Wasanii Wapenda Amani Waungana Kupinga Maandamano UKUTA Ya Chadema

MATANGAZO

MATANGAZO
WASANII mbalimbali wanaopenda amani wameungana kwa pamoja kupinga maandamano ya UKUTA yanayotarajiwa kufanyika Septemba Mosi, mwaka huu.
 
Akizungumza jana mbele ya Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Wasanii hao wapenda amani, Steve Nyerere alisema hamna haja ya maandamano bali tunahaja ya kufanya kazi hususan kwa vijana.
 
"Vijana ndio muhimili mkubwa kulinda amani ya nchi,tusiwaze maandamano bali tuwaze je Akinamama na Watoto wanapata huduma hospitali"alihoji Steve Nyerere.
 
Kwa Upande wa Makamu Mwenyekiti wa Wasanii hao, Asha Baraka alisema wameamua kupaza sauti zao kwa niaba ya Wasanii wote wanaopenda amani.
 
Alisema Tanzania ni nchi ya Amani sio nchi ya vita hivyo wanapofanya shughuli za UKUTA shughuli zote za kijamii zitasimama.
 
Hatahivyo aliomba Septemba 1,  UKUTA wasimamishe maandamano hayo, pia watafute njia muafaka ya kuweza kuongea Vyama kwa Vyama na wakapata muafaka ili nchi iweze kwenda mbele.