Wema Sepetu Atoa Tahadhari kwa Wabaya wake
Madam Wema Sepetu amewatumia ujumbe wa tahadhari wabaya wake wanaomfuatilia anga zake.Ni ukweli usiopingika kuwa Wema amekuwa akihangaika mara nyingi huku na kule ili apate mtoto lakini mambo bado yamekuwa yakienda kombo kwa kuishia kuumia huku baadhi ya watu wakimkejeli kwa matusi wakisahau jambo la kupata mtoto ni neema ya Mungu pekee.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Wema Sepetu ameweka picha ya Blac Chyna mwenye ujauzito inayomuonyesha sehemu yake ya tumbo na kuandika, “Na ningeomba mfunge kweli account zenu ikifika hii hali…. Mxxxxxxiiiuee.”
Mapema mwaka huu ilidaiwa kuwa Wema ana ujauzito wa Idris Sultan lakini baada ya muda walitoa taarifa za kutoka kwa ujauzito huo japo haijajulikana kama ilikuwa ni kweli au ni kiki. Usikate tamaa madam Wema ipo siku machozi yako yatageuka furaha.
No comments:
Post a Comment