Utafiti wa Zao la Mahindi

MATANGAZO

MATANGAZO
mahndshambnmzr-620x308

Utafiti uliofanyika katika zao la mahindi hapa nchini umeonyesha kwamba kumekuwa na upotevu mwingi wa mahindi wakati wa
uvunaji kutokana na wakulima wengi kukosa ushauri wa kitaalam kutoka kwa maafisa ugani.

Utafiti huo uliofanyika katika wilaya ya Mbozi na shirika la chakula duniani FAO, ulionyesha kwamba asilimia 30 ya mahindi hupotelea shambani wakati wa uvunaji .
Utafiti huo umetolewa na Zalam Tadesse ambaye amemwakilisha mwakilishi mkazi wa FAO nchini katika mkutano uliomhusisha pia mkurugenzi msaidizi mipango na bajeti kutoka wizara ya kilimo,mifungo na uvuvi David Biswalo

Amesema FAO itaendelea kushirikiana na serikali katika kuwafikia wakulima wengi hususani wa pembezoni ili kuwapatia ujuzi wa uhifadhi wa chakula na ushauri mwingine wa kilimo cha kisasa.

Mkurugenzi msaidizi mipango na bajeti kutoka wizara ya kilimo,mifungo na uvuvi David Biswalo ameshauriwa wakulima kufuata ushauri wa maafisa ugani sehemu wanazoishi ili kuokoa mazao hayo ya mahindi yanayopotea shambani.