Uteuzi mwingine alioufanya Rais Magufuli leo August 21 2016

MATANGAZO

MATANGAZO
Taarifa iliyotolewa na Ikulu leo August 21 2016 imesema kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Gabriel Fabian Daqarro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.
Gabriel Fabian Daqarro anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mrisho Mashaka Gambo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Uteuzi wa Bw. Gabriel Fabian Daqarro unaanza mara moja.