Waziri acharuka kuwekwa ndani watumishi wa afya

MATANGAZO

MATANGAZO


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amekemea vitendo vya kuwaweka ndani watumishi wa afya bila kufuata utaratibu vinavyofanywa na wakuu wa wilaya na mikoa.

Amesema hayo leo Jumatano Oktoba 25,2017 katika kongamano la afya.

Mwalimu amesema makosa ya kitaaluma hayapaswi kumweka daktari au mtumishi wa afya ndani, bali anatakiwa kupelekwa kwenye baraza la madaktari.

"Juzi (Oktoba 23,2017) nimepigiwa simu daktari amewekwa ndani sababu mtoto amefariki dunia, nilishasema wakuu wa wilaya na mikoa msiingilie masuala ya utaalamu, wapelekeni baraza la madaktari. Ila akipatikana daktari amelewa, amepokea rushwa, mzembe awekwe ndani," amesema Mwalimu.

Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Obadia Nyongole amesema ni vyema Serikali ikaweka mfumo wa kuratibu utoaji huduma nchi nzima.