DC wa Morogoro amefuta vibali vyote vya mikusanyiko isiyo ya lazima

MATANGAZO

MATANGAZO
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Bi.Regina Chonjo ametangaza hali ya hatari katika wilaya hiyo baada ya kupokea tarifa za kiintelijensia za kuwepo matukio ya uhalifu yanayoshabihiyana na vitendo vya ugaidi katika maeneo tofauti ya wilaya hiyo na hivyo kufuta vibali vyote vya mikusanyiko isiyo ya lazima hadi itakapo tangazwa hali ya amani.

Mkuu wa wilaya Bi.Chonjo ametoa tarifa hiyo wakati wa wito wa dharura kwa waandishi wa habari ambapo amewataka wananchi wote wa wilaya ya Morogoro kutoa tarifa katika vyombo vya dola wanapoona watu wasiowafahamu na matukio yanayoashiria uvunjifu wa amani.

Aidha amewataka wamiliki wa vyumba za kulala wageni na kumbi za starehe kuwa makini na wageni wanaoingia na kutoka huku akiwataka wenyeviti wa vjiji,mitaa pamoja na watendaji wote kufanya jitihada za kuwatambua wageni wote walioko katika maeneo yao.

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa wilaya Morogoro wameomba Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi katika kituo cha mabasi cha Msamvu pamoja na maeneo ya sokoni kwani ndiyo maeneo yenye mikusanyiko ambayo haiwezi kuzuiliwa.