lilipo shimo ambalo wanatarajia kuwapokea Fetty na askari wengine
“Jamani tusishuke kwanza” Agnes alizungumza
“Kwa nini?”
 
“Hamuwezi kujua kama jamaa wamejificha wanatusubiria tushuke watushambulie”
“Hapo,umezungumza point”
Wakazisimamisha gari zao mbali kidogo na kilipo kituo cha gesi,wakisubiria kufanya kazi moja tu ya kuwashambulia askari hao pale watakapo mchukua Fetty

***************
Inspector Julio akaanza kutetemeka huku akimeza mafumba ya mate,kwani ni mwaka wa 25 sasa analitumikia jeshi la polisi,ila hajawahi kukutana na mwanake hatari kama Fetty.Kwa woga akajikuta akiminya kitufe cha kuziruhusu risasi kutoka,kwa bahari mbaya bunduki yake tayari imeisha risasi.
“Kwaheri”
 
Fetty alizungumza huku akiziruhusu risasi mbili kuchomoka kwenye bastola yake aina ya ‘browningu SFS’ na kuzichangua sehemu za siri za Inspector John,Fetty akasimama na kumtazama askari wa kike anaye fanana naye kuanzia mavazi hadi sura ya bandia aliyo valishwa.Fetty akataka kumuua  askari huyo ila akasitisha zoezi lake na kumnyanyua
“Nipe funguo nijifungue”
“Zip.....o kwa inspector John”
 
Fetty akamtazama kwa umakini askari,akachuchumaa kwa umakini huku bastola yake akiielekeza kwa askari huyo anaye itwa Rehema.Akaipapasa mifuko ya Inspector John na kuzitoa fungua nyingi.Akachagua funguo moja inayoweza kufungua kwenye mnyororo,kwa bahati nzuri akaipata.Akajifungua na kumuomba Afande Reheme kutangulia mbele huku akiwa ameshika tochi inayowasaidia kuona mbele.Wakafika kwenye njia nne tofauti,wakabaki wakiwa wamesimama wakiwa hawajui ni wapi waende
“Sema njia  ni ipi?”
“Sujui hata mimi”
 
Fetty akampiga kofi la shavu Afande Rehema huku akiwa amemnyooshea bastola
“Sema ni njia gani la sivyo nakumwaga ubongo?”
“Hii.....”
 
Afande Rehema alizungumza ili mradi aepukane na kifo cha kupigwa risasi.Japo amejitamkia ila njia aliyo ionyesha ndio sahihi.Wakaendelea na mwendo wao hadi wakafika sehemu yenye ngazi za chuma za kutokea nje.Fetty akamtanguliza afande Rehema japo amefungwa pingu za mikononi ila akajitahidi hivyo hivyo kuanza kupanda kwenda juu
 
*****************
Milio ya risasi waliyo isikia kupitia redio ya upepo,iliwachanganya sana wakuu wa polisi na kuwafanya waanze kubabaika na kuwapa taarifa wapelelezi kuwa kuna hali tete ambayo inaendelea chini walipo askari.

Mbaya zaidi kila wanapo jaribu kuwasiliana na wenzao hawakuweza kupata jibu la aina yoyote.Wapelelezi wakajiandaa kwa chochote kitakacho jitokeza kwenye shimo huku bastola zao wakiwa wameziandaa kwa umakini wa hali ya juu
Wakauona mfuniko wa shimo,ukifunguliwa na kichwa cha Afande Rehema kikatokeza,
“Musiniue”
 
Afande Rehema alizungumza huku akijitoa kwa kasi kwenye shimo.Fetty akajua kuna hali ya hatari ipo juu,akaishika bastola yake vizuri na kupandisha ngazi kwa hataka kabla hajajitokeza juu akakiona kichwa cha mpelelezi mmoja akichungulia,Mpelelezi akiwa anashangaa kati ya Rehema na Fetty yupi ni muhalifu kwani wanafanana,akastukia risasi ikipiga kwenye paji la uso wake na kumuangusha chini
 
Milio wa risasi ukawastua Rahab na wenzake,kwa haraka wakawasha magari yao na kuyasimamisha pembeni ya kituo cha gesi.Wakashuka kwa haraka kila mmoja banduki yake ikiwa mkononi.

Walinzi wa kitua cha gesi wakazidi kuchanganyikiwa kwani mlio huo wa risasi umesikika nyuma ya kituo na watu walio ingia kwenye  kituo chao hawaeleweki.Mlinzi mmoja akaikoki bunduki yake aina ya gobora,kitendo cha mlinzi kuishika bunduki yake,Anna alikiona vizuri,pasipo kuuliza ni nini mlinzi anataka kukifanya,akafyatua risasi iliyo muangusha mlinzi chini.Walinzi wengine wakalala chini kwa woga baada ya kumouona mwenzao akivuja damu nyingi
 
Wapelelezi wakabaki katika hali tata,huku kila mmoja akikataa kwenda kuchungulia kwenye shimo asije akakutwa na ktu kilicho mkuta X.

Wakiwa katika taharuki risasi zisizo na idadi zikatua mwilini mwao zikitokea nyuma yao na ukawa ndio mwisho wa maisha yao.Agnes akanza kupiga hatua za haraka akimfwata Afande Rehema aliye lala chini
“Fetty nyanyuka tuondole”
 
Fetty alianza kushua ngazi kurudi kwenye shimo ila baada ya kuisikia milio mingi ya bunduki.
“Fetty twende”
Agnes alizidi kumuita Afande Rehema baada ya kumuona anababaika.Kabla Fetty hajamalizi kushuka kwenye ngazi ya mwisho kuingia kwenye shimo akaisikia sauti ya Agnes.
“Agnes huyo sio Fetty ni polisi mimi nipo humu”
 
Fetty alizungumza huku akianza kupanda ngazi kwa haraka,Agnes akabaki akiwa ameshangaa,akamuona Fetty akichomoza kichwa kwenye shimo.Afande Rehema akajaribu kuiokota bastola ya askari mmoja aliye anguka chini.Risasi kama sita zikatua mgongoni mwake kutoka kwa Rahab.Fetty akamkimbilia Agnes na kumkumbatia
“Pole shosti”
“Asante”
 
Kabla hawajaondoka,mwanga mkali wa helcopar ya polisi iliotumwa kufika kwenye eneo hilo,ukaanza kuwamulika.Wakaanza kukimbia wakielekea mbele ya kituo walipo ziacha gari zao, kitendo cha Halima kujitokeza wakakutana na gari zipatazo kumi za polizi zikiwa zimetanda mbele ya kituo na askari wengi wakiwa na bunduki zao wakiwa wameelekezewa wao.
“WEKENI SILAHA ZENU CHINI”
“Shitii”
 
Wote watano wakabaki wakiwatazama askari huku helcopar ya polisi ikiwa inawamulika kwa mwanga mkali mweupe ambao umelifanya eneo walilo simama wao kuwa kama mchana na endepo watafanya kitu chochote cha kijinga,askari wenye bunduki wapatao thelasini wenye bunduki watazifyatua risasi zao pasipo kuwa na huruma


SHE IS MY WIFE(NI MKE WANGU)……8


“Nini tunafanya”
Rahab aliwauliza wenzake,huku taratibu mikono yake akiwa anainyanyua juu.Kila kitu ambacho kinaendelea katika eneo la kituo cha gesi,Dokta William anakifwatilia akiwa amelisimamisha gari lake mbali kidogo na eneo walilopo askari.

Kwa haraka alifungua nyuma ya gari lake kwenye buti na kutoa bunduki yake yenye uwezo wa kupiga risasi kwa masafa marefu inayoitwa ‘THE BOR SNIPER’ yenye uzito wa kilo sita na urefu wa milimita 1,038 sawa sawa na nchi 40.9 za urefu.

Akaiweka chini pembeni ya gari lake,kisha akalala na kufungua kifuniko cha lenzi inayoweza kuvuta karibu,Uzuri wa hii bunduki yake unaweza kuona muda wowote hata kama kuna giza ila kwa kutumia mwanga wa kijani uliopo kwenye lenzi yake unaweza kuona vizuri bila shida.

Akaifunga kiwambo cha kuzuia sauti.Alipo hakikisha kila kitu kipo sawa,akwakavuta kwa karibu Rahab na wezake na kuwaona wamenyoosha mikono yao juu .Pembeni na walipo jipanga  askari kuna tanki kubwa la gesi.Akapiga ishara ya msalaba kisha akafyatua risasi moja iliyoingia kwenye tanki la gesi.

Ndani ya sekunde mlipUko mkubwa wa gesi ukawarusha mbali askari karibia wote,mbaya mlipuko huo ukaendelezwa na magari yao yanayo tumia mafuta ya petrol na desel
Haikuwa kwa askari tu kurushwa,ila hata Rahab na wezake wakarushwa na kurudishwa nyuma walipo tokea.Halima akawa wa kwanza kunyanyuka,
“Jamani tuondokeni”
 
Alizungumza akiwahimiza weNzake,wakanyanyuka kwa haraka na kuanza kutokomea kwenye pori.Mitungi iliyo chimbiwa chini ya ardhi ikaanza kupata moto,mwisho wa siku ikaanza kulipuka mmoja baada ya mwIngine na kuzidi kusababisha vifo vya askari.Rubani anaye iendesha helcoptar ya polisi akachanganyikiwa sana,na jinsi moto unavyo waka.

Akaipeleka juu kidogo Helcoptar yake.Dokta William akaona kitendo cha rubani wa Helcoptar kuinyanyua juu.Akamvuta karibu rubani na bila ya huruma akamtandika risasi ya kifua na kumfanya aachie kila kitu alicho kishika na helcoptar ikaanza kurudi chini kwa kasi ya ajabu na kuingia kwenye moto mwingi wa gesi na kuzidi kuongeza mlipuko wa eneo la kituo
 
Dokta William akainyanyua bunduki yake kwa haraka na kuirudisha sehemu alipo itoa kwenye gari kisha akaingia ndani ya gari na kuondoka eneo alilopo,huku akilini mwake akiwa amejawa na mawazo mengi sana kwani kitendo ambacho amekifanya kwanza ni kinyume na sheria za nchi ya Tanzania pamoja na hata nchi yake ya Israel na endapo tukio hili litajulikana kama yeye ndio mtendaji mkuu atahukumiwa kifungo cha maisha jela au kunyongwa mbele ya halaiki ya watu.Kingine kinacho muumiza kichwa ni Fetty na wezake ambao aliwashuhudia wakirushwa na mlipoko wa tanki la gesi
 
Akatoa simu yake ambayo anawasiliana na Rahab na wezake.Akawapigia na kwabahati nzuri akazisikia sauti zao
“Mupo wapi?”
“Tupo kwenye haka kapori kalichopo nyuma ya kituo,tunakaribia kufika kwenye makazi ya watu”
“Sasa nyinyi,katokeeni katika barabara kuu maeneo ya Mbezi”
“Sawa”
 
Rahab na wezake wakabadilisha muelekeo na kuanza kukimbia kuelekea walipo elekezwa na Doktar Willian,ndani ya robo saa wakawa ameshafika Mbezi.Fetty kutokana amevaa nguo za polisi,ikawa ni nafasi nzuri kujitokeza barabarani kutazama ni wapi lilipo gari la Dokta William.
 
Dokta Willim akamuona Fetty  na kumtambua mara moja,akawasha gari lake kwani alikuwa amelisimamisha pembezoni mwa bararaba.Akafika sehemu walipo Fetty na wezake na wote kwa haraka wakaingia ndani ya gari ya dokta William aina ya Ford na kuondoka kwa mwendo wa kasi

***********
Tangu mwaka 1961 nchi ya Tanzania ilipo pata uhuru hapakuwahi kutokea tukio la kinyama lililo husisha mauaji ya askari zaidi ya thelathini kwa wakati mmoja tena wakiwa wanapambana na jeshi la polisi,isitoshe kuna baadhi ya wanachi waliokuwa katika kituo hicho nao pia wamefariki dunia.Tukio hili likaingizwa katika matukio ya kigaidi.Vilio vingi vilitanda kwenye nyumba za askari ambao wamefariki,hivyo hivyo kwa wananchi walio fariki hali ilikuwa ni moja ya kuomboleza vilio
 
Magazeti ya serikali na udaku yakatawaliwa na taarifa ya magaidi kulitingisha jeshi la polisi.Moja ya magazeti linalo itwa Story Za Eddy likatawaliwa na kichwa cha habari kilicho wakera viongozi wengi serikalini
 
(UZEMBE  WAUA ASKARI 30)
“Nitafutieni muandishi wa hili gazeti”
Mkuu wa polisi alizungumza kwa jazba,huku akiwatazama askari wake watatu walio simama mbele yake.Akaendelea kulipitia gazeti moja baada ya jingine kuangalia habari zilizo andikwa kwenye magazeti ya nchi hii.Akakutana na habari nyingine iliyo andikwa
(CHEZEA MAJAMBAWAZI WEWE,WAMEUNYUTI WENYEWE) Huku pembeni kukiwa na picha yake ya kikatuni ikitazama jinsi makatuni askari wakilipuliwa na moto wa gesi.Bwana Gudluck Nyangoi IGP wa polisi ikambidi kufumba macho yake na kuachana na habari ya kuyasoma magazeti ambayo yanazidi kuipandisha hasira yake.Akaitisha kikao cha wakuu wa jeshi la polisi nchi nzima na akawapa masaa manne wote wawe wamefika makao makuu ya polisi,hakujali wengine umbali wa mikoa yao ila tamko lake akaitaji lifanyiwe kazi mara moja
                                                                                           ************
Katika siku walizo amka na furaha ni hii ya leo,Agnes akaingia jikoni na kuwaandalia wezake kifungua kinywa cha nguvu na wote wakakutana katika meza ya chakula,pamoja na dokta William
“Fetty hongera” Agnes alizungumza
“Na nini?”
 
“Nimekukubali sana,wewe ni noma”
“Ahaa mbona kawaida”
“Ahaa,hivi ulisema wale askari uliwafanya nini ndani ya mtaro?”
“Wazembe wale,sema wamekufa ila wangekuwa hawajafa ningewashauri warudi tena mafunzoni”
Wakati Fetty na Agnes wanazungumza,dokta William akawa na kazi ya kupitia habari zinazo endelea kwenye mitandao ya kijami,akianzia na Facebook
 
“Jamani mambo sio mazuri kabisa”
“Kwa nini?” Halima aliuliza
“Huko nje mnatafutwa kama nini”
“Wametujua?”
“Hakuna picha hata moja inayo waonyesha sura zenu ila ni habari tuu”
“Doktar picha ya Fetty je?”
“Huyu picha yeke niliiona tuu,ila haijaandikwa vibaya”
“Imeandikwaje?” Fetty aliuliza
“Iliandikwa anatafutwa”
Wakabaki wakiwa wanacheka na kumfanya Dokta William kushangaa
 
“Mnacheka nini......!!?”
“Si hivyo unavyo sema kuwa haijaandikwa vibaya sana...ila anatafutwa,Doktar sasa hapo unadhani hayo maneno ni mazuri?” Rahab aliuliza huku akicheka
“Sawa tusikilizane,mimi nitaondoka mara moja kwenda Israel nyumbani.Hii ishu ikipita nitarudi”
“Dokta,pesa yetu?”
“Hiyo pesa yenu mimi nitawaingizia kila mmoja kwenye akaunti yake”
 
“Hapa sote unapo tuona hakuna hata mmoja ambaye ana akaunti benki,sasa hatujajua kama kunauwezekano wa sisi kuipata hiyo pesa”
 Anna alizungumza huku sura ya furaha ikiwa imepotea usoni mwake
“Nimewaelewa,kikubwa ni mawasiliano kati yangu mimi na nyinyi kwani hata nikiwa nje ya nchi nitaendelea kuwasiliana na nyinyi”
“Dokta mbona kama sijakuelewea? Ina maana pesa yetu ndio hakuna?”
 
Anna aliuliza huku akijiweka sawa kwenye kiti alicho kalia
“Pesa yenu ipo.Ila kwa kiasi cha pesa mbacho mnanidai chote kipo katika benki ya serikali ambayo kwa sasa akaunti zote zimefungwa kutokana na tukio la jana”
“Wewe kama wewe una kiasi gani kwenye hiyo benki?”
“Milioni mia sita”
“Mmmmm,wataifungua lini?”
“Hata mimi mwenyewe sijui”
“Wewe umejuaje?”
“Kuna mtu alinitumia meseji asubuhi”
“Ni nani?”
 
“Ni kiongozi wa juu,kwenye hiyo benki”
Swala la Dokta William kuto kuwa na pesa ya kumalizia kuwalipa Agnes na wenzake likaanza kumsumbua akili mmoja baada ya mwengine.Anna akanyanyuka na kuingia chumbani kwake na kurudi na bastola na kukaa kwenye kiti alicho kuwa amekikalia
 
“Dokta,tunakuamini tena sana.Ila mimi kwa hili bado hujanishawishi hata kidogo.Kwanza kumbuka sisi ni wasichana wadogo sana ambao kama tungeendelea kufanya kazi yetu ya kuiuza miili yetu tusinge tafutwa kwa mabaya kama hivi sasa.Sasa ninakupauchague vituu viwili,Uzungumze ni lini unatupa pesa yetu au uzungumze na huyu mjamaa hapa”
 
Anna alizungumza huku bastola akiiweka mezani,wenzake wote wakamtazama kisha wakamgeukia Dokta William
“Anna mimi nipeni masaa kadhaa nitawaletea pesa yenu”
“Huyu muongoo” Halima alidakia
“Siwadanganyi jamani”
 
“Mbona saa zote ulikuwa unajikenua kenua mbele yetu tuu?”
“Nilikuwa ninawapima kama mnaniamini au laa” Doktar William alizungumza kwa kujiamini
“Kuna vitu vya kudanganyana na vingine si vyakudanyanyana.Pesa ndio kila kitu bwana”
 
Fetty alizungumza huku akimtazama Dokta William kwa macho makali sana yasiyo na utani hata kidogo.Dokta William akasimama na kutoka nje ya handaki huku nyuma akiwa ameongozana na Fetty.Wakafika chini ya mti mmoja uliopo karibu sana na handaki lao,Dokta William akafukua kidogo na kutoa mfuko wa rambo ulio jaa pesa nyingi za kigeni.
“Duuu kumbe tunaishi na benki hapa ila hatujui chochote kinacho endelea”
 
“Si kutokana na nyinyi sio wachunguzi,mngejuaje”
Dokta Willia akampa mfuko Fetty na wote wakarudi ndani.Dokta William akawalipa kila mmoja kiasi chake anacho hitaji kulipwa.
 
“Jamani ninaondoka Tanzania leo.Mtajua ni nini cha ufanya na hizo pesa.Ila kwa ushauri sasa hivi ninawaomba msitembee tembee sana kwa maana mtakuwa munatafutwa kupindukia”
“Sawa”
Dokta William akandoka na moja kwa moja akafika nyumbani kwake ambapo alichukua nguo baadhi na kuelekea uwanja wa ndege

 
   **************
“Jamani dokta ndio hivyo ameondoka”
Rahab alizungumza huku akiwatazama wezake
“Itakuwaje sasa?”
“Ina bidi madili tujitafutie sisi wenyewe” Anna alizungumza
“Ngoja kaka nilisikia kuwa kuna pesa ambazo zipo benki ya Taifa?”
“Ndio”
 
“Sasa mnaonaje,tukapiga ishu ya mwisho kila mtu akaamua kwenda kivyake kutafuta maisha kwa mbele” Halima alitoa wazo lililo wanyamazisha wezake kwa muda
“Jamani mimi kuishi bila nyinyi mwenzenu wala siwezi” Rahab alizungumza
 
“Sote kuishi mbali mbali hatuwezi”
“Sasa inakuwaje,kwa maana kwa sasa tunatafutwa na vijipesa tulivyo navyo hivi hata tukisema tuondoke nchini huko tuanapokwenda tutapata shida”
 
“Ni kweli hicho ulicho kizungumza Fetty,kama mimi natamani siku na mimi niitwe mama fulani.Niwe na mume wangu tuishi maisha salama tuu” Rahab alizungumza
“Sawa ,ni lini tunapiga hiyo ishu?”
“Tuanze kuitafuta ramani ya benki ambayo tutakwenda kupiga tukio”
 
“Wewe Agnes tunakutegemea wewe ndio fundi mitambo,ingia kwenye kompyuta hizo ututafutie ramani ya benki tukapige tukio”
 
Agnes akasimama na kukaa kwenye kompyuta zilizopo sebleni kwao na kuanza kufanya utundu wake kwenye mtandao,baada ya dakika kadhaa akawa ameipata tamani ya jengo zima la benki kuu ya Tanzania
“Kazi imeanza”
 
 ***********
Ulinzi ukazidi kuimarishwa katika viwanja vya ndege vilivyopo nchini Tanzania,mipaka na bandari zote zipo chini ya uangalizi mkali wa polisi ambao kila unaye muona unatambua ana hasira na majambazi yalio waua wenzao.Hakuna mtu  hata mmoja ambaye alihitaji kutoka nje ya nchi pasipo kukaguliwa.
 
Simu ya dokta William inaita akiwa hatua chache kufika ulipo uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius K.Nyerere.Simu inatoka kwa mkuu wa polisi bwana Gudluck Nyangoi,mapigo ya moyo yanampasuka na kujikuta akiitazama simu kwa muda na anaamua kulisimamisha gari lake pembezoni mwa barabara na kuipokea simu kabla haijakata
“Habari yako dokta William”
“Salama tuu”
“Samahani dokta kwa kukusumbua,”
“Bila samahani”
“Tunakuhitaji hapa makao makao makuu”
“Saa ngapi?”
“Sasa hivi”
 
Simu ikakatwa na kuzidi kumuongezea wasiwasi Dokta William,akaitazama simu yake na kutaka kumpigia mkuu wa polisi bwana Gudluck Nyangoi ila akaacha.Akashuka kwenye gari na kutembea hatua kadhaa hadi ulipo uwanja wa ndege na kuzishuhudia gari nyingi zikiwa kwenye foleni na moja baada ya nyingine inakaguliwa.Akashusha pumzi nyingi huku asijue nini afanye,akarudi kwenye gari lake na kuingia.Nafsi moja inamuambia aende makao ya polisi huku nafsi nyingine ikimuambia asiende.
“Ngoja niende”
 
Akawasha gari lake na moja kwa moja akaelekea makao makuu ya polisi,akasimamisha gari lake kwenye maegesho na kushuka.Akatazama pande zote na kuona polisi wakiwa katika kazi ya kuimarisha ulinzi mkali.Baadhi ya polisi wakawa wanamtazama kwa macho makali.Akajikaza kiume na kuanza kupiga hatua za kawaidia na kungia  ndani ya ofisi
 
“Samahani dada nahitaji kuonana na mkuu” alizungumza na askari mmoja wa kike
“Ingia kwenye lifti pandisha hadi gorofa ya tano,utakunja kulia utaona kibao kidogo juu ya mlango kimendika UKUMBI WA MKUTANO,Utamkuta hapa”
 
“Asante”
Dokta William akaingia kwenye lifti kabla haijafunga wakaingia askari wawilii wenye vyeo vingi kwenye mashati yao.
“Hawa majambazi,tukiwakamata mama yangu nitawanywa damu yao hadharani”
 
“Kweli bwana,yaani nimeacha msiba wa mwanangu ninakuja kwenye hicho kikao.Naapa haki ya Mungu nikimkamata mmoja wao lazima nivunje sheria za nchi”
“Hivi mwanao ni miongoni mwa askari  walio kufa?”
“Ndio,tena ndio kwanza anamwaka wa pili kazini”
“Pole sana”
 
Dokta Williama aliendelea kuwasikiliza wakuu hawa wa polisi ambao vyeo vyao vinawatambulisha kama ma RPC kwenye mikoa yao.Lifti ikafunguka na wote wakatoka ndani ya lifti.Askari hao wakaendelea kwa mwendo wa kasi na kuingia kwenye ukumbi wa mikutano.Dokta William akajiweka sawa nguo zake na kuingia ndani ya ukumbi huu.Gafla macho yake yakatazamana na midomo ya bastola alizo elekezewa na wakuu wa polisi waliokaa kwenye viti vyao huku wakioneka kukasirishwa sana na uwepo wake

Itaendelea.......
Read More

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 5 & 6



Muandishi : Eddazaria g.Msulwa

Ilipoishia....
.....Rahabu akapunguza mwendo wa pikipiki na agnes akaruka na kukimbilia njia aliyo kwenda kibopa,rahab akapita njia aliyo kwenda muntar.Muntar akajibanza kwenye mti na kuokota gongo kubwa na kulishika kwa umakini.Gafla rahab akajikuta akiichia pikipiki na kuanguka chini hii ni baada ya kupigwa gongo la kifua na muntar akajitokeza mbele yake huku akiwa na gongo mkononi....

Edndelea....
.....Rahab akanyanyuka haraka,akamtazama muntar ambaye alianza kucheka kwa dharau akimtazama rahab kuanzia juu hadi chini.Muntar akarusha gongo kwa kutumia nguvu nyingi,rahab akalikwepa na kurusha teke lililotua shingoni mwa muntar na akaayumba,kabla hajajiweka sawa rahab akampiga muntar ngumi kadhaa za kifua na kuzidi kumfanya muntar kuyumba mithili ya mtu aliyelewa kwa pombe za kienyeji.(mataputapu).

Muntar akajaribu kurusha ngumi ila rahab akafanya maamuzi ya haraka katika kuudaka mkono wake wa kulia,akajigeuza na kwakutumia bega lake akauvunja mkono wa muntar.Kilio cha maumivu makali kikamkumba muntar.Pasipo kuwa na huruma rahab akampiga mtama muntar na kumfanya aliachie gongo alilolishika.Rahab akaliokota gongo na kuanza kumpiga muntar gongo la kichwa hadi damu nyingi zikaanza kutoka nje kwa kasi kama bomba la maji lililo pasuka sehemu ndogo.

 Kibopa akafunga breki za miguu yake baada ya kukutana uso kwa uso na agnes.Kibopa akameza funda kubwa la mate huku mwili wake ukimtetemeka kiasi kwamba akabaki akiwa hajajua nini la kufanya.Agnes akaachia tabasamu pana baada ya kuiona surulia ya kibopa ikianza kuchora ramani ya kutota kwa mikojo aliyo shindwa kuizuia.
“ni....Iisssa...Mehe”

Kibopa alizungumza kwa kigugumizi kikali,agnes akapiga hatua hadi alipo simama kibopa na akamtisha kama anampiga ngumi ya uso,kwa woga uliokithiri ukammdondosha kibopa chini kama mzigo na akaanza kulia kama mtoto mdogo
“khaa wewe si jambazi,mbona unalia sasa?”

“mimi ni nilikuwa kibaraka waoo tuu,sioooo jambaazzziiii” kibopa alizungumza kwa kuyavuta vuta maneno kama amemeza fumba la uji wa moto na anashindwa kuumeza.Agnes akamtazama kwa huruma kipopa ambaye taratibu alianza kupiga magoti akimuomba msamaha.Agnes akampiga kofi la shavu kipopa na kumuamuru kusimama
“wenzenu wapo wapi?”
“wameshakufaa”
“changanya mbaliga zako,kabla sijabadilika”
“eheee....!!”

Agnes akampiga kibopa teke la makalio huku akimsindikiza na kofi la mgongoni na kumfanya kibopa aanze kukimbia kwa kasi kubwa.Agnes akabaki kucheka kwani hakutarajia kama ataweza kukutana na mwanaume muoga kama kibopa.

                                          *****

Jackson luther mpelelezi anaye sifika kwa kazi yake nzuri akaanza kupandisha ngazi kwenda juu alipo anna kwa lengo la kumtia nguvuni kwa kosa la mauaji.Anna akaanza kukimbia akipandisha ngazi kwa kasi hadi akafika alipo waacha wezake.
“tuondokeni kimenuka”

Wakasaidiana kumkokota fety ambaye amechoka sana kwa kazi ya kupambana na karim pamoja na shamsa.Wakaingia ndani ya lifti na kushuka hadi gorofa ya kwanza,jackson akaitoa bastola yeka na kuwa makini zaidi,taratibu akaanza kuuunguza mwili wa muntar na kuhakikisha kwamba uhai wa mwili huo umesharudi kwa Mungu baba.

Kitu ambacho kinamchanganya jackson luther ni juu ya nani aliyeweza kumuua karim kwani ni miongoni mwa majambazi ambao alijaribu kuwafuatilia kwa kipindi kirefu pasipo kupata mafanikio ya aina yoyote katika kazi ya uchunguzi wake.Akapandisha hadi gorofa ya tano alipomuona anna akimalizikia na akakuta korido ikiwa haina mtu hata mmoja.

Akachunguza sehemu yote na kumkuta mtu aliye anguka chini akiugulia maumivu na mlango wa kuingilia chumbani kwake ukiwa upo wazi, akamsogelea na kumpa mkono na kumuinua kutoka alipokuwa.

“umepatwa na nini?”
“kuna wadada bwana hapa,walikuwa wakipigana na kuniangusha”
“umeumia?”
“ndio nimepiga kiuno chini.”
“wameelekea wapi?”
“hata sijui wametoka vipi humu ndani kwangu”
“sawa”

Anna,fetty na halima wakaingia kwenye jiko kuu la kupikia vyakula kwa kutumia mlango wa chini wakashuka kwenye ngazi na kutokezea upande wenye maswimcming pool katika hotel,wakawatizama watu waliomo ndani ya hotel na kuona hakuna anayewatilia mashaka kwa mwendo wa umakini wakaanza kuelekea kwenye sehemu lilipo gati la kuingilia hotelini.Kabla ya kutoka nje ya geti walinzi wakawasimamisha,kwa jicho la kuiba fetty kwa kupitia kioo cha dirisha la kijumba cha walinzi akaona video inayomuonyesha akipambana na shamsa kupitia kwenye tv ndogo iliyopo kwenye kijumba cha walinzi

                                            *****

Rahab alipo hakikisha amekipasua kichwa cha muntar kwa kukipiga magongo,akatafuta sehemu chini ya mti na kukaa huku akiyasikilizia maumivu makali ya kifua aliyopigwa kutokana na kupigwa gongo.Agnes akaanza kumtafta rahab na kwabahati nzuri akamkuta akiwa amekaa chini ya mti
“shost umempata huyo mjinga?”
“ndio”
“umemuua?”

“hapana,nimemuachia aende zake kwa maana nimeona hana hatia.”
“mpumbavu kweli wewe,unadhani atashindwa kwenda kujipanga na kuja kutudhuru?”
“atatupatia wapi?”
“wewe mjinga nini?” rahab alizungumza kwa hasira kubwa.
“mpumbavu mwenyewe unadhani kila mtu ni wakumuua,mtu gani huna roho ya huruma”
“ila kumbuka ni nini tulichoamua”

“si tumesha kamilisha kama ni muntar kufa umesha muua,sasa kwa nini damu nyingine zije juu yetu pasipo kuwa na sababu ya msigi”
“katika siku ambazo ag nikuona kuwa wewe ni mjinga,limbukeni,poyoyo ni leo”
Rahab aliendelea kuzungumza kwa dharau iliyo changanyikana na hasira kali
“mimi poyoyo si ndio?” agnes alizungumza kwa hasira
“ndio wewe poyoyo”

Agnes akamsukuma rahab na kumfanya rahab kunyanyuka kama mbogo mkali aliye punyuliwa na risasi,akamrukia agnes kwa kutumia teke lake na kumuangusha agnes chini.Agnes akampiga mtama rahab na kumuangusha chini,wakaanza kushikana nywele zao na kuanza kuminyana huku wakipiga piga kelele.

“rahab nitakuua”
“niue kama unaweza”
Agnes akamuachia rahab nywele na akasimama.Rahab akamtazama kwa jicho kali agnes na akachia msunyo mkali
“rahab hebu tuache maswala ya kitoto,sisi ni marafiki kitu kinacho tufanya haswa tugombane ni nini?”

“wewe si ndio mzembe,unafanya vitu vya kijinga”
“sio vitu vya kijinga,kuna mambo yakufanya na mengine sio ya kufanya.Hivi rohoni mwako unaroho gani hadi umuue mtu asiye ha hatia”
“agnes hebu mtazame yule mjinga alivyokuwa akitumiminia risasi,unadhani angetuua ingekuwaje?”

‘ila haijawa,cha msingi tufanya mpango turudi tunapo ishi”
Agnes akampa mkono rahab na kumnyanyua,wakauvuta mwili wa muntar na kuuficha kwenye kichaka.Agnes akaikagua pikipiki na kukuta haijaharibika sana zaidi ya kuvunjika kioo cha pembeni cha upande wa kushoto.Agnes akaiwasha pikipika na rahab akapanda kwa nyuma na kuondoka porini na kutokea barabara kuu iendeyo mikoani na safairi ikaendelea
                                                                                                                                                                                                                    
                                          *****
 
“hamruhusiwi kutoka humu ndani”
Mlinzi mmoja alizungumza huku akiwazuia anna,fetty na halima wasitoke,wakaongezeka walinzi wawili wakasimama mbele yao huku mikononi wakiwa na bunduki zao
“kwa nini,huturuhusiwi kutoka?” anna aliwahoji
“kwa sababu maalumu.Tunawasubir......”

Fetty hakumuacha mlinzi kumaliza sentensi yake,akamtwanga kichwa kilichomfanya mlinzi kuishika pua yake iliyoanza kuvuja damu.Kwa shambulio hilo walinzi wengine wakawa wameduwaa kumuona mkubwa wao akivujwa na damu.Anna na halimwa kwa utaalamu mkubwa wakawapokonya walinzi bunduki zao,
“polisi”

Sauti ya jackson luther ikasikika kwa nyuma ikiwaamrisha fetty na wezake kutulia kama walivyo huku akiwa ameishika bastola yake kwa umakini.Anna akageuka kwa haraka na kufyatua risasi moja iliyompiga jackson luther kwenye paja la mguu wa kushoto na kumfanya aanguke na bastola ikaangukia mbali na alipo.

Mlinzi mmoja akajaribu kumrukia halima ila risasi ya bunduki  iliyotua tumboni mwake ikamfanya arudishwe nyuma na kuanguka kama mzigo wa kuni.Macho ya jackson luther yakatazama na macho ya anna akajaribu kuunyoosha mkono wake kwenye bastola yeka ila akastukia risasi nyingine ikitua kwenye mkono wake na kumfanya jackson luther kutoa ukulele mkali wa maumivu.
Fetty akamvuta kwa haraka askari aliye mpiga kichwa na kumchomolea bastola iliyopo kiunoni mwake.
“waamrishe wezako kutufungulia geti”

Fetty alizungumza huku bastola akiwa ameielekezea kwenye kichwa cha mkuu askari wa hoteli,akawaamrisha wezake waliopo kibandani na wakalifungua geti linaloendeshwa kwa umeme.Wa kwanza kutoka akawa ni halima,akawaamuru watu waliomo ndani ya gari la kifahari aina ya range rover linalo ingia kwenye hoteli.

Vijana wawili wa kiarabu waliomo ndani ya gari wakashuka na kulala chini.Halima akaingia na kuwasubiria fetty na anna ambao nao wakingia kwa na kuondoka hotelini wa kasi,gari mbili za polisi zilizokuwa zinafika hotelini baada ya kupigiwa simu na wasamaria wema zikaanza kuwafukuzia kwa nyuma.

Wakiwa ndani ya gari fetty akatoa simu na kumpigia dokta willim huku akizitazama kwa nyuma gari za polisi zinazo kuja kwa kasi
“vipi kazi imekwenda vizuri?”
“ndio ila kuna tatizo limetokea”
“tatizo gani?”
“tumezidiwa ng............”

Fetty hakumalizia sentesi yake na akajikuta akijigonga kichwa kwenye kioo na gari yao ambayo ilikumbwa na lori la kubebea mchanga ambalo halima ajiribu kulipita kwa kupitia upande wa kushoto kinyume na sheria za barabara,gari ikaanza kuserereka ndani ya mtaro kwa kasi ya ajabu kwa ubavu wa kustoto aliopo fetty na kugonga kwenye karavati la barabara na kusababisha gari kuminyika minyika vibaya sana  na gari moja ya polisi ikamshinda dereva wake kuwahi kufunga breki na ikajikuta ikiligonga lori kwa nyuma na kupenya chini ya uvungu wa lori na kusababisha askari wote sita waliopo ndani ya gari,miili yao kugawanyishwa vipande viwili

                  She is my wife(ni mke wangu)……6

Ajali hii mbaya ikaanza kuwakusanya wananchi waliopo jirani na eneo la ajali,kila mmoja akijaribu kujua ni nini kinacho endelea.Halima akawa wa kwanza kujichomoa ndani ya gari,sehemu kidogo ya paji lake la uso ikiwa imechanika kidogo na kumwaga damu.Anna akajiminya minya kwenye siti aliyoikalia na kufanikiwa kutoka nje ya gari.Ila ikawa ni tofauti kwa fetty ambaye amepoteza fahamu.Kabla hawajaanza kumsaidia kumtoa fetty wakashuhudia gari la polisi likisimama sehemu walipo pata ajali wezao na askari wote wakaruka ndani ya gari lao wakiwa na bunduki mikononi
“anna tuondoke”
“na fetty je?”
“twende nimekuambia tutarudi kumchukua”

Halima hakuwa na haja ya kubaki eneo la tukioa kwa maana tayari askari walishaanza kuwasaka.Wakajichanganya katikati ya askari na kuanza kukimbia kwa wakikatiza mitaani.Wakafanikiwa kufika nje ya baa moja na kumkuta mtu mmoja akishuka kwenye gari lake.Kabla hajaufunga mlango wa gari lake wakamvamia na kumuamrisha atoe funguo za gari lake
“nyinyi kama kina na......”

Jamaa hakumalizia sentesi yake akapigwa kigoti ya tumbo na anna akabaki akiwa amejishika tumbo,akazitoa funguo za gari lake aina ya ‘premore’.Anna akazichukua funguo za gari na wote wakaingia na kuondoka na kumuacha jamaa akipiga kelele za mwizi

“gari yangu ya mkopo ina wiki ya pili ile” jamaa alizungumza huku akimwagikwa na machozi,mbaya zaidi hakuna mtu aliyepo katika eneo la baa aliyeweza kutoa msaada wowote kwao

                                                  *****

Askari  wakamchomoa fetty ndani ya gari na kumfunga pingu japo ajitambui kwa lolote.Wakamuingiza ndani ya gari lao na kumpeleka hospitali ya taifa muimbili huku akiwa chini ya ulinzi mkali.Wakamkabidhi kwa madaktari ambao pasipo kupoteza muda wakaanza kummuhudumia

“tunaomba mumfungue pingu za mikononi”
Daktari mmoja alizungumza na askari mmoja akatii ombi la daktari.Matibabu yakaanza kufanyika kwa haraka.Wakagundua fetty amepeta mstuko tuu uliomfanya kuweza kupoteza fahamu.

                                           ****

Pikipiki waliyopanda rahab na agnes haikuwa na mafuta ya kutosha,ikawazimikia maeneo ya saruji na kwa bahati nzuri wakapata lori linaloelekea dar es salaam ambalo linasafirisha mifuko ya saruji(cement).Wakafika eneo la kuingilia kwenye msitu kulipo na handaki lao.

Wakamuomba dereva kuwashusha,wakawashukuru na kuanza kutembea kwa miguu kuelekea ndani ya msitu, hii ni baada ya gari walilolipanda kuondoka.Japo kuna giza ila wakajiamini sana,wakiwa njiani gafla wakaona taa za gari zikija kwa nyuma yao.Gari ikasimama pembeni yao,anna akafungua kioo cha gari 

“vipi nyinyi?”
“safi”
“ingieni ndani ya gari”
Rahab na agnes wakaingia ndani ya gari na safari ikaendelea.
“jamani fetty yupo wapi?” agnes aliuliza
“wee acha tuu,tumepata ajali mbaya”
“amekufa......!!?” rahab aliuliza kwa mshangao
“hajafa ila alipoteza fahamu na isitoshe,askari walikuwa wanatufukuza
“sasa itakuwaje jamani?”
“mmmm hapa nilipo mimi nimechanganyikiwa”

Wakafika kwenye handaki na kitu cha kwanza kukifanya ni kufungua tv yao kuangalia kama kuna taarifa yoyote inayo endelea.Hawakukuta chohote kinachoendelea
“hivi vyombo vya abari vya ajabu kama nini?”
Rahab alizungumza huku akiachia msunyo mkali na kuingia chumbani kwake.Agens akaanza kuwahudumia wezake majeraha waliyo yapata

“jamani tunafanyaje?”
“inabidi tujue ni wapi alipo fetty,ikiwezekana tukamuokoe sisi wenyewe pasipo msaada wa mtu yoyote”
Anna ilo ulilolizungumza ni kweli,ila ni wapi tutapata magari ya kutumia kwa maana hapa yanaitajika magari si chini ya matatu”

“mumezungumza na huyo babu?”
“nani?”
‘si huyo dokta”
“fetty ndio alikuwa akizungumza naye kabla ya ajali,ngoja”
Anna akatoa simu yake mfukoni na kumpigia dokta william
“anna mbona mmekuwa wazembe kiasi hicho?”
Sauti ya dokta william iisikika kwenye simu baada tu yakuipokea

“badala ya kutuuliza tunaendeleaj,wewe unajidai ukituambia kuwa sisi ni wazembe.Si ungeifanya kazi yako wewe mwenyewe?”
Anna naye alizungumza kwa hasira
“hata kama sijawafundisha hivyo,nyinyi mlitakiwa mtumie akili”
“akili ehhee”

Halima akampokonya anna simu na kuiweka sikioni mwake
“nisikilize wewe mzee kwa umakini,sisi hatukuwa na la kufanya zaidi ya kufanya kile tulicho kifanya.Sasa ni hivi tunakupa masaa mawili uje huku ukiwa na jibu ni wapi alipo pelekwa fetty la sivyo......Utaisoma namba kama ni ya kirumi,kichina au kimakonde.”

Halima akaikata simu na kumrudishia halima.
“jamani,mimi nimechoka ngoja nijipumzieshe”
Agnes alizungumza na kuingia ndani kwake.Anna na halima wakabaki wakiwa amejilaza kwenye masofa,kila mmoja akitafakari kitu cha kufanya akilini mwake

Asubuhi na mapema dokta william akawasili kwenye handaki.Hadi anaingia hakuna aliye msalimia zaidi ya kutazamwa kama kinyago
“habari yenu”
“salama”
“ehee agens vipi kazi ya tanga mmeifanikisha?”
“ndio ila kwa shida kubwa”
“ehee na nyinyi?’
“kwani hujui”

Anna alijibu kwa dharau huku akitafuna taratibu popkone zilizopo kwenye kifuko.Dokta william akashusha pumzi nyingi huku akiwatazama halima na anna.
“fetty yupo katika hospitali ya taifa muhimbili,ila yupo chini ya unagalizi mkubwa wa madaktari na askari wenye silaha kali”
“tutampataje?” anna aliuliza
“kikubwa ni kusubiri siku ambayo atasafirishwa kupelekwa gerezani
“alafu.....”

“ndio tunaweza kufanya harakati za kumuokoa”
“dokta hivi unadhani,mwezetu atajisikiaje.Kama atakaa hospitali mwaka basi tusubirie tuu?” anna alimuuliza dokta william huku akimtazama kwa macho makali
“sijamaanisha hivyo....”
“kwani hapa ulisemeje? Si umesema hadi siku atakayo pelekwa hospitali ndio tukamuokoe au?”
“anna kuwa mpole,”
“sio niwe mpole.Fetty kwetu ni muhimu sana kuliko unavyo fikiria”

“oya anna kausha mwanagu tumsikilize dokta atakacho kizungumza,kupanick haisaidii kitu” rahab alimkanya anna na akakaa kimya
“sikilizeni,fetty anataokolewa kesho hospitalini.Atasafirishwa muda wa saa mbili usiku kupelekwa gereza la segerea”
‘”ngoja kwanza,watapitia njia ipi?”
“kwa njia bado sijafahamu,ila watatumia magari matatu yanayo fanana.Gari moja atakuwepo fetty na gari mbili watakuwepo midoli inayo fanana na fetty”
“sasa hapo itakuwa vipi?”

“muda wote mutawasiliana na mimi,kutokana mimi ndio ninaye shughulika na utengenezaji wa madoli yanayo fanana na fetty”
“je niwapi sisi tutapata usafiri?”
“kuhusiana na hilo wala musijali,kikubwa ni kuwa makini kwa kila jambo na kitu kikubwa ni kujipanga vizuri.Sitaki kutoke tatizo la kijinga”
“sawa”
Dokta william akaondoka zake na kurudi jijini dar es salaam

                                           *****

Gari tatu aina ya gvc zilizotolewa kama msaada kutoka katika serikali ya marekani na kukabidhiwa katika jeshi la polisi nchini tanzania.Zipo tayari nje ya hospitali ya muhimbili kwa ajili ya kumsafirisha fetty ambaye anahesabiwa kama jambazi sugu.Ulinzi mkali unazidi kuhimarishwa kwenye eneo zima la hospitali ya muhimbili kila gari linaloingia na kutoka ni lazima liweze kukaguliwa na askari.

Kuanzia majira ya saa kumi na mbili asubuhi waandishi wa habari wamepiga kambi katika hospitali ya taifa muhimbili kusubiria kumuona fetty ambaye amepata umaarufu katika wakati mchache,hii ni kutokana na mkuu wa jeshi la polisi kutoa siku kumi na mbili za kujisalimisha kwa halima na anna.

Anna,rahab,agnes na halima wapo tayari kwa ajili ya kazi moja tuu,yakumuokoa fetty kutoka mikononi mwa askari.Wote wanne wamevalia nguo nyeusi na viatau vya jeshi vyenye rangi nyeusi.Vifuani wamevalia majaketi ya kuzuia risasi kupenya.Kila mmoja katika suruali yake aliweza kuchomeka magazine zipatazo kumi zilizo jaa risasi za kutosha.Mabomu ya kurusha kwa mkono kila mmoja aliweza kubeba ya kutosha kadri ya mtu alivyo kadiria kuona yanamtosha kwa kazi iliyopo mbele yao.Kila mmoja alachukua bunduki anayo ipenda yeye mwenye.
“kila mmoja yupo tayari?” rahab aliuliza
“ndio”

Kwa pamoja wakaikutanisha mikono yao ya kulia wakiwa wakekunja ngumi huku viganja vyao vikiwa vimefunikwa na gloves ngumu za rangi nyeusi tuu
“kwa umoja tunaweza”
Waliizungumza kauli mbiu yao,inayowafariji kila wanapofanya jambo la pamoja
“jamani msiniache nife usiku wa leo”
Rahab alizungumza huku akiwatazama wezake machoni kwa umakini
“hakuna atakaye kufa,tunakwenda wanne na tunarudi watano” halima aliweka msisitizo

Wakakumbatiana kwa pamoja kisha wakaachiana.Wakaanza kutoka ndani y a handaki lao mmoja baada ya mwengine.Wakazitazama gari tatu zilizopo mbele yao aina ya ferrali zilizo letwa na dokta william alizoziagizia kutoka nchini china.Kutokana na uwezo wa kifedha alio nao dokta william gari hizo ziliweza kusafirishwa kwa haraka na kuingizwa tanzania kwa njia magendo zikipokelewa mpakani mwa kenya na tanzania uliopo mkoani tanga.Kila dereva ambaye aliweza kuzifikisha gari hizo kwenye handaki aliuawa kwa kupigwa risasi dokta william kwa lengo la kuficha siri ya lilipo handaki lao
“hei mnanisikia” 

Anna alizungumza huku akikirekebisha kinasa sauti chake alicho kichomeka sikioni.Kila mmoja akamjibu amemsikia kutokana wote walikuwa na vinasa sauti hivyo ambavyo vinaweza kuwasaidia katika mawasiliano kati yao pamoja na dokta william.Wakaingia kwenye magari yao huku anna akiwa gari moja na agnes.Halima na rahab kila mmoja akiwa ndani ya gari lake.Saa zao za mikononi zinawaashiria ni saa moja na nusu usiku.Na muda uliopangwa kwa fetty kupelekwa gerezani ni saa mbili na dakika tano usiku.

Kwa mwendo kasi wa gari zao wakafika maeneo ya muhimbili na gari zao wakazisimamisha umbali kidogo kutoka lilipo geti la kuingilia hospitaini.Rahab kwa kutumia darubin akaweza kuyaona magari matatu meeusi yakitoka katika geti la hospitali huku mbele yao zikiwa zimetangulia pikipiki tatu za polisi.Gari zote zimefungwa vioo ambavyo ni vyeusi
“mnanisikia mabinti”
Sauti ya dokta william ilisikika katika vinasa sauti walivyo vichomeka masikioni mwa

“ndio”
“sasa sijui mumeshafika eneo la tuukio”
“ndio”
“mumeziona hizo gari zinazo toka?”
“ndio”
“zote zinamidoli,inayo fanana na fetty”
“sasa dokta mbona unatuchanganya sasa”
“tuli,kuna kagari chenye bodi chakavu aina ya taksi kitatoka kama dakika tano zijazo”
“hicho kigari ndipo alipo fetty”
“hapana”
“ila?”

“hicho kina askari wapelelezi wapatao wanne,ambao wao watapita njia za panya kuhakikisha wanakwenda kumpokea fetty maeneo ya kimara na fetty anapelekwa iringa na sio segerea kama tulivyo tarajia”
Anna akashusha pumzi nyingi kila mmoja hakujua kama lengo litabadilika
“hiyo ni plan b iliyo badilishwa muda mfupi kabla ya fetty kupelekwa segerea”
“yeye fetty anatapitishwa njia gani?”
“kuna bomba la maji machafu lililopo chini ya ardhi ndilo atakalo pitishwa fetty,askari waliopo kwenye bomba hilo wapo sita.Na wanatembea kwa miguu”

“duu,na zile gari tatu?”
“zile ni danganya toto.Na zile zote zinakwenda segerea na zitapita njia tofauti.Ninacho waambia mimi kiaminini”
“ni muda gani watatumia hadi kufika kimara?”
“kama lisaa na nusu kutokana wanatumia miguu”
“hiyo nayo ni mpya,sasa ni kimara gani kwa maana zipo nyingi?”

“kikubwa ifwateni hiyo taksi tena kwa umbali mkubwa na ikiwezekana muifwate kwa gari moja tuu ili wasistuke kwani wote waliopo humo ni watu hatari sana”
“tumekupata,baby’s kazi ni kwetu tondokeni” rahab alizungumza na gari zao wakaziwasha na kuondoka kwa mwendo wa kawaida

                                             *****

Hata fetty mwenyewe hakutarajia kama atapitishwa kwenye bomba kubwa la maji machafu,ambalo maji yake yalizuiwa kwa muda ili kuwafanya wao kupita kiurahisi.Fetty akiwa kwenye vazi la kiaskari aliweza kufanana mavazi na askari wanao mshikilia.Tofauti yao iliyopo kati yao ni fetty yeye ni mualifu amefungwa pingu za mikononi na kufungwa cheni nene na ndefu miguuni ila askari wangine watano ni wanaume wenye silaha huku askari mwengine wa kike aliye tengenezwa sura kama fetty na kimo kikiwa ni sawa,ni tofauti sana kwa mtu yoyote kuweza kumgundua.Isitoshe na yeye amefungwa pingu za mikono ila miguuni hakufungwa kitu cha aina yoyote

Harufu ya maji machafu haikuwazudia wao kusonga mbele wakitumia tochi kubwa zilizo wasaidia kuona mbele.Akili ya fetty ikawa na kazi ya kumchunguza mmoja baada ya mwengine na akaapia akipata nafasi yoyote ni lazima ajiokoe kuliko kwenda kunyongwa kisiri kwani ndio mazungumzo aliyoyasikia wakizungumza askari kipindi amelazwa wodini.Gafla fetty akajiangusha na kujifanya amepoteza fahamu,kwa umahiri mkubwa akazibana pumzi zake na kuyafanya mapigo yake ya moyo kupoteza muelekeo.

“bosi tumepata tatizo,over”
Askari mmoja alizungumza kwa kutumia simu ya upepo
“tatizo gani? Over”
“amepoteza fahamu huyu binti,over”
“fanyeni chochote,ila muhakikishe munatoka naye,over”
“sawa mkuu.Over”

Askari mmoja mwenye mwili mkubwa akamnyanyua fetty na kunuweka begani mwake na safari ikaendelea.Fetty akayafumbua macho yake na kuona askari aliye mbeba ndio wa mwisho katika mstari wanao tembea,kwa ustadi wa hali ya juu,fetty akaichomeka mikono yeke katikati ya shingo ya askati,kwakutumia pigu akaanza kumnyonga askari huku akiwa ameninginia kwa nyuma.Mikoromo ya asakri ikawastua wezake waliopo mbele kitendo cha wao kugeuka wakamkuta mwenzo ndio yupo kwenye hatua za mwisho huku macho yake akiwa ameyatoa nje....

Itaendelea.......
Read More
Powered by Blogger.

Hot

© Copyright KAHAMA 24