Mgogoro Wakulima na Wafugaji Kiteto

MATANGAZO

MATANGAZO
waku vs wafu
Wakulima wilayani kiteto mkoani Manyara wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro wa ardhi baina yao na wafugaji wa kabila la kimasai ili kuepuka umwagaji damu wilayani humo kutokana na wafugaji kulisha mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima kupitia rika dogo la Morani maarufu kama nyangulo.
Wananchi hawa kutoka kata ya Bwagamoyo mtaa wa Jangwani pamoja na wananchi wa kijiji cha Njoro wilayani Kiteto wametoa kilio hicho mbele ya kamati ya ulinzi na usalama chini ya mkuu wa mkoa wa Manyara mara baada ya kamati hiyo kufanya ziara katika maeneo haya na wananchi kupata fursa ya kueleza kero zao .
Dkt Joel Nkaaya Bendera ni Mwenyekiti wa Kamati ya usalama mkoa ambapo amekemea vikali tabia hiyo ya wafugaji kulisha mifugo yao katika mashamba yenye mazao ya wakulima na kuahidi kuchukua hatua kali kwa watakaoendelea na ukiukwaji huo.
Ziara ya kamati hii chini ya mkuu wa mkoa imeandamana na zoezi la uwekaji mawe ya msingi katika miradi mbalimbali wilayani kiteto.