RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 33 & 34 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )
Mtunzi:EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA....
“Duu kweli malipo ni hapa hapa duniani?”
“MAMA YAKO NI KATILI SANA TENA ZAIDI YA SANA JAPO USONI MWEKE NI MWAMA KUPITILIZA”
Maneno ya baba yakanicha mdomo wazi huku nikishangaa nisijue ni kwanini amesema mama yangu ni katili sana
ENDELEA...
Nikaendelea kumtazama baba kwa macho ya mshangao
“Mama yako ni katili sana kiasi kwamba aliyaaribu maisha yangu kwa kiasi kikuwa....Kipindi ambacho wewe bado hujazaliwa tulikuwa tunapendana sana na kaka yangu na kwajinsi tulivyokuwa tunapenda tuliamini kwamba hakuna kitu amaco kitaweza kutuchonganisha...Ila ninanakumbuka kipindi baba yaka anaingia jeshini mimi nilifeli majaribio kutokana kipindi kile nilikuwa ninaumwa na ugonjwa wa miguu”
“Basi baba yako akaja kukutana na mama yako na kutokana kipindi kile sisi tulikuwa ni fukara sana na wazazi wetu walisha fariki ikabidi kaka ambaye nilisha zoea kumuita kurwa aliniomba nihamie kwa mama yako amaye kwa kipindi kile alikuwa ni daktari ila kwao walikuwa ni matajiri sana kwahiyo swala la pesa kwake lilikuwa ni la kawaida......
Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 1991 ambapo mama yako alianza kujiingiza kwenye mambo ya vyama kwa maana uchaguzi ulikuwa unaelekea miaka ya mbeleni.....Mambo mengi sana akawa ananishirikisha kama mtu wake wa karibu sana kiasi kwamba ikafikia kipindi tukaanza mahusianao ya kimapenzi pasipo kurwa kujua na yeye kwa kipindi kile ilikuwa ni ngumu sana kuweza kujua ukweli kutokana alikuwa yupo kambini kwenye kambi ya jeshi Morogoro na sisi tulikuwa tunaishi Dar es Saalam”
“Kuseme kweli mama yako alimpenda sana kurwa na mimi alinichukulia kama kituliza nafsi.....Ninazungumza ukweli ili uweze kumjua mama yako vizuri na yale yote aliyo nitendea”
Nikabaki kimya huku nikiendelea kumsikiliza baba hata mat yenyewe mdomoni hayakuweza kupita sikujua ni kwanini.
“Basi kipindi alipo gundua amepeta mimba yako na ilipo kuwa na wiki mbili akaanza kutengeneza chuki juu yangu na kipindi kile kwa Tanzania masimu yetu yalikuwa ni yale ya mezani hazikuwepo kama hizi za siku hizi,Alipiga simu kambini na kumuomba kaka kuja nyumbani.Basi baada ya kaka kuja akaanza kuniumiza moyo kwa kufanya mambo yao hadharani huku mimi nikiwashuhudia.......Kitendo cha mama yako kutuchanganya kiliniuma sana na nikaapia ipo siku nitamwambia Kurwa kila kitu kinacho endelea ila kitu ambacho ninakijutia hadi leo ni kwajinsi nilivyo anza kumuambia mama yako kwamba nitamwambia kurwa ukweli wote wa mambo tuliyo yafanya na kipindi hicho tayari ujauzio wake ulisha anza kukua”
“Kitu alicho anza kukifanya mama yako ni kuanza kufanya vitisho vya kutaka kuniua na akaniomba niweze kuondoka Tanzania kama maisha yangu ninayapenda.....Ila kutokana alikuwa na damu yangu tumboni nikawa ninavuta subra niweze kumuona mwanangu amabaye ni wewe....na nililikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwengine ambaye alikuwa amenihifadhi na baada ya mama yako kutambua kuwa ninamwanamke mwengine akatua matu na wakatuvamia sehemu ambayo sisi tunaishi na yule mwanamke....Wa...walimuua kwa kumuingiza chupa sehemu zake za siri na kumkata maziwa na kitendo hicho kilifanyika mbele yangu”
Baba akatulia kimya huku machozi yakianza kububujika kiasi kwamba na mimi kwa mbali machozi yakaanza kunilenga lenga.
“Na mbaya zaidi yule mwanamke alikuwa na ujauzito wangu wa mwezi mmoja na nusu na akafariki na mwanangu tumboni na mimi wakanichoma sindano ya sumu kiasi kwamba sehemu hii yote ya chini ya mwili wangu ikawa haifanyi kazi,pamoja na kinywa changu kikawa kimepinda kwa na sikuweza kuzungumza kitu cha aina yoyote...Basi ninakumbuka kuna daktari wa kizungu alikuwa ni rafiki yangu sana aliweza kunisaidi na kwake kulikuwa ni huku Africa kusini....basi nilipo muelezea kuhusiana na yaliyo nikuta akaamu kunileta kuhu Afrika kusini ambapo nilifanyiwa upasuaji na ikawalazimu kunikata miguu yote miwili na kutokana yule mzee alikuwa na pesa sana akaamua kunichongeshea miguu ya bandia ambayo ni kama hii unayo iona”
Baba akanifunulia suruali yake na kuiona miguu yake ya chuma ikifanana kama ya mwanariadha maarufu Afrika kusini ambaye naye ana miguu ya namna hii,machozi yakaanza kunimwagika huku yakiambatana na maumivu makali ya moyo.
“Basi nilianza kufanya kazi kwa yule mzee na kipindi anafariki hakuwa na mtoto wala ndugu na mali zake zote aliniridhisha mimi na ndio maana unaniona nina mali nyingi kiasi hichi.....Hayo nileyo kueleza ni machache ila kuna mengi sana ambayo mama yako alinifanyia ila kutaoka upo hapa nitakuwa ninakuadisia kila muda utakavyo kuwa unakwenda”
Baba akatoa kitambaa mfukoni mwake na kunipatia na kuanza kujifuta machozi ambayo yananimwagika na nikabaki nikiwa sina cha kuzungumza kwani sikuweza kuamini kama mama anaweza kumfanyia ukatili mtu aliye mbebea damu yake tumboni.
Baba akasimam na kuisogelea meze iliyo jaa mizinga ya pombe kali kisha akachukua mzinga mmoja na akamimina kiasi cha kidogo cha pombe kwenye glasi kisha akapiga fumba moja la pombe hiyo huku akiikunja sura yake akionekana kuwa kitu anacho kinywa ni kikali sana kisha akaviweka mezani na kurudi sehemu aliyokuwa amekaa kisha akashusha pumzi nyingi
“Eddy nilikutafuta sana mwanangu kupitia sehemu mbali mbali hususani mitandano ya kijamii ila kitu ambacho kilikuwa ni kigumu ni kuto kulifahamu jina lako.”
Nikaanza kuyaamini maneno ya baba kuwa mama anaroho mbaya kutokana na jinsi alivyokuwa akimkataa Manka na kutaka kumsweka gerezani kwa kunipiga risasa na kitu kingine nilicho kikumbuka ni maneno ya yule dereva taksi ambaye nilipata naye ajali.
“Haaa huyu mama naye yupo.....Kweli Mungu hapendi dhambi kuna siku bwana alikuwa na dereva wake sasa kwa bahati mbaya nikamchomekea kwa mbele ile barabara ya kuingilia K.C.M.C nilikuwa namuwahisha mgonjwa hospitalini.Ahaaaa alikwenda kunilaza polisi hadi siku anaondoka Arusha ndio wakaniachia......Tena hao watekaji kama wanajua wamfanye wa kwanza kufa kwa maana yule mama roho mbaya sana”
Baba akanisogelea na kunishika bega na kuniomba ninyanyuke kisha akaniweka vizuri shati langu na kuniomba twende nje.Akaanza kunitembeza kwenye eneo la jumba lake la kifahari na kwaharaka haraka utajiri wa baba ni mara tano ya utaji alio nao mama.
Ila moyoni mwangu sikuweza kuiruhusu chuki iliyopo kati ya wazazi wangu kunitawala moyoni mwangu ila chuki yangu kwa sasa ilibaki kwa baba mkubwa ambaye amemtekana mama akisaidia na Emmy mwanamke aliye jitambulisha kama daktari.
No comments:
Post a Comment