Rais Magufuli ateua Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ndege ATCL

MATANGAZO

MATANGAZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,  tarehe 15 Septemba, 2016 amemteua Mhandisi Emmanuel Korosso kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).


Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi wa Mhandisi Emmanuel Korosso unaanza mara moja.

Mhandisi Emmanuel Korosso anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Salim Msoma ambaye alimaliza muda wake.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Mhandisi Ladislaus Ernest Matindi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).

Kabla ya uteuzi huu Mhandisi Ladislaus Ernest Matindi alikuwa Mkurugenzi katika Shirika linaloshughulikia masuala ya usafiri wa anga Barani Afrika (EGNOS-Africa Joint Programme Office) lenye makao yake nchini Senegal.

Uteuzi huu unaanza mara moja.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

15 Septemba, 2016