Zitto Kabwe Afunguka Kuhusu Upungufu wa Mizigo Bandarini..Adai Madereva 27,600 Wamepoteza Kazi

MATANGAZO

MATANGAZO


Takribani madereva na matingo wa malori 27,600 wamepoteza Kazi tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani

TATOA (Umoja wa Wamiliki wa Magari ya Kusafirisha Mizigo Nchini) unamiliki Wastani wa Malori 23,000 Kwa sasa. 60% ya Malori Husika Kwa sasa hayafanyi kazi Kabisa Kwa Sababu ya Uhaba wa Mizigo Bandarini.

Kila gari Moja hutumia Wastani wa Lita za Mafuta 2000 kutoka Bandari ya Dar es salaam Kwenda Burundi, Zambia ama DRC. Ambapo Magari yote 23,000 hutumia Lita Milioni 46 Kwa Safari Moja katika Nchi Tatu Hizo, Na Serikali hukusanya Shilingi 650/- Katika Kila Lita Moja ya Mafuta Kama Kodi.

Kwa Msingi Huo Ukifanya Mahesabu Utaona Athari Za kushuka Kwa Mizigo Katika Bandari ya Dar zinavyosambaa Kutoka Bandarini, Kwenda TRA, Kisha Kwa TAFFA (Umoja wa Mawakala wa Mizigo Nchini), kuja kwetu TATOA, Kwenda TASAA (Umoja wa Mawakala wa Meli Nchini) mpaka Kwa ICDs (Umoja wa Wamiliki wa Bandari Kavu Nchini)".