Polisi Msiogope Kutumia Nguvu kwa Wahalifu

MATANGAZO

MATANGAZO

nchemba
Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Chemba amewaasa wananchi kutiii sheria na kujiepusha na vitendo vya viovu huku akilitaka jeshi la Polisi lisiogope kutumia nguvu wakati wa kukabiliana wahalifu wanaofanya mauaji na kuvuruga amani ya nchi.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na askari wa vikosi mbalimbali vilivyopo chini ya wizara mambo ya ndani wakati wa ziara yake mkoani hapa .
Amesema katika siku za karibuni kumezuka tabia ya baadhi ya makundi kushawishi wananchi kuvunja sheria na mengine kushabikia vitendo vya mauaji na uhalifu mbalimbali unaofanywa hapa nchini ambao unavuruga amani na kulitaka jeshi la polisi kuwachaukulia hatua wahusika wote.
Aidha ameagiza wananchi kushirikiana na jeshi la Polisi kufichua uingizwaji wa bidhaa za magendo, wahamiaji haramu na kukomesha uuzaji wa dawa za kulevya kwa kutoa taarifa zitakazofanikisha kuwakamata wauzaji wa rejereja ambao ndio chanzo cha vijana kuharibika na kujiingiza katika vitendo uhalifu.
Awali akisoma taarifa kwa waziri Kaimu Mkuu wa mkoa wa Tanga ambaye ni mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe, amesema hali ya ulinzi na usalama katika mkoa wa Tanga imeimarishwa na eneo ambalo lilikua limevamiwa na wa halifu huko amboni limedhibitiwa.