Mrema Awashauri Watanzania kutoshiriki UKUTA Septemba Mosi
Wananchi wameshauriwa kutoshiriki maandamano ya Chadema yanayoitwa Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta) yatakayofanyika Septemba Mosi.
Baadhi ya viongozi wa siasa wametoa ushauri huo akiwamo Spika wa zamani wa Bunge, Pius Msekwa aliyezungumza katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) akiwataka Watanzania kuacha kufuata mkumbo wa kisiasa.
“Ni tabia ya Watanzania kushabikia mambo wasiyoyafahamu ilimradi yanawafurahisha masikioni au machoni mwao, hata huko mitaani wanakimbilia ngoma bila ya kujua inatokea wapi au inaelekea wapi. Hivyo nawasihi wawe makini na mbinu za siasa zinazotumiwa na baadhi ya vyama kwa kuwa nyingine zina madhara ndani yake,” amesema.
Mwenyekiti wa Bodi ya Msamaha kwa Wafungwa (Parole), Augustine Mrema amesema hakuna haja ya kufanya maandamano hayo kwani hayana faida kwa Taifa kwa kuwa wananchi wa kawaida ndio watakaoathirika.
No comments:
Post a Comment