Mkurugenzi NEC: Matokeo ya Rais Hayawezi Kuhojiwa Popote, Labda Tubadili Katiba

MATANGAZO

MATANGAZO
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Tanzania Kailima Ramadhani, amesema kitendo cha kuweza kushtaki mahakamani na kupinga matokeo ya urais kama ilivyofanyika Kenya, nchini Tanzania haitawezekana kutokana na sheria zake za uchaguzi.

Kailima ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba sheria za Kenya zinaruhusu jambo hilo, lakini hapa kwetu litawezekana tu iwapo katiba ya nchi itabadilishwa.

“Wao wametekeleza ile kazi kwa mujibu wa sheria za Kenya, na sisi tunatekeleza majukumu yetu kwa mujibu wa sheria zetu, huwezi kufanya kitu ambacho kwenye katiba yako hakuna, lakini kwa katiba ya Tanzania inasema matokeo ya Rais hayawezi kuhojiwa, kabadilishe katiba lete hilo jambo tutakwenda”, amesema Bwana Kailima.

Hivi karibuni Tanzania kunatarajiwa kufanyika chaguzi ndogo ndogo, kwa mujibu wa sheria za nchi na serikali za mitaa, ambazo pia zinasimamiwa na Tume ya Uchaguzi.