Tanzia: Msanii wa Nyimbo za Asili "Nyanda Madirisha" Afariki Akijiandaa Kufanya Show Huko Simiyu..Tazama Video Zake Hapa
Pikipiki iliyoondoa uhai wa msanii Nyanda Madirisha
Gari la Msanii Nyanda Madirisha alilokuwa anatumia kufanyia show zake enzi za uhai wake.
Msanii wa nyimbo za asili kutoka Kahama mkoani Shinyanga maarufu kwa jina la Nyanda Madirisha amefariki dunia kwa ajali ya pikipiki mkoani Simiyu alipokwenda kufanya show zake.
Malunde1 blog imeambiwa kuwa Msanii maarufu Nyanda Madirisha amefariki dunia leo Jumamosi Agosti 06,2016 mchana wakati akitoka kununua mafuta ya petrol kwa ajili ya jenereta analotumia kufanyia show zake kwenye gari lake ambapo alitakiwa kufanya show siku ya Jumapili Agosti 07, 2016 katika eneo la Shinyanga Mwenge katika wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.
“Alikuwa anatoka Lalago kuchukua mafuta ya petrol sasa wakati anatoka kuchukua mafuta hayo pikipiki ikamshinda na kumwangusha katika eneo la Mision ya Gula ambapo kuna kona akafariki papo hapo..show ya mbele ya pikipiki imenyofoka na hatuelewi sijui ameikosa kosaje hiyo kona”,mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ameiambia Malunde1 blog.
“Huenda kifo chake kimesababishwa na ulevi kwa sababu amekutwa na chupa za bia na viroba,pengine kutokana na kulewa ndipo pikipiki ilimshinda na kusababisha kifo chake papo hapo”,aliongeza shuhuda mwingine wa tukio hilo.
Malunde1 blog inawapa pole ndugu,jamaa na marafiki wakiwemo wapenzi wa nyimbo za asili kwa msiba huu.
Pumzika kwa amani Nyanda Madirisha.
Nimekuwekea hapa baadhi ya nyimbo zake hapa chini alizowahi kufanya enzi za uhai wake ...Play kuona video zake kali zilizobeba ujumbe mzito imo aliyojitabiria kifo
1.Wimbo unaitwa matukio kutoka kwa msanii Nyanda Madirisha
2.Nyimbo inaitwa Shikolo kutoka kwa msanii Nyanda Madirisha
4.Wimbo unaitwa Ngoshi Wane wa Nyanda Madirisha akishirikiana na Ng'wana Mazuri
No comments:
Post a Comment