Ushahidi wa awali kwa watuhumiwa wawili wa kulawiti watoto 14 mkoani Singida Daud Idd na Abdallah Yahaya tayari umewasilishwa kwa mwanasheria wa serikali

MATANGAZO

MATANGAZO
Ushahidi wa awali kwa watuhumiwa wawili wa  kulawiti watoto 14 mkoani Singida Daud Idd na Abdallah Yahaya tayari umewasilishwa kwa mwanasheria wa serikali kanda ya Singida ili kuweza kuandaa hati ya mashtaka.

Hilo limethibitishwa na Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Singida Mratibu Mwandamizi wa Polisi Costantine ambaye amesema hatua za awali za kufanya uchunguzi baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa walalamikaji ambao ni wazazi wa watoto, umekamilika na kinachosubiriwa ni Mwanasheria kuandaa hati ya mashtaka.

“Tayari jeshi la polisi limeshakusanya ushahidi na kuukabidhi kwa mwanasheria wa serikali kanda ya Singida ili aupitie na akiridhika nao kwamba unajitosheleza kwaajili ya watuhumiwa kufunguliwa kesi basi mara moja watuhumiwa watafikishwa mahakamani”, amesema Kamanda Costantine.

Daudi Idd (74) ambaye ni mganga wa kienyeji pamoja na Abdallah Yahaya (31) ambaye ni mtoto wa mdogo wake wanadaiwa kuwalawiti na kuwabaka watoto 14 kwa nyakati tofauti kati ya Disemba mwaka jana, hadi Oktoba mwaka huu.

Watuhumiwa hao walikamatwa Oktoba 16 mwaka huu baada ya mtoto mmoja wa miaka 7 kulalamika kuwa anasikia maumivu makali katika sehemu yake ya siri alipokuwa akiogeshwa na mama yake ndipo mama huyo akachunguza na kubaini kuna michubuko inayotokana na kuingiliwa kimwili ndipo akaripoti Polisi.