Wema Sepetu: Sirudi Tena Dar

MATANGAZO

MATANGAZO
Malkia wa filamu Wema Sepetu amelikimbia jiji la Dar es salaam na kuamua kuanzisha makazi mapya mkoani Arusha kama alivyodai mwenyewe.

Mwigizaji huyo ambaye kwa sasa yupo mkoani Arusha ameonyeshwa kuvutiwa na jiji la Arusha na kuamua kuwarusha roho mashabiki wake kwa kuwaambia kwamba hatarudi tena Dar es salaam.

“My shouger nikimpenda hovyooo, kweli watu tumetoka mbali, huyu ndiye atakayenifanya nihamie Arusha kwakweli,” aliandika Wema katika picha hiyo hapo juu akiwa na rafiki yake.

Kadhi siku zinavyozidi kwenda mrembo huyo anaonyesha kuendelea kuvutiwa mji wa Arusha.

“Nirudie nini Dar mie, kurudi Dar majaliwa, na sirudi Dar ng’o,” aliandika Wema katika ujumbe wake wa pili.

Hata hivyo uwamuzi huyo umepokewa tofauti na baadhi ya mashabiki wake katika mitandao ya kijamii.

Haya ni maoni ya baadhi ya mashabiki wake.

Hopeolivier24
Dar bila Wema Itawezekana kweli? Itakuwa manispaa maana jiji unaliamishia ArushaπŸ˜€πŸ˜€

Zai_miss
Kwaiyo ushahamia arusha jamani khaaaa vigoma vyako itakuwaje My mmmh ila umefanya lamaana maana bongo kwa moto arusha Baridi kisheziπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Theonerealdully
Utarudi tuu. Watu wa dar miji mingine hamuiwezi hekaheka zenu na mafoleni mwayapenda hivyohivyo

Andymsalali
jamn kwann, rudi bhana, tumekuzoea wenyew kukuona dar

Zeyaabdallah
Wema Rudi home coz matatizo hayakimbiwi dadaangu mpenz Wang.sawa Bali unatakiwa uyakabi

Bongo5