Wabunge Upinzani Wakacha Bunge

MATANGAZO

MATANGAZO
Wabunge wa upinzani wakiwamo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ni kama wamesusia Mkutano wa 11 wa Bunge ulioanza vikao vyake mjini Dodoma jana huku viti vyao vikionekana vitupu.

Aidha, kutokana na kutokuwapo bungeni kwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), swali laki ilibidi liulizwe na Mbunge wa Liwale, Zuberi Kuchauka (CUF).

Wabunge hao wameshindwa kuhudhuria vikao hivyo ambapo jana wabunge waliokuwapo walikuwa wanne tu kutoka Chama cha Wananchi (CUF) na wabunge wawili wa Chadema.

Hata hivyo, leo wabunge wa Chadema hawakuwapo kabisa ambapo baadaye walionekana wabunge wawili tu, akiwamo Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na Mbunge wa Viti Maalumu, Rose Kamili ambao walionekana kwa muda mfupi kwa nyakati tofauti na kupotea.

Kubenea aliingia bungeni asubuhi na kutoka kabla ya kikao kuanza huku Kamili akionekana nje ya ukumbi wa bunge bila kuingia ndani.

Wabunge wa CUF walikuwapo lakini idadi yao ikiwa haifiki 20 wakati wa kipindi cha maswali na majibu na kubaki tisa pekee baada ya kipindi hicho.